Pre GE2025 Olengurumwa: Kitendo cha kuwanyima haki ya kuchagua na kuchaguliwa Wananchi wa Ngorongoro hakikubaliki kwa wapenda haki

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

informer 06

Member
Joined
May 11, 2024
Posts
66
Reaction score
49
Kufuatia Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), kudaiwa kuviondoa kwenye orodha vituo vya kupigia kura vilivyokuwa kwenye Tarafa ya Ngorongoro na kupelekea hali ya sintofahamu kwa wakazi wa maeneo hayo, Mratibu Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), Wakili Onesmo Olengurumwa amesema kuwa wanalaani suala hilo, ambalo amedai kuwa linawapoka Wananchi haki yao muhimu ya kuchagua na kuchaguliwa.
IMG_5564.jpeg

Akizungumzia sakata hili leo August 3, 2024 siku moja baada ya baadhi ya Vongozi kutoka eneo hilo kujitokeza wazi kutoa tamko la kutokukubaliana na uamuzi huo, Olengurumwa amesema kuwa suala hilo halikubaliki na linaweza kuleta doa kubwa endapo mamlaka husika zitashindwa kulipatia ufumbuzi wa haraka.

"Tumefuatilia na kuona Wananchi katika Tarafa ya Ngorongoro, takribani laki moja na elfu 20 wanakweda kukosa haki yao ya kushiriki kwenye Chaguzi katika eneo lao la Tarafa ya Ngorongoro, maana yake ni sawa na kusema nusu ya Wakazi wa Wilaya ya Ngorongoro wanakweda kukosa haki yao ya Kikatiba ya kuchagua na kuchaguliwa kwenye chaguzi zinazokuja, kinyume kabisa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania"amesema Olengurumwa

Ameongeza kuwa "Tunasikitishwa kusikia hali inayoendelea Ngorongoro imefikia hatua hii. Hili ni tatizo kubwa na yoyote ambaye anazungumzia haki na yoyote muungwana hawezi kulifumbia macho suala hili"

Olengurumwa ananukuu kifungu kutoka kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977), ambacho anasisitiza kuwa kinatakiwa kuzingatiwa 21.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ya 5, ya 39 na ya 67 ya Katiba hii na ya sheria za nchi kuhusiana na masharti ya kuchagua na kuchaguliwa, au kuteua na kuteuliwa kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, ama moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kwa hiari yao, kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria."

Kutokana na hali hiyo ameshauri Rais Samia Suluhu Hassan kuingilia kati suala hilo ambao amesema kuwa endapo likiachwa litakuwa linaenda kinyume na 4R ambazo amekuwa akizizitiza mara kwa mara kama nyenzo anayoiamni katika utawala wake.

"Ushauri wangu kwa Mh. Rais Samia hili suala hasilikubali kabisa kwa namna yoyote litokee, bado anayo nafasi ya kuwaita watu wake na kuwapa maagizo kwamba lisitokee, Watanzania kwenye eneo la Ngorongoro warudishwe waandikishwe na washiriki shughuli za uchaguzi" amesema Olengurumwa

Amedai "Ni suala ambalo linaleta doa kubwa sana katika Chaguzi zijazo lakini katika utawala wake, kwahiyo ushauri wangu kwake asikie kilio cha hao Watu na aweze kuwaita vingozi wa Tume na TAMISEMI waweze kubadilisha hayo maamuzi ili kuepuka kuingia kwenye mitafaruko"

Olengurumwa ameongeza kuwa kutokana na hali ilivyo kwa sasa ya wananchi kubakia na sintofahamu iliyopo, ni vigumu wao binafsi kukubalina na utaratibu huo lakini amesema kuwa suala hilo haliwezi haliwezi kufumbiwa macho na Watetezi wa haki za binadamu wa ndani na hata nje, hivyo ametoa wito kwa mamlaka kutafakari upya hili kepusha hali inayoweza kujitokeza kutoka na uamuzi uliofanyika.

Aidha amedai kuwa tayari kumeanza kujitokeza vitendo visivyo rafiki kutoka kwa baadhi ya maafisa wa vyombo vya dola ikiwemo Jeshi la Polisi kutaka kuwanyima Wananchi Ngorongoro fursa ya kujieleza kwenye jambo ambalo hawakubaliani nalo.

"Lakini tunakemea pia matukio yanayotaka kunyamazisha Watu hao, jana tuliona viongozi wa jamii walitaka kuzungumza kule Arusha, lakini baadhi ya Askari Polisi na usalama walienda kuvamia hoteli waliyotaka kuitumia"amesema Olengurumwa

Hata hivyo amewahasa viongozi wa Ngorongoro kuendelea kudai haki zao kwa kuzingatia taratibu kwa kuwa suala hilo linagusa mstakabali wa maisha yao.

Jana August 1, 2024 Viongozi mbalimbali kutoka Tarafa ya Ngorongoro walitoa tamko wakipinga utaratibu wa INEC kuondoa vituo kujiandikisha na kupiga kura kwenye eneo hilo huku pia wengine kudaiwa kupangiwa Msomera Mkoani Tanga ambalo sio wakazi.

Itakumbukwa Serikali kupitia kauli za viongozi mbalimbali ikiwemo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na vingozi wengine wamekuwa wakisikika wakisema kuwa wananchi katika eneo hilo wanaohama kwa hiari na kuwa wanaobaki hawalazimishwi kuhama wala hakuna anayelazimishwa.

Lakini kumekuwepo na mwendelezo wa taarifa zinazodai kuwa baadhi ya huduma zimekuwa zikisitishwa kwa wakazi waliobakia eneo hilo tofauti na ilivyokuwa awali kabla mchakato wa kuhama haujaanza, hali ambayo imekuwa ikiibua mijadala.
 
View attachment 3060566

Asiishie kulalamika tu na kulaani, aende Mahakamani akafungue Kesi ya kikatiba kwa Hati ya dharula.

"The right cannot be given as a gift by the oppressor, it must be demanded by the oppressed."
Martin Luther King Jr.
 
Martin Luther King Jr yupo sahihi.
 
Back
Top Bottom