el nino
JF-Expert Member
- Nov 5, 2013
- 4,712
- 5,058
Honeymoon is over..!!!
Mashabiki wa mpira na Duniani na England kwa ujumla walimzodoa sana Mou kwa msimu mmbaya aliokuwa nao wakachochea hadi Mzee wa watu akatimuliwa.
Ole akaja na upepo wake wa muda mfupi, Baada ya upepo wa Ole kukatika sasa ndio tunaona True colours , Ole hajabadilisha chochote kile licha ya kukabidhiwa champions league material team ameigeuza Europa league material team.
Ukiiangalia Man untd imegeuka mzigo wa lawama, leo watasema Mou tatizo licha ya kufanikisha kumaliza nafasi ya pili na Man untd hii hii aliyopewa Ole, kesho watasema tatizo Pogba , Sanchez na Lukaku na kesho kutwa watakwambia Woodward!!!... Kama tatizo lingekuwa wachezaji basi Mou asingemaliza Top 2 na hii timu.
Kwa namna Man United inacheza sasa hivi ni suala tu la muda limebakia na wote tutakubaliana kuwa Ole hakupaswa kuaminiwa na Mou alifukuzwa kimakosa kwa mihemuko tuu, na ukiangalia kwa makini kuna mambo yanashangaza Kama Sanchez kutolewa na Lingaard kuachwa licha ya kutofunga au kutoa assist tangia December , Namaliza kwa kutabiri kuwa Ole atakula Xmass mwaka huu akiwa kwao Norway