Last two fights za Fury nilijua hatatoboa kwa Usyk.
Fury alimpiga Wilder kwa KO lakini hakupata ushindani uliotakiwa, Wilder alikuwa mwepesi na hakuwa na stamina, kuanzia round ya 7 kwenye fight yake na Fury alichoka akawa anasubiri kuangushwa dakika yoyote, na ndicho kilichotokea.
Baada ya pale, Fury akaja kucheza na Ngannou, jamaa aliyetokea kwenye MMA, fight yake ya kwanza kwenye boxing bado aka manage kumuangusha Fury kwa konde moja zito. Japo Fury alikuja kushinda baadae kwa pointi, lakini nilijua tu huyu akija kukutana na bondia anayejielewa lazima apoteze.
Hiki ndicho kilichotokea kwa Usyk, Fury hawezi kumpiga Usyk hata kwenye rematch mwezi wa kumi, naamini bado atapigwa tu, kwasababu;
- Kwanza Usyk ana stamina, ana uwezo wa kumaliza round zote kiushindani, hachoki kizembe.
- Anajua kujilinda, umbo lake fupi anajua namna ya kulitumia pale anapokuwa akishambuliwa, utaishia kumchezea maeneo mengine ya mwili kama mbavu, lakini kichwa chake utakitafuta sana...