Ole Sabaya asomewa mashtaka mapya 5 ya uhujumu uchumi. Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha yapewa mamlaka kusikiliza kesi

Ole Sabaya asomewa mashtaka mapya 5 ya uhujumu uchumi. Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha yapewa mamlaka kusikiliza kesi

Wale waliodai huyu mtu atachomoka basi kama kweli atachomoka na kesi zote hizo nitaamini kweli uchawi upo.
Huoni kwamba wamizikusanya zote kwa pamoja ili wazibutue once and for all.....tafakari brother
 
Kwa kweli! Mbona kama tuliambiwa utetezi/ushahidi ulikamilika na tunasubiri hukumu tarehe 1 Oktaba. Imekuwaje tena?
Hiii ni keai nyingine tofauti na ile muwe mnaelewa.. ile inasubiri hukumu hii ni mpya imeanza
 
tatizo ni kuwa wale waliokuwa mashahidi wa kubakwa na kulawitiwa waliingia mitini kwahiyo unavyoona hizi mza uhujumu uchumi hazina nguvu?
Atafakari nini? Ile nyingine inasubiri hujumu hii ndio imeanza huoni tofauti?!
 
09 September 2021
Mahakama ya Hakimu Mkazi
Arusha
Tanzania

SABAYA ASOMEWA MAKOSA MAPYA MATANO "ALICHUKUA MILIONI 90 KWA MFANYABIASHARA"

Aliyekuwa mkuuu wa wilaya ya hai Lengai Ole Sabaya na wenzake sita wamesomewa shtaka la uhujumu uchumi lenye makosa matano kwa madai yakuchukua million 90 kutoka kwa mfanyabiashara ili wasimchukulie hatua kwa kosa la ukwepaji wa kodi.

Ole Sabaya na wenziwe wakituhumiwa makosa ya uhujumu uchumi, unyang'anyi wakutumia silaha na utakatishaji fedha.

---
DPP aipa mamlaka Mahakama Hakimu Mkazi kusikiliza kesi ya Sabaya na wenzake

Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) imeipa mamlaka Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, kusikiliza kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake.

Ole Sabaya na wenzake wanakabiliwa na mashitaka matano ikiwemo kujihusisha na rushwa na utakatishaji fedha haramu Sh90 milioni.

Ofisi ya DPP imewasilisha hati ya kuipa mamlaka mahakama hiyo, leo Alhamisi Septemba 9, 2021 kupitia Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tarsila Gervas wakati kesi hiyo ilipofikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa.

Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ya Uhujumu Uchumi namba 27, 2021 ni Enock Mnkeni, Watson Mwahomange, John Aweyo, Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya.

Mbele ya Hakimu Mkazi, Patricia Kisinda, Wakili Tarsila ameieleza Mahakama kuwa DPP ametoa hati na ridhaa hiyo ya mahakama hiyo ya chini kusikiliza kesi hiyo.

"Mahakama Kuu ndiyo yenye mamlaka ya kusikiliza kesi hii, ila DPP chini ya Kifungu cha 12(3) cha Sheria ya Uhujumu Uchumi ameona kwa maslahi mapana ya Taifa shauri hili lisikilizwe mahakama hii ya chini.

“Tutaanza kuwasilisha hati hizi alizotoa DPP na kwa kuwa Mahakama imekuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi hii ni rai yetu kuwasilisha hati ya mashtaka na kuwasomea," amesema.

Baada ya Mahakama kupokea nyaraka hizo Wakili huyo aliwasomea upya mashitaka matano yanayowakabili ambayo ni kuongoza genge la uhalifu, kujihusisha na kitendo cha rushwa, matumizi mabaya ya madaraka na utakatishaji fedha haramu Sh90 milioni, makosa ambayo washitakiwa hao walikana kuyatenda.

Kati ya makosa hayo matano, Sabaya peke yake anakabiliwa na makosa matatu ambayo ni kujihusisha na kitendo cha rushwa, kujihusisha na vitendo cha rushwa na kuchukua rushwa Sh90 milioni kutoka kwa Francis Mrosso na matumizi mabaya ya madaraka akiwa DC.

Mengine ni kumtishia Mrosso kuwa atamfungulia mashtaka ya kukwepa kodi kitendo ambacho ni kinyume na sheria kwa lengo la kujipatia fedha ya Sh90 milioni.

Baada ya kusomewa mashitaka hayo na kuyakana kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 13, 2021 ambapo watasomewa hoja za awali za kesi hiyo.

Chanzo: Mwananchi
Kwa Ccm hilo ni jambo la kawaida. Sifa kuu ya kuwa kiongozi Ccm ni uwe mwizi jambazi.
 
Back
Top Bottom