Ole sio kocha , ni msimamizi wa mazoezi

el nino

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2013
Posts
4,712
Reaction score
5,058


Honeymoon is over..!!!

Mashabiki wa mpira na Duniani na England kwa ujumla walimzodoa sana Mou kwa msimu mmbaya aliokuwa nao wakachochea hadi Mzee wa watu akatimuliwa.


Ole akaja na upepo wake wa muda mfupi, Baada ya upepo wa Ole kukatika sasa ndio tunaona True colours , Ole hajabadilisha chochote kile licha ya kukabidhiwa champions league material team ameigeuza Europa league material team.

Ukiiangalia Man untd imegeuka mzigo wa lawama, leo watasema Mou tatizo licha ya kufanikisha kumaliza nafasi ya pili na Man untd hii hii aliyopewa Ole, kesho watasema tatizo Pogba , Sanchez na Lukaku na kesho kutwa watakwambia Woodward!!!... Kama tatizo lingekuwa wachezaji basi Mou asingemaliza Top 2 na hii timu.

Kwa namna Man United inacheza sasa hivi ni suala tu la muda limebakia na wote tutakubaliana kuwa Ole hakupaswa kuaminiwa na Mou alifukuzwa kimakosa kwa mihemuko tuu, na ukiangalia kwa makini kuna mambo yanashangaza Kama Sanchez kutolewa na Lingaard kuachwa licha ya kutofunga au kutoa assist tangia December , Namaliza kwa kutabiri kuwa Ole atakula Xmass mwaka huu akiwa kwao Norway
 
Sisi mashabiki damu wa man u tunataka ole aongezewe mkataba na mshahara
 
Kama vipi njooni tushabikie timu ya mabaharia pale Merseyside Liverpool.
 
Tutabadilisha makocha sana na tutaendelea kuwa wasindikizaji sana.Napendekeza Ole avumiliwe tu ajenge misingi ya Man Utd tuliyoizoea ambayo hata yeye alikuwa sehemu yake.Hakuna mafanikio ya kufumba na kufumbua.
 
Tutabadilisha makocha sana na tutaendelea kuwa wasindikizaji sana.Napendekeza Ole avumiliwe tu ajenge misingi ya Man Utd tuliyoizoea ambayo hata yeye alikuwa sehemu yake.Hakuna mafanikio ya kufumba na kufumbua.

Misingi gani wakati timu inazidi kuwa mbovu..

Kwa jinsi United ilivyo ni Ngumu sana kushawishi mchezaji yeyote mkubwa kuichezea United , ndio maana inaishia kununua kina Maguire kwa 80 million pounds Wakati upande wa pili Klopp anatumia pesa chache kupata wachezaji Wakali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…