Oleksandr Usyk amtwanga Tyson Fury na kuwa Undisputed Heavyweight Champion...

Mabondia wa siku hizi miili imejaa minyama tu, ni aibu!
 
..Tyson Fury ni mrefu kupita kiasi na hiyo ni advantage kubwa.

..kwasababu ni mrefu anatumia jab mkono wa kushoto kushambulia na kujikinga.

..jab ya mkono wa kushoto iko very fast, na mpinzani wake asipoweza kujilinda nayo, au kuikwepa, basi hawezi kumshinda Tyson Fury.

..Na Tyson Fury hutumia jab ya mkono wa kushoto kutengeneza upenyo wa kupiga ngumi ya nguvu zaidi kwa kutumia mkono wa kulia.

..kwa maoni yangu, bondia anayeweza kumshinda Tyson Fury lazima awe na uwezo wa ku-defend, au kukwepa jab. Pia lazima awe na kasi ya kumuingilia na kumjeruhi Tyson Fury mapema.

..Usyk aliweza kumpiga Tyson Fury kwasababu alimuumiza akawa anatoka damu puani. Kitendo cha kutoka damu puani kikapunguza kasi na shabaha / accuracy ya Tyson Fury kutupa jab.

..Nakubaliana na wanaosema Refa alimuokoa Tyson Fury asishindwe kwa Knock Out.
 
Uzani wa juu hauna mabondia siku hizi.Mapambano mengi niyakutafuta pesa tu.Ata hili pambano hakuna ata ngumi za maana zilizopiganwa.Ila ndo dunia ya sasa ilivyo.watu wako kibiashara zaidi.
 
Duh! Nilishangaa raundi ya Tisa Tyson anatupa taulo, refa ndio kamsaidia , la sivyo angepigwa kwa aibu. Alikuwa ameshakubali yaishe. Yule refa mjinga Sana.
Zile jebu alizokula round ya 9 Kwan pambano halikuishia hapo?cz mi nliangalia clips tu
 
Pambano lilipaswa kuisha raundi ya 9 ila refa aliamua kumbeba Fury.

Usyk akija kumpiga Wilder, atakuwa kamaliza kila kitu kwenye Heavy-Weight boxing.
kwa punch alizokula fury, wilder sidhan kama atatoboa huyu mtu wa ukraine anarusha makombora kiroho mbaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…