Ole Sabaya asomewa Mashtaka Sita (6) kwa Uovu aliotenda Hai. Aenda Rumande hadi Juni 18

Ole Sabaya asomewa Mashtaka Sita (6) kwa Uovu aliotenda Hai. Aenda Rumande hadi Juni 18

Ebhana kwa mtu anayejielewa na kujitambua unapopewa nafasi ya kiuongozi kubwa kama iyo inafaa kuishi vizuri na watu na pia kuacha hii tabia ya kuvimba hii ni aina moja wapo ya kitu kinachotuponza sana vijanq sio tu pale tunapopata nafasi kubwa ya mamlaka bali ata pia pale vijana tunapofanikiwa kupata kipato kikubwa sana katika umri wa ujana mara nyingi huwa tunakitumia kipato chetu kama fimbo ya kuwachapia wengine tujifunze na kujirekebisha
True thus Mungu kawanyima waafrika mali sababu ya kujitutumua, we check blacks wakiwa na mali fully ushamba sio USA wala afrika check ushamba wa mayweather, tyson, haspup, ginimbi, nk ni nadra Sana kukuta whites wakishambika na mali
 
Kabaki pekee yake aliyemfurahisha yupo kuzimu anapiga push up.
Hii dunia ikanyage taratibu.
 

Attachments

  • VID-20210604-WA0034.mp4
    1.7 MB
Nimesoma maoni mitandaoni na nimeona kuna idadi kubwa ya watu wakishangilia na kushabikia ama kutamani wafungwa wambake jamaa. Kwa maoni yangu huu ni ukatili na unyama. Siyo poa kuombea mwenzako apate mateso, sembuse abakwe? Hapana ndungu zangu. Tuwe na utu na tujitengenezee fikra za upendo zaidi ya chuki kwa bidamu wenzetu hata kama wao waliishi kama mashetani.
 
Naomba tu MUNGU asaidie kwenye hili kusiwe na chenga chenga,wala bla bla Ole Sabaya afungwe miaka isiyopungua 30. Akae mahabusu kwanza miaka 8,halafu ndio waje msomee hukumu miaka 30
 
Nimesoma maoni mitandaoni na nimeona kuna idadi kubwa ya watu wakishangilia na kushabikia ama kutamani wafungwa wambake jamaa. Kwa maoni yangu huu ni ukatili na unyama. Siyo poa kuombea mwenzako apate mateso, sembuse abakwe? Hapana ndungu zangu. Tuwe na utu na tujitengenezee fikra za upendo zaidi ya chuki kwa bidamu wenzetu hata kama wao waliishi kama mashetani.
Yeye aliwapa watu wangapi mateso? amewaachia watu wangapi makovu? Wacha avune alichopanda
 
sheria haitambui hivyo. its ethier ww ni muhalifu na unastahili adhabu or not. hakuna neutral ground
Nakubali. Aadhibiwe. Nilichokuwa napinga ni watu kushabikia na kumuombea abakwe. Siyo poa kutamani mtu abakwe au afanyiwe vitendo vya kikatili. Kibinadamu hata mimi huwa napata mawazo maovu mengi tu ila natambua kuwa siyo poa na najitahidi kuachana nayo.
 
Mtu wa Hai anaenda kusomewa mashitaka Arusha ili iweje?
Hai hamna mahakama? Na mkoa wa Kilimanjaro je?
Wameogopa mafuriko ya watu mahakamani.

Mahakamani ni sehemu ya kutoa haki kwa hiyo ni vizuri amepelekwa huko ili sasa akina Mbowe wawe wanaenda mahakamani kutoa ushahidi juu ya madai yao.
Mbowe asipoenda kutoa ushahidi mahakamani tutajua ni unafiki tu

Hata Mbowe alikaa Segerea kwa miezi nne na madawa ya kulevya yakaisha mtaani


Mkuu ukifanya kosa Arusha utasomewa ulipofanya kosa mbona hii ni basic za sheria...
 
Aliyekuwa mkuu DC wa Hai amesomea mashaka yake sita UHUJUMU UCHUMI UJAMBAZI KWA SILAHA KUTAKATISHA FEDHA NK AMEKWENDA RUMANDE MPAKA TAREHE 18/6/2021

View attachment 1808139
View attachment 1808140
View attachment 1808141

=======

Aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya (34) na walinzi wake watano wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha wakikabiliwa na makosa mbalimbali likiwemo la uhujumu uchumi, utakatishaji fedha na kupokea rushwa.

Sabaya ambaye alisimamishwa na Rais Samia Suluhu Hassan Mei 13, 2021 kupisha uchunguzi alifikishwa mahakamani hapo akiwa amefungwa pingu na baada ya wote kushuka kwenye magari ya polisi, walitakiwa kuchuchumaa na kisha kupelekwa katika chumba maalum na baadaye kuingizwa mahakamani.

Waendesha mashtaka wa Serikali, Tumaini Kweka, Abdallah Chaula na Tresla Garvas mbele ya Hakimu Mfawidhi, Martha Mahumbuga na Hakimu Mkazi Mkuu, Salome Mshasha wamesema Sabaya na wenzake walitenda makosa hayo Januari 20 na Februari 9, 2021.

Kweka amesema Sabaya na wenzake watano anatuhumiwa kwa makosa ya kuunda genge la uhalifu, uhujumu uchumi, kujipatia fedha kwa njia ya rushwa na utakatishaji fedha ambapo Sabaya alijipatia Sh90 milioni kutoka kwa mfanyabiashara, Francis Mroso mkazi wa kwa Mromboo ambaye alikuwa anatuhumiwa kwa makosa ya ukwepaji kodi ili amsaidie jambo ambalo ni makosa.

Pia, Sabaya na walinzi wake wawili, Sylivester Nyengu (26) maarufu kicheche na Daniel Mbura (38) wanakabiliwa na makosa mawili ya ujambazi wa kutumia silaha wakidaiwa kuyatenda Februari 9, 2021.

Wanadaiwa walimfunga pingu na kumpiga Bakari Msangi ambaye ni diwani wa CCM kata ya Sombetin na kumuibia Sh390,000 na pia katika eneo la Bondeni jijini Arusha wakitumia silaha, Sabaya na walinzi hao wanatuhumiwa kumpiga, kumtishia silaha na kumpora Ramadhani Ayoub simu na Sh35,000.

Kwa kuwa makosa hayo hayana dhamana watuhumiwa hao walipelekwa mahabusu Gereza Kuu la Kisongo na kesi hiyo kuahirishwa hadi Juni 18, 2021.
huyu JAMBAZI aliyekuwa analindwa na MWENDAZAKE leo ni kesi yake hapo ARUSHA, tunasubiri mafaili yake ya MOSHI na Arusha mjini, yapo kwa HAMDUNI.
 
Back
Top Bottom