Mratibu Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Wakili Onesmo Olengurumwa, amemtembelea Padri Dkt. Charles Kitima katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam, kufuatia tukio la kushambuliwa na watu wasiojulikana.
Padri Kitima, ambaye ni mmoja wa viongozi wa dini wanaoheshimika nchini, alishambuliwa siku ya jana na watu wawili waliomvamia akiwa chooni.
Amesimulia kuwa watu hao walionekana awali wakila katika mgahawa wa TEC uliopo ndani ya eneo hilo kabla ya kutekeleza shambulio hilo la ghafla.
Kitima alimwambia Olengurumwa kuwa siku hiyo alikuwa ameitisha mkutano wa viongozi wa dini mbalimbali ili kutafakari ujumbe walioutoa wakati wa Pasaka na Sikukuu ya Eid kwa Serikali. Wakati akiwa kwenye mgahawa ambao upo ndani ya eneo la makazi ya Maaskofu kwenye ndipo tukio hilo lilipotokea.
Shambulio hilo linazua maswali mengi, hasa ikizingatiwa kuwa lilitokea katika mazingira ambayo yalihusisha shughuli ya kidini.
View attachment 3322668