Ole Sabaya: Rais Samia Suluhu ameleta tumaini jipya katika wakati bado taifa likiwa kwenye maombolezo ya Hayati Magufuli

Ole Sabaya: Rais Samia Suluhu ameleta tumaini jipya katika wakati bado taifa likiwa kwenye maombolezo ya Hayati Magufuli

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
8,018
Reaction score
16,802
Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya amesema kuwa Rais wa sasa wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameleta tumaini jipya katika nchi yetu wakati bado Taifa likiwa kwenye maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati Dkt John Magufuli

"Katikati ya majonzi umeleta tumaini jipya,wakati wa saa ngumu umeinua tena mioyo ya watu kwa faraja ya vitendo, lile swali la 'Itakuwaje sasa' umelijibia Chamwino kwa kishindo, sauti thabiti imedhibitisha kwamba "Hautaruhusu nchi ichezewe na Watanzania wadharaulike".

"Mtakapoiona ishara ya kwanza nanyi mtajua wokovu wenu upo Karibu, Kazi ya kwanza leo imethibitisha udhabiti na namna Rais Samia alivyofuzu kwa viwango vya juu toka kwa mtu uliyemuita Mwalimu na Kaka yako Mwenda zake JPM"

"Namtakia kila la kheri Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan. Sasa ni shwari kuu katikati ya dhoruba. Italazimu kumtambua Simba mpole lakini asiyetaka mzaha" Alisema Sabaya.

Chanzo: #CloudsDigitalUpdates

Kazi yetu Kuu ni Kukushauri tu Madame President ila huyu Mtu ni Mafia ( Intarahamwe ), Mtu wa Fursa ( Opportunist ) na ni Mnafiki ( Hypocrite ) sana hivyo Usimuamini kwani hapo anakujaza tu Upepo ili umuone yupo nawe. Kuwa makini mno.
 
Jambazi namba moja oOe Sabaya. Ingekuwa tunafuata kwa umakini utawala wa sheria, huyu katika list ya watu wa mwanzo mwanzo kutimuliwa na kupelekwa mahakamani ilikuwa huyu ole sabaya. Inatakiwa asiruhusiwe hata kugombea nyumba kumi
 
Hakuna sehemu Sabaya ameikosea serikali. Wapinzani acheni kujiona kama vile mmechukua dola. Hii bado ni serikali ya CCM.
 
Job Ndugai fyekelea mbali, Mwigulu fyekelea mbali, Nape kaa nae mbali, Jafo piga bench.. weka sub huyo 😀😀😀😀
 
Ole Sabaya ni hazina ya uongozi wa nchi hii. Huyu ndio kiboko ya manyani na waganga njaa hana chembe ya mzahanao.
Ni kweli kabisa, lakini kuna simtofahamu nyingi juu yake.
Kuna wengi wamenyanyashwa na huyo Sabaya kiasi cha kuharibu mazuri yake.
 
Back
Top Bottom