Ole Sabaya: Rais Samia Suluhu ameleta tumaini jipya katika wakati bado taifa likiwa kwenye maombolezo ya Hayati Magufuli

Ole Sabaya: Rais Samia Suluhu ameleta tumaini jipya katika wakati bado taifa likiwa kwenye maombolezo ya Hayati Magufuli

Malofa mnaangaika sana na ya CCM ili tusihoji aliko Mbowe.
Sabaya na RPC Kili wako busy wanapiga picha za kumlilia Marehemu Jiwe, tumaini lao. Wakiishamaliza maombolezo watakujulisha.
 
Hakuna sehemu Sabaya ameikosea serikali. Wapinzani acheni kujiona kama vile mmechukua dola. Hii bado ni serikali ya CCM.
Akili yako unadhani mtu akimkosoa Sabaya ni wa vyana vya upinzani.
Huyu jamaa anatukosea hata sisi wenzie.
Isitoshe CCM haimaanishai ndo kiwe na watu wa hovyo.
 
Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya amesema kuwa Rais wa sasa wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameleta tumaini jipya katika nchi yetu wakati bado Taifa likiwa kwenye maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati Dkt John Magufuli....
Kujipendekeza sasa basi!!
 
Sabaya nasikia mikono yake imejaa wafu wasiokifani, nasema nasikia
 
Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya amesema kuwa Rais wa sasa wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameleta tumaini jipya katika nchi yetu wakati bado Taifa likiwa kwenye maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati Dkt John Magufuli

"Katikati ya majonzi umeleta tumaini jipya,wakati wa saa ngumu umeinua tena mioyo ya watu kwa faraja ya vitendo, lile swali la 'Itakuwaje sasa' umelijibia Chamwino kwa kishindo, sauti thabiti imedhibitisha kwamba "Hautaruhusu nchi ichezewe na Watanzania wadharaulike".

"Mtakapoiona ishara ya kwanza nanyi mtajua wokovu wenu upo Karibu, Kazi ya kwanza leo imethibitisha udhabiti na namna Rais Samia alivyofuzu kwa viwango vya juu toka kwa mtu uliyemuita Mwalimu na Kaka yako Mwenda zake JPM"

"Namtakia kila la kheri Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan. Sasa ni shwari kuu katikati ya dhoruba. Italazimu kumtambua Simba mpole lakini asiyetaka mzaha" Alisema Sabaya.

Chanzo: #CloudsDigitalUpdates

Kazi yetu Kuu ni Kukushauri tu Madame President ila huyu Mtu ni Mafia ( Intarahamwe ), Mtu wa Fursa ( Opportunist ) na ni Mnafiki ( Hypocrite ) sana hivyo Usimuamini kwani hapo anakujaza tu Upepo ili umuone yupo nawe. Kuwa makini mno.
Dogo kaanza kujipendekeza
 
Jambazi namba moja oOe Sabaya. Ingekuwa tunafuata kwa umakini utawala wa sheria, huyu katika list ya watu wa mwanzo mwanzo kutimuliwa na kupelekwa mahakamani ilikuwa huyu ole sabaya. Inatakiwa asiruhusiwe hata kugombea nyumba kumi
Hawa vijana wanaishi kijanja janja wanaishi kwa kujitia utahira wa kujikombakomba ili siku zao ziende, wako radhi waue watukane wadhalilishe ili wapate mkate kwa watawala, makonda alisujudu kwa samueli sita baadae kageuka akawa kwa jk, akageuka akawa kwa jpm na kuponda ya kikwete leo baba katutoka ghafla wanapenyeza vikauli vya kujikomba na mapambio kwa mama, style yao ya maisha imekera na kuudhi umma sana....wakafitinisha umma, viongozi na serikali yetu...hadi watu wakaona wamwachie Mungu.....kama ndio yataendelea hivi.....tuone
 
Back
Top Bottom