Olengurumwa: Ufafanuzi wa Kisheria kuhusu Ardhi ya Loliondo na Ngorongoro

KWENYE GAZETI LA "JAMVI LA HABARI" pia kuna makala juu ya sakata hili

1655102768187.png
 
Kuna mkono wa Kenya mgogoro wa Loliondo.......

Gazeti la Jamhuri April 12, 2022

*Wakenya wajipenyeza hadi ndani ya CCM na kushinda udiwani wakati si raia

*Maslahi binafsi yatawala, wafikia hatua ya kumkashifu Waziri Mkuu hadharani

*Waamini wao ndio wenye turufu kuamua nani awe Waziri wa Maliasili Tanzania

*Seneta wa Narok aishambulia Tanzania bungeni kwao, apinga Loliondo kuhifadhiwa

ARUSHA

Na Manyerere Jackton

Mgogoro wa ardhi unaoendelea katika Pori Tengefu la Loliondo (LGCA) mkoani Arusha ni wa kiuchumi, huku raia na walowezi kutoka Kenya wakiwa vinara wa mgogoro huo.

Ripoti zinabainisha uwepo wa mamia kwa maelfu ya Wakenya katika tarafa za Loliondo na Sale wakiendesha shughuli za ufugaji ng’ombe, mbuzi na kondoo.

Wageni hawa wameigeuza Loliondo na Sale kuwa eneo la kuchunga na kunenepesha mifugo kabla ya kuwauzia wenye viwanda vya kusindika nyama walioko Narok (mpakani na Loliondo) na Nairobi.

Uchunguzi uliofanywa miaka kadhaa iliyopita ulibaini kuwapo kwa mamia ya Wakenya wakiwa na maelfu ya mifugo katika vijiji vya kata za Engaresero, Orgosorok, Oloipir, Oloirien-Magaiduru, Oloosoito-Maaloni na Ololosokwan.

Wakenya hao wamejipenyeza hadi kwenye uongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), na kwenye serikali za vijiji. Ushahidi wa madai haya upo wazi. Baadhi ya Wakenya wameshika hadi nafasi za udiwani kabla ya kuomba na kupewa uraia. Baadhi ya NGOs zinaongozwa na Wakenya na ndizo zimekuwa mstari wa mbele kupinga uamuzi wowote wa serikali.

Lakini mbaya zaidi, kwa siku za karibuni kumejitokeza viongozi wa jumuiya za CCM, wabunge na baadhi ya watu wenye masilahi binafsi kuhakikisha wanakwamisha mpango wowote unaolenga kuilinda Loliondo. Wengine wamejitokeza hadharani kumkashifu na hata kumtukana Waziri Mkuu na viongozi wengine wakuu.

Kutokana na jamii inayoishi eneo la mpakani mwa Tanzania na Kenya kuwa ni ya koo mbili za Loita na Purko; hali hiyo imefanya mwilingiliano uwe rahisi. Ardhi ya Tanzania imekuwa shamba la bibi kutokana na sheria zinazohalalisha rasilimali hiyo kuwa mali ya umma chini ya udhamini wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tofauti na Tanzania, ardhi ya Kenya ni mali ya mtu binafsi, hali iliyowafanya wachache wenye ukwasi wawe wamiliki.

Pale upande wa Kenya unapoona Serikali ya Tanzania ikitaka kuratibu matumizi ya ardhi hasa kwa kutenga eneo la uhifadhi na la matumizi ya vijiji, mara moja upande wa Kenya kupitia viongozi wao mapandikizi na asasi za kiraia (NGOs), husimama imara kuikwamisha serikali.

Oktoba 5, 2017 viongozi wa vijiji na kata, hasa kutoka Ololosokwan walizuru Kenya na kupitia msaada wa Seneta wa Kaunti ya Narok, Ledama Olekina, wakafanikiwa kumuona kiongozi wa upinzani wakati huo, Raila Odinga; rafiki mkubwa wa Rais John Magufuli.

Wakamuomba Odinga amshawishi Rais Magufuli asitishe mpango wa kuhifadhi eneo la kilometa za mraba 1,500. Odinga alikubali kufanya kazi hiyo; na baadaye taarifa zikapatikana kwamba ameshamwambia Rais Magufuli juu ya kilio chao.

Hazikupita siku nyingi aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Jumanne Maghembe, aling’olewa kwenye nafasi hiyo; hali iliyoibua shangwe kubwa.

Ni Ledama huyu huyu ambaye juzi alisimama bungeni kwao Kenya na kuishambulia Tanzania kwa msimamo wake wa kuihifadhi Loliondo. Kwa ufupi Wakenya wanataka Loliondo iendelee kuwa himaya yao ya malisho na huduma nyingine za kiuchumi.

Kabla na baada ya tukio hilo, Wakenya wanaamini kuwa wao ndio wenye turufu ya nani awe nani katika Wizara ya Maliasili na Utalii alimradi tu awe upande wa masilahi yao, hasa kwa kuhakikisha hagusi habari ya Loliondo.

Baadhi ya viongozi waliokwenda na maji ni aliyekuwa Diwani wa Ololosokwan, Yanik Ndoinyo na Mwenyekiti wa Kijiji cha Ololosokwan, Kerry Dukunyi.

Kwa miaka yote tumesema raia wengi wa Kenya wamejipenyeza Tanzania na kujifanya ni Watanzania, lakini ukweli ni kwamba ni Wakenya wanaofanya mambo kwa manufaa ya Wakenya kwa kutumia ardhi ya Tanzania.

Mifugo mingi iliyoko Loliondo ni mali ya Wakenya. Inanenepeshwa Loliondo na baadaye kuuzwa Kenya kupitia minada ya Wasso na mnada mkubwa kabisa uko Posmoru upande wa Kenya.

Wafugaji kutoka Kenya wamevuka kutoka Pori Tengefu la Loliondo hadi kuingia ndani ya Hifadhi ya Taifa Serengeti. Vijiji kama Ololosokwan, Kirtalo, Maalon na Arash ni mfano halisi wa namna walowezi walivyojipenyeza nchini.

Katika kipindi cha Machi na Aprili, 2017, Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya, kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya, Kata na Vijiji ilifanya operesheni kuwabaini walowezi na mifugo yao walioingia kiharamu kutoka Kenya.

Hawa ni wa jamiii zote za Purko na Loita katika vijiji vya Ololosokwan, Kirtalo, Mondoros, Oloipiri, Arash, Olalaa na Piyaya. Idadi iliyopatikana kwa majina na vitongoji walipokuwa wamevamia ilifikia 175 (orodha tunayo).

Hawa watu 175 peke yao walikuwa na mifugo 31,371; ng’ombe wakiwa 15,461. Fikiria, idadi hiyo ya mifugo ya nje ndani ya ardhi ya nchi nyingine huru!

Kisingizio ilikuwa ni ukame mkubwa uliokuwapo maeneo ya kwao, yaani Narok na Kajiado nchini Kenya. Hili la ukame linatumika kama kisingizio lakini ukweli ni kuwa Loliondo ndilo shamba lao!

Tunao ushahidi wa maandishi unaoonyesha namna viongozi wa Kenya wanavyowasiliana na baadhi ya viongozi wa vijiji ili wawaruhusu kuingiza mifugo yao kwa ajili ya malisho.

Kudumu kwa mgogoro wa Loliondo kunatokana na aina ya masilahi hatarishi ambayo yamekuwapo kwa baadhi ya watu wasio na nia njema na taifa letu. Mgogoro huu ulianza kwa mara ya kwanza baada ya kuanzishwa kwa shirika (NGO) la KPOK mwaka 1992.

Shirika hili liliongozwa na Lazaro Parekipunyi. Baadaye zikaanzishwa NGOs za LADO na OSEREMI. Mwanzoni mwa miaka ya 2000 ikaanzishwa Pastoralist Women Council (PWC) na viongozi wake walikuwa marafiki wa Parekipunyi.

NGOs zilikuwa na kazi ya kuwaelimisha vijana wa jamii ya wafugaji kupata elimu, hasa elimu ya sheria ili kufanya kile walichokiita kuwa ni kulinda ardhi yao. Wazo hilo la ‘kulinda ardhi’ lilitolewa na William ole Ntimama ambaye hadi anakufa nia yake ilikuwa kuwafanya Wamasaai wawe na nchi yao (Maasai Land). Mpango huo ungali hai.

Umoja huu wa kuwa na ‘nchi yao’ umezima mgogoro wa kikabila katika tarafa za Sale na Loliondo ambao ulikuwa ukisababisha vifo na maafa mengine.

NGOs za PWC, UCRT, PINGOs, NGONET, PALSEP, RAMAT, TPCF na nyingine nyingi zimeanzishwa na kujipatia fedha nyingi kwa kigezo cha kuwatetea Wamaasai. Japo ajenda yao inaonekana ni ya utetezi, lakini nyuma ya pazia kuna siri kubwa inayobebwa na dhana ya masilahi binafsi ya kiuchumi.

Kuna kiongozi mkubwa wa zamani wa Tanzania akiwa msibani Loliondo, alisema: “Nawapongeza sana Wamaasai kwa kusimamia imara na kuhakikisha ardhi ya Wamaasai haiondoki. Hii ni vita yetu sote na tutashinda, mimi nipo nyuma yenu nafuatilia kwa karibu na tutashinda kwa umoja wetu.”

Kauli hii ilipokewa kwa furaha kubwa na Wamaasai wa Loliondo na wenzao kutoka Narok, Kenya. Mara moja ramani ya eneo la ‘nchi ya Wamaasai’ ikatolewa na kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii. Hapo ndipo ikafahamika kuwa kumbe suala si mgogoro wa ardhi tu, bali ni kujenga himaya ya kiutawala.

Kwa sasa hali ya Loliondo si nzuri. Kumekuwapo hamasa ya chini kwa chini inayofanywa na viongozi wa kisiasa na NGOs kwa ajili ya kuendeleza vurugu kwa nia ya kuivuta jumuiya ya kimataifa ione kuwa wananchi wa Loliondo wanapokwa ardhi yao, jambo ambalo si la kweli.

Ardhi ya Lolindo ya kilometa za mraba 4,000 ni mali ya serikali ndani ya Pori Tengefu. Hakuna ardhi ya kijiji na ndiyo maana Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewahi kusema hakuna Tangazo la Serikali (GN) la kutambua kijiji katika eneo la Loliondo.

Serikali kupitia kwa Waziri wa Maliasili na Utalii mwaka 2013 iliamua kuachia kilometa za mraba 2,500 ili zitumiwe na wana vijiji kwa kupitia mpango wa matumizi bora ya ardhi. Kilometa za mraba 1,500 zikapendekezwa ziendelee kutunzwa kwa sababu eneo hilo ni muhimu mno kwa ikolojia ya Serengeti – Maasai Mara.

Kwanini eneo hili ni muhimu?

Ni muhimu kwa sababu kadhaa:

i) Mosi, ni chanzo cha mito sita inayomwaga maji katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. Asilimia 48 ya maji yanayoingia Serengeti yanatoka ndani ya Pori Tengefu la Loliondo. Eneo hili ni muhimu kwa ikolojia ya Serengeti ikiwa na vyanzo sita vya maji, mapito na mazalia ya wanyamapori.

Pia eneo hili linategemewa na wakazi wa kata saba kama maeneo ya makazi, malisho ya mifugo na upatikanaji wa maji kwa ajili ya shughuli zao za kila siku.

Baadhi ya vyanzo vya maji vilivyomo katika eneo hili:

*Mto Pololeti – vijiji vya Oloipiri, Soitsambu, Maaloni, Arash, Ololosokwan.

*Mto Irmolelian – vijiji vya Piyaya, Arash, Malambo, Maaloni.

*Mto Orgumi – Losoito, Arash, Oloipiri, Magaiduru, Piyaya.

*Vyanzo vya maji vya Lima One – vijiji vya Soitsambu, Oloipiri, Oloirien, Ololosokwan.

*Chanzo cha Maji Mlima Loilale – vijiji vya Ololosokwan, Kirtalo, Soitsambu.

*Chanzo cha Maji Mlima Loili – vijiji vya Ololosokwan, Soitsambu.

ii) Ni sehemu ya mazalia ya nyumbu na pundamilia ambao ni kivutio kikuu cha utalii.

iii) Ni mapito ya wanyama (ushoroba) wahamao kwenye ikolojia ya Serengeti-Maasai Mara.

iv) Pori Tengefu la Loliondo ni eneo la ‘kupumulia’ la hifadhi za Serengeti, Ngorongoro na Maasai Mara.

v) Pori hili ni chanzo kikuu cha mapato kwa serikali kutokana na utalii wa uwindaji na picha.

Mgogoro umekuwapo kwa kuwa NGOs zina masilahi binafsi – zinataka udumu ili ziendelee kuvuna fedha kutoka kwa wafadhili. NGOs. Serikali nayo imekuwa ikikosa utayari wa kuumaliza mgogoro huu mapema licha ya taarifa zote za wataalamu kuonyesha hatari inayolikabili eneo la Loliondo na Ngorongoro.

Baadhi ya viongozi wenye mamlaka ya kutoa uamuzi, ama wamekuwa waoga, au wanazembea kutekeleza mapendekezo ya wataalamu wa uhifadhi na Sheria ya Uhifadhi Namba 5 ya mwaka 2009, na kanuni zake za mwaka 2010. Mfano halisi ni kusuasua kwa uwekaji vigingi vya mpaka katika eneo la kilometa za mraba 1,500 linalopendekezwa kubaki Pori Tengefu.

Nguvu za wafugaji kutoka nchi jirani kutaka waendelee kutumia Loliondo kama sehemu yao ya malisho ni miongoni mwa sababu hizo. Lakini pia kuna taarifa za kiintelijensia za mkakati wa nchi jirani kuua utalii nchini mwetu ili watalii na wawekezaji waende kwao.

Kwanini mgogoro baada ya mwekezaji mpya?

Wizara ya Maliasili na Utalii kwenye taarifa yake ya Desemba 2017 inasema hivi: Tangu kipindi cha ukoloni eneo hili lilitumika kwa shughuli za uwindaji kwa wageni mbalimbali waliokuja nchini.

Kutokana na upatikanaji wa nyara nzuri na kubwa, tena kwa urahisi, serikali ililitumia eneo hili kwa ajili ya kuwindisha wageni wa kitaifa. Shughuli za uwindaji zilifanyika kwa wageni mbalimbali chini ya serikali hadi lilipoundwa Shirika la Wanyamapori Tanzania (Tanzania Wildlife Cooperation – TAWICO) mwaka 1978.

Shughuli zote za uwindaji wa kitalii zilisimamiwa na TAWICO hadi mwaka 1988 zilipokabidhiwa rasmi kwa Idara ya Wanyamapori. Wakati TAWICO ikisimamia uwindaji wa kitalii, eneo la Loliondo liligawanywa katika vitalu viwili; Loliondo North iliyotumiwa na Kampuni ya Safari East Africa Tanzania Ltd na Chasse de Afrique Safaris (ikisimamiwa na Munisi) na eneo la Loliondo South ambalo liliendelea kusimamiwa moja kwa moja na TAWICO.

Kwa kipindi hicho pia Gordon Gordon na mwindaji mahiri (PH) wa Kampuni ya TAWICO, Dan Tarimo, kupitia Kampuni yake ya Dan Tarimo Hunting Safaris, waliendesha shughuli za uwindaji wa kitalii katika eneo la Loliondo chini ya usimamizi wa TAWICO.

Kampuni ya TAWICO na Chuo cha Taaluma ya Wanyamapori Mweka waliwinda katika eneo hilo kwa ajili ya kupata nyara za kutumika katika kiwanda cha nyara cha TAWICO kilichopo Tengeru, Arusha.

Baada ya shughuli za usimamizi wa uwindaji wa kitalii kukabidhiwa Idara ya Wanyamapori mwaka 1988, TAWICO ilijiendesha kama kampuni ya uwindaji wa kitalii na iligawiwa baadhi ya vitalu vya uwindaji ikiwa ni pamoja na vitalu vya Loliondo hadi mwaka 1992 serikali ilipokodisha eneo hilo kwa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ambako ilibidi kuanzisha kampuni ya kusimamia shughuli hizo, yaani kampuni ya uwindaji wa kitalii ya Otterlo Business Cooperation (OBC).

Kampuni ya OBC ilitaarifiwa kuhusu matumizi ya eneo la Loliondo kwa uwindaji kwa wageni wa kiserikali/taifa.

Eneo la Pori Tengefu la Loliondo ni sehemu ya mtandao wa uhifadhi wa wanyamapori wa mfumo-ikolojia wa Serengeti (Serengeti ecosystem) unaojumuisha pia Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro, Hifadhi ya Taifa Serengeti, Mapori ya Akiba Grumeti, Ikorongo, Kijereshi na Maswa.

Kwa mujibu wa Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009, makazi na kuchunga mifugo haviruhusiwi katika Mapori Tengefu.

Ushauri

Serikali haina budi kuumaliza mgogoro huu. Ripoti nyingi za Loliondo na mapendekezo vimeshatolewa kwa miaka zaidi ya 15. Hakuna taarifa isiyojulikana kwa mamlaka za uamuzi. Muda na fedha nyingi vimetumika kwenye mgogoro huu, na sasa ni wakati wa kuona thamani ya vitu hivyo.

Kwenye ripoti zote kumeelezwa umuhimu wa kuihifadhi Loliondo, hasa lile eneo la kilometa za mraba 1,500 linalopendekezwa litungiwe sheria maalumu ili kulilinda.

Walowezi kutoka Kenya waliojiingiza kwenye uchochezi wa mgogoro huu wasiachwe watambe. Tanzania ni nchi huru inayostahili kuachwa iamue mambo yake kwa masilahi ya watu wake, lakini pia na walimwengu. Faida za kuilinda Loliondo hazikomei kwa Watanzania pekee, bali kwa walimwengu, hasa kwenye suala la ikolojia.

Mamlaka za nchi zisiiache Loliondo ikawa ‘jamhuri’ ndani ya Jamhuri ya Muungano. Sharti taratibu na sheria za nchi kama vile uhamiaji zitumike katika kulinda usalama na masilahi ya nchi.

Kiburi kinachojengwa Loliondo cha baadhi ya watu kudai ardhi ni mali yao, na kwamba hawapaswi kuamuliwa na serikali, ni dharau kwa mamlaka za nchi.

Dharau ndiyo hii tunayoshuhudia viongozi wetu wakuu wakitukanwa hadharani. Endapo kila kabila likiamua kupinga uamuzi na mipango halali ya serikali nchi haitatawalika.

Suala la Loliondo na Ngorongoro limezungumzwa mno. Huu ni wakati wa kuondokana na hii migogoro inayochochewa na watu wasiotaka kuangalia masilahi mapana ya nchi, bali masilahi yao na wafadhili wao. Maneno yametosha. Sasa ni wakati wa kuzilinda Loliondo na Ngorongoro. Tusipofanya hivyo kizazi kijacho kitatushangaa.

MY OBSERVATION:
Bado wapo baadhi ya Wamasai waliopo Kenya akiwemo seneta wa Narok wanaamini kuwa hayati Sokoine aliyekuwa waziri Mkuu wa JMT alitaka kuwepo kwa himaya ya wamasai na hivyo wanataka kuirejesha ndoto hiyo.huu ni ujuha kalulu!!!

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!
LEO NIPO SOITSAMBU NGORONGORO
 
Additional Facts:

1. Ngorongoro ni jina la wilaya

2. Ngorongoro ni jina la tarafa iliyopo ndani ya wilaya ya Ngorongoro yenye tarafa tatu

3. Ngorongoro ni jina la kreta (caldera) iliyomo ndani ya tarafa ya Ngorongoro

4. Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro ni eneo lote la tarafa ya Ngorongoro

5. Wafugaji wanaohamasishwa kuhamia Msomera ni wale wanaoishi ndani ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (Tarafa ya Ngorongoro ) na kwamba si Wafugaji wote katika eneo hilo wanatakiwa kuhama

5. Si mara ya kwanza serikali kuchukua hatua ya kupunguza idadi ya wafungaji ndani ya hifadhi ya eneo la Ngorongoro (Tarafa ya Ngorongoro) kwani serikali iliwahi kuwahamisha wafungaji wa jamii ya kabila la Wamag'hati au Watatoga kwenda maeneo mengine nje ya hifadhi hatukusikia kelele
 
Ile ishu ya loliondo gate ya 94 au 95 .....yule mmiliki naye eneo lake ni lipi?
Je mkataba uliisha na je uliongezwa? Na kama umeongezwa je hajaongezewa mraba mwingine?
 
CCM inajaribu kumwagilia maji hili jambo.
CCM haiwezi kukimbia hili.
CCM badala yake inakimbizwa na mgogoro huu.
 
Ile ishu ya loliondo gate ya 94 au 95 .....yule mmiliki naye eneo lake ni lipi?
Je mkataba uliisha na je uliongezwa? Na kama umeongezwa je hajaongezewa mraba mwingine?
Soma. Uache kukurupuka. Mwenye uzi kafafanua vizuuuri tuu!
Msianze kuleta za kuleta
 
hata kama wangekuwa walipewa na hati ya ardhi kabisa, hoja ni kwamba, serikali imeona wamasai wamezidi mno kuzaliwana, wakaamua eneo ilo lisikaliwe na watu tena. kama compensation, wamewapa ardhi kubwa zaidi, wakawajengea na nyumba. nini mnataka tena masai ambacho hamjaelewa?
 
Tatizo ni kutumia nguvu kwenye kila kitu.

Swala la kuondoa masaai Loliondo linataka mkakati wa muda mrefu. Hakuna anaekataa kukuwa kwa hiyo jamii kuna athiri ecosystem ya wanyamapori.

Serikali ilitakiwa ianze na hatua ya kisheria kupiga marufuku ya ujenzi wa makazi mapya ndani ya hifadhi na kusimamia kikamilifu sheria, kuendelea kutenga maeneo mengine ya kuwapa wamasai kuhama voluntarily na kutoa elimu itakayo shawishi watu kuhama taratibu.

Lakini kwenda kuwahamisha watu katika mazingira pekee wanayoyajua, kwa mkupuo and with short notice; it’s a recipe for disaster.
 
Wakili Onesmo K. O, hujui kwamba ardhi yote iko chini ya rais na kwamba anaweza kufuta hati za umiliki na kubadili matumizi, kwa maslahi mapana ya nchi?

Mbona kule Ujiji, Ihefu Mbalali, na Katavi watu walifurushwa hamkujitokeza kuwatetea?
 
UFAFANUZI WA KISHERIA KUHUSU ARDHI YA LOLIONDO

Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na taarifa zisizo sahii zinazotolewa na baadhi ya viongozi kwa ushirika na wale wenye kutamani ardhi ya Loliondo kuwa ardhi yote ya Loliondo na Sehemu ya Tarafa ya Sale ni ardhi ya hifadhi. Wanaodai kuwa kilometa za mraba 4000 za Tarafa ya Loliondo na Sale sio ardhi ya vjijiji, huenda hawajui wanachosema au wameamua kutumia nafasi zao kuchukua ardhi ya vijiji kwa nguvu. Naomba ifahamike pia kuwa sio viongozi wote wanaamini kuwa eneo lote la Loliondo sio ardhi ya vjijiji bali wanaotangaza kuwa kilometa za mraba 4000 si za ardhi ya vjiji ni wachache kwa maslahi ya wachache. Natumia nafasi hii kufafanua kisheria kuhusu hadhi ya ardhi ya Loliondo na Sale kisheria ili kubaini ukweli kuhusu hadhi ya ardhi ya Loliondo kisheria.

Baada ya uhuru, serikali iliendeleza mfumo wa utawala ambapo wilaya na vijiji viliendelea kuwa sehemu ya utawala wa Serikali za Mitaa ambapo eneo la wilaya ya Ngorongoro ilikuwa chini ya utawala wa Wilaya ya Maasai. Wilaya ya Maasai ilijumuisha Wilaya za sasa za Kiteto, Simanjiro, Monduli, Longido na Ngorongoro na makao makuu ya wilaya ikiwa ni Monduli. Baadae mwaka 1979, Wilaya mpya ya Ngorongoro ilianzishwa ili kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi. Wilaya ya Ngorongoro ina Tarafa tatu ambazo ni; Tarafa za Ngorongoro, Loliondo na Sale. Jumla ya kilimeta za Mrabza za Wilaya ni 14,036 ambapo Tarafa ya Ngorongoro ina kilometa za mraba 8,300, Sale 3,500 na Loliondo 2,200. Manake kilometa za mraba za lililokuwa Pori Tengefu la Loliondo lilichukua kilometa za mraba zote 2,200 za Loliondo pamoja na kilometa za mraba 1800 za Tarafa ya Sale.

Ikumbukwe kwamba kabla ya uanzishwaji wa Wilaya ya Ngorongoro, wananchi katika tarafa za Loliondo na Sale walikuwa wakiishi na kumiliki ardhi katika vijiji vyao vilivyosajiliwa ndani ya iliyokuwa Wilaya ya Maasai. Baadhi ya vijiji katika tarafa vilisajiliwa kabla ya kuanzishwa kwa Wilaya mpya ya Ngorongoro. Mgogoro uliopo wa sasa ni kuhusu mpango wa serikali wa kutaka kuchukua ardhi ya vijiji yenye ukubwa wa kilometa za mraba 1500 kuwa sehemu ya hifadhi pekee na kuwaondoa wananchi pamoja na kuzuia kazi za ufugaji. Mkuu wa Mkoa wa Arusha pamoja na viongozi wengine tangu mwaka huu uanze wamekuwa wakisisitiza kuwa ni lazima serikali itenge ardhi hiyo ya vijiji kwa shughuli za uhifadhi pekee. Wamekuwa wakisisitiza kuwa hilo eneo si la vivjiji bali ni eneo lilikuwa pori tengefu ambapo serikali inataka kuchukua kilometa za mraba 1500 na kugawia wananchi kilometa za mraba 4000.

Hadhi ya Ardhi ya Loliondo ilikuwaje wakati wa Ukoloni

Matokeo ya majadiliano na mapitio ya nyaraka mbalimbali yanaonyesha kuwa kabla ya ujio wa wakoloni wa Kijerumani na baadae Waingereza jamii ya kimasai ilikuwa inamiliki na kutumia ardhi hii kwa taratibu za kimila chini ya usimamizi na uangalizi wa viongozi wa mila kwa niaba ya jamii.

Ujio wa wakoloni ulileta utaratibu mwingine ambao ulikuwa chini ya sheria za kikoloni hasa wakati wa Wajerumani na baadae Waingereza walipokuja na sheria ya Ardhi namba 3 ya mwaka 1923 na kufuatiwa na sheria zingine ikiwemo za Uhifadhi wa Wanyamapori. Umiliki wa ardhi kimila ulitambuliwa pia na Sheria ya Ardhi ya mwaka 1923 na iliyofanyiwa marekebisho mwaka 1928, ili kutambua zaidi haki za wenyeji.

Pamoja na kutungwa kwa sheria mpya ya Ardhi, wakati huo wa utawala wa waingereza ni wakati huo pia zilitungwa sheria zinazo husiana na usimamizi, ulinzi wa wanyamapori na uhifadhi. Uwepo wa mapori ya wanyama katika eneo la Sale na Loliondo ulikuwa ni wa muda mrefu tangu miaka ya wakoloni wa Kijerumani hadi wakoloni wa Kiingereza. Ilipofika miaka ya 1930, Serikali ya kikoloni ya Waingereza waliona umuhimu wa kuanza kutunga sheria za kulinda maeneo ya wanyamapori hapa nchini na pia kuweka utaratibu wa kisheria wa kufanya shuguli za uwindaji. Kwa miaka yote hiyo ya nyuma wakati wa ukoloni maeneo haya ya Loliondo na Sale yalikuwa katika maeneo ya wananchi yanayomilikiwa kisheria kama ilivyofafanuliwa hapo juu kwa lengo la kulinda na kuratibu shughuli za Wanyama pekee.

Jitihada za kutaka kuanzisha maeneo ya uhifadhi na mapori tengefu kisheria zilianza rasmi na Wajerumani mwanzoni mwa karne ya 20. Mikakati yote hii zilijaribu kwa kiasi fulani kutambua umiliki wa kimila wa ardhi wa jamii asili. Mikakati hii kwa maeneo mengi ya Afrika Mashariki zilianzisha taratibu za kuweka mazingira ya jamii ya wamaasai kuanza kusumbuliwa katika maeneo yao. Pamoja na kwamba ardhi ya wamasai Tanzania haikukaliwa na wakoloni, tishio kubwa lilikuja kuwa baadae ni taratibu za kisheria za uhifadhi wa rasilimali asili na mbuga za Wanyama kuanza kupewa kipaumbele na serikali za wakoloni na baadae serikali zetu.

Himaya ya Wajerumani (German East Africa ) ilianza kuweka mikakati ya kumiliki maeneo kuanzia mwaka 1885 hadi 1914 walipovamiwa na kuondolewa na Waingereza. Mfano mwanzoni mwa karne ya 20, Wajerumani walianzisha Sheria ya kusimamia Wanyama Pori iitwayo Game Preservation Ordinance ya mwaka 1908 hadi 1911.Baadae baada ya vita ya kwanza ya Dunia Waingereza walikuja na kutunga sheria zingine nyingi baada ya vikao huko Waingereza kuamua kulinda Wanyama na maeneo yao kama ifuatavyo zenye kulenga kwenye usimamizi wa wanyamapori na uhifadhi

i. Kuanzishwa kwa Idara ya Wanyamapori (Tanganyika Game Department in 1919)
ii. Sheria ya Wanyamapori (The Game Preservation Ordinance 1921) iliyoanzisha pia Pori la Akiba la Serengeti kwa wakati huo wa 1929.
iii. Sheria ya Ardhi ( Land Ordinance 1923 )
iv.Sheria mpya ya wanyamapori ( New Game Ordinance ya 1948), Sheria hii ndiyo iliokuja na utaratibu wa kuanzishwa Hifadhi ya Serengeti (Serengeti National Park). Hii ndiyo sheria ya kwanza iliyoanza kuleta maumivu makubwa hasa kwa ardhi za Wamaasai waliokuwa wanaishi Serengeti, Ngorongoro na Loliondo. Mwaka 1959 Kutokana na sheria hii, Wamaasai wakaondolewa maeneo ya Serengeti Mwaka 1959 na kuhamishiwa maeneo ya Ngorongoro na Loliondo na kuungana na ndugu zao wengine.
v.Sheria ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ya mwaka 1959- Sheria hii ilianzishwa na watawala wa kikoloni ili kuhifadhi eneo la Ngorongoro na pia kuwalinda na kuendeleza jamii ya wamaasai waliokuwepo na waliohamishiwa eneo la Ngorongoro kupisha uanzishwaji wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Sheria mpya ya wanyamapori (New Game Ordinance ya 1948), ndiyo iliyokuja na utaratibu wa kuanzisha Hifadhi ya Serengeti (Serengeti National Park). Hii ndiyo sheria ya kwanza iliyoanza kuleta maumivu makubwa hasa kwa ardhi za Wamasai waliokuwa wanaishi Serengeti, Ngorongoro na Loliondo. Mwaka 1959 Kutokana na sheria hii Wamasai wakaondolewa maeneo ya Serengeti Mwaka 1959 na kuhamishiwa maeneo ya Ngorongoro na Loliondo na kuungana na ndugu zao wengine. Sheria ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ya mwaka 1959 ilitungwa na watawala wa kikoloni ili kuhifadhi eneo la Ngorongoro na pia kuwalinda na kuendeleza jamii ya wamaasai walikuwepo na waliohamishiwa eneo la Ngorongoro kupisha uanzishwaji wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Hadhi ya Ardhi ya Loliondo Baada ya Uhuru

Baada ya uhuru, serikali ya Tanzania ilitunga sheria ya Uhifadhi wa wanyamapori ya mwaka 1974 na kuanzisha mapori tengefu ambapo Loliondo na Sale yalitangazwa kwenye Gazeti la Serikali Na. 269 la mwaka 1974. Sheria ya Wanyamapori ya mwaka 1974, imechambuliwa zaidi kwa lengo la kubainisha uhusiano na uwepo wa sheria hii na ardhi za vijiji. Uchambuzi wa sheria hii unaonyesha jinsi mapori tengefu na mapori ya akiba yalivyoanzishwa kwa lengo la kusimamia rasilimali za wanyama pori kipindi cha nyuma bila kuathiri milki za kimila za ardhi katika ardhi za Vijiji wakati wa ukoloni na baada ya Uhuru. Kabla ya sheria hii ya wanyamapori kutungwa baada ya uhuru, kulikuwa na sheria ya Ukoloni iliyoitwa Fauna Game Ordinance, iliyoanzisha pori la akiba la Loliondo katika ardhi ya vijiji ambayo ilikuwa inatumika kwa taratibu za kimila na tamaduni zao kama ilivyokuwa nchi nzima kabla ya ukoloni. Sheria ya Wanyamapori ya mwaka 1974 ilitambua aina tatu za mfumo wa ulinzi. Mapori tengefu pekee ndiyo yalianzishwa katika maeneo ya Vijiji ambapo hayakuwa na mgogoro kwa kuwa hayakugusa milki ya ardhi ya Vijiji.

Kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi ya mwaka 1923 katika kifungu cha 9, ilitoa mamlaka kwa Mkurugenzi wa Huduma za Maendeleo ya Ardhi kutoa hati za kumiliki ardhi za Vijiji. Baada ya mabadiliko ya sheria za Ardhi za Tanzania hasa mwaka 1999, Sheria Mpya ya Ardhi ya Vijiji Na.5 ya mwaka 1999 illibainisha kuwa, kutakuwa na Vyeti vya ardhi vya Vijiji tofauti na hati za kumiliki ardhi zilizotolewa kwa Vijiji kwa mujibu wa Sheria ya ardhi ya mwaka 1923.Vilevile Sheria hizo mpya za ardhi zimeendelea kutambua hati hizo ambazo zilitolewa kwa Mujibu wa Sheria zingine kabla ya kutungwa kwa Sheria hiyo.

Kipindi hiki itakumbukwa kutokana na jitihada za mageuzi makubwa ya upimaji wa Vijiji vya wafugaji katika Tarafa za Loliondo na Sale kwa kupitia viongozi wa Vijiji, Kata, Wilaya na mashirika ya kiraia ambapo vijiji mbalimbali vilipimwa na kupata Hati za kumiliki ardhi katika Vijiji vyao kama ilivyoelezwa katika Taarifa ya Jamii kuhusu mgogoro huu. Mchakato wa upimaji na hatimaye kutolewa kwa hati za kumiliki ardhi hizi, ulisimamiwa na Halimashauri ya wilaya ya Ngorongoro kwa msaada wa mashirika ya KIPOC na ADDO.

Jumla ya ardhi ya vijiji vyenye ukubwa wa Hekta 346,672 za tarafa ya Loliondo zilipimwa na kupatiwa hati za umiliki wa ardhi. Baadhi ya vijiji vilivyoweza kupata hati hizo ni pamoja na Arash, Loosoito/Maaloni, Olorien/ Magaidur, Oloipiri, Soitsambu na Ololosokwan, kwa mujibu wa sheria ya ardhi ya mwaka 1923. Jitihada zote hizi zinabainisha kuwa eneo la kilometa za mraba 4000 za Loliondo na Sale ni ardhi halali za vijjiji zilizokuwa zinatumika pia kama pori tengefu.

Usajili wa Vjijiji Loliondo na Sale

Kifungu cha 7 (12) cha sheria ya Ardhi ya Vijiji kinatambua hati zote za milki ya ardhi ya Vijiji vilivyotolewa kwa mujibu wa sheria zingine kabla ya kutungwa kwa sheria hiyo. Hivyo kwa mujibu wa sheria ya Ardhi ya Vijiji ya mwaka 1999, Vijiji vyote vya tarafa za Loliondo na Sale vilivyosajiliwa kwa Mujibu wa Sheria ya Serikali za mitaa [Mamlaka za wilaya] Na. 7 ya 1982 na kupata hati za kumiliki ardhi ni halali na vinaendelea kutambulika kisheria. Aidha ni dhahiri kuwa hatua ya Serikali ya kutaka kumega ardhi ya Vijiji kiasi cha kilomita za mraba 1,500 inavunja Ibara ya 24 ya katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sheria za ardhi ambazo zinatoa haki ya msingi ya kumiliki mali ambapo ni pamoja na ardhi kama rasilimali kuu.

Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori ya mwaka 1974, ilianzisha mapori tengefu ambapo Loliondo na Sale ilitangazwa kwenye Gazeti la Serikali Na. 269 la mwaka 1974. Kabla ya sheria hii ya wanyamapori kutungwa baada ya uhuru, kulikuwa na sheria ya Ukoloni iliyoitwa Fauna Game Ordinance iliyoanzisha pori la akiba la Loliondo katika ardhi ya vijiji ambayo ilikuwa ikitumika kwa taratibu za mila na tamaduni zao kama ilivyokuwa nchi nzima kabla ya ukoloni ambapo haikuwa na madhara katika milki ya ardhi ya Vijiji kwa kuwa ilitumika kulinda na kuratibu shughuli za wanyamapori. Baada ya miaka kadhaa baadae baada ya uhuru, mwaka 1974, Sheria hiyo ikafutwa baada ya kutungwa sheria mpya tajwa hapo juu ya wanayamapori. Sheria hii pia ilitangaza maeneo ya mapori tengefu katika maeneo ya Vijiji na haikuondoa haki ya milki ya ardhi ya wananchi katika ardhi ya Vijiji.

Ikumbukwe pia kwamba eneo hili la Loliondo ndilo ambalo wakoloni walionyesha kuwa makazi ya wenyeji baada ya uanzishwaji wa Hifadhi ya Serengeti. Lakini wakati wa ukoloni dhana ya mapori ya akiba yalianzishwa kwa lengo la kusimamia wanyamapori bila kuathiri matumizi na mila za usimamizi wa ardhi za wenyeji. Hata hivyo, changamoto za kimaslahi kati ya vijiji vya wafugaji na makampuni binafsi ya kitalii na kiuwindaji zilianza pale Tanzania ilipoingia katika sera za mfumo wa soko huria na kuanza kubinafsisha hadi mashirika yaliyokuwa yanaratibu maswala ya rasilimali asili hapa nchini. Serikali iliruhusu hadi makampuni binafsi kuanza kusimamia shughuli za uwindaji.

Miaka hiyo kabla ya ubinafsishaji mfano kazi za uwindaji zilikuwa chini ya Tanzania Wildlife Company (TAWICO) lakini baada ya miaka 1990 makampuni binafsi yalishamiri katika utalii wa uwindaji na ndio ujio wa Kampuni ya Kiarabu ya Kiwindaji ya Ottero Business (OBC) katika eneo la Loliondo mwaka 1992, na kupewa eneo lote la kilometa za mraba 4000 la Vijiji vya Loliondo na sale. Ujio wa Kampuni hii ya Kiarabu ulianzisha changamoto ya wananchi kutumia maeneo yao ya vijiji kinyume na sheria za ardhi na pia sheria hii ya Wanyamapori ya mwaka 1974. Migogoro mingi ilianza kuzuka baina ya kampuni hii na wananchi na pia baina ya kampuni hii ya OBC na watumiaji wengine wa ardhi ya vijiji kama makampuni mengine yanayofanya kazi za kitalii eneo hili.

Lililokuwa Pori Tengefu (GCA) la Loliondo lilifutwa na Sheria ya Wanyamapori ya mwaka 2009

Mwaka 2009, Sheria mpya ya wanyamapori ilitungwa ambapo pia ilifuta Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori ya mwaka 1974. Mabadiliko ya Sheria ya Wanyamapori yalibadili hadhi ya mapori tengefu na kuondoa shughuli zote za kibinadamu kama ilivyokuwa awali. Sheria hii kwa kutambua kuwa maeneo mengi yaliyokuwa na mapori tengefu ni ardhi halali za vijiji iliweka utaratibu katika kifungu cha 16 (4) na 16 (5) kwa Waziri mwenye dhamana (Maliasili na Utalii) kufanya mapitio upya na kuondoa mapori tengefu katika ardhi za Vijiji ndani ya mwaka mmoja baada ya Sheria hiyo kuanza kutumika (“ For the purpose of sub-section 4 , The Minister shall ensure that no land falling under the village land is included under the game controlled areas’ Section 16).

Sheria hii imepiga marufuku shughuli zote za kibinadamu katika maeneo ya mapori tengefu ambayo kimsingi yalikuwa yamepachikwa katika ardhi za Vijiji kwa kuwa lengo lake lilikuwa ni kusimamia rasilimali za wanyamapori na sio milki ya ardhi. Tafsiri yake ni kuwa, kwa kutambua kuwa maeneo mengi karibu asilimia 60 ya mapori tengefu hapa nchini yalikuwa katika ardhi za vijiji, Bunge ambalo ni muhimili wa kutunga Sheria liliona umuhimu wa kuondoa mapori tengefu katika maeneo ambayo ni ardhi za vijiji kama ilivyokuwa kilometa za mraba 4000 za pori tengefu la Loliondo. Bahati mbaya zoezi hili kwa upande wa Loliondo halikufanyika kama sheria ilivyoagiza, badala yake kumekuwemo na maneno mengi kuwa bado Loliondo nzima ni pori tengefu kinyume na utaratibu wa sasa wa kisheria ambao hauruhusu pori tengefu kuchangamana na shughuli za kibadamu.

Matokeo yake ni kwamba kwa mujibu wa sheria ya Wanyamapori ya sasa Loliondo hakuna tena pori tengefu linalotambulika kisheria. Kwa uchambuzi huu ni wazi kuwa eneo lote la kilometa za mraba 4000 za Loliondo na Sale ni ardhi halali ya vijiji.

Pamoja na uwepo wa mgogoro wa ardhi ya Vijiji katika Tarafa za Loliondo na Sale kuanzia miaka ya 1992, mabadiliko hayo ya kisheria yamechochea kasi ya mgogoro baada ya kutekelezwa kwa jaribio la kutenga eneo halali la Vijiji lenye ukubwa wa kilomita za mraba 1500, kupitia Mpango wa Matumizi ya Ardhi ya wilaya ambayo ilifadhiliwa na Kampuni ya uwindaji ya OBC mwaka 2010, kwa lengo la kulinda maslahi yake ya uwindaji katika eneo hilo. Baada ya wananchi kugundua nia ya Kampuni ya OBC kumegewa ardhi ya Vijiji, mgogoro mpya uliibuka ambapo Kijiji cha Soitsambu mwaka 2010 kilitoa Notisi ya kusudio la kumuondoa OBC kwenye ardhi ya Kijiji kwa barua yenye kumbukumbu namba AR/KJ/55/402/4/1331, kwamba ifikapo mwezi Desemba Kijiji hicho kitakuwa huru kupangia matumizi mengine katika ardhi hiyo ya Kijiji.

Matokeo ya Mabadiliko ya Sheria ya mwaka 2009 kwa pori tengefu la Loliondo Sheria iliyokuwa imetambua mapori tengefu ndani ya ardhi za wananchi ilibadili hadhi ya mapori tengefu na kuondoa shughuli zote za kibinadamu bila kutambua eneo lote la Loliondo na sehemu ya Sale yalikuwa ni ardhi za vjijiji vilivyokuwa na mapori haya tengefu. Wilaya zingine za kifugaji ambazo zimekuwa na mapori tengefu ndani ya ardhi ya vijiji ni Pamoja na Longido, Monduli na Simanjiro na vijjiji vingi katika wilaya hizi vimepatiwa hati za umiliki.

Sheria hii kwa kutambua kuwa maeneo mengi yaliyokuwa na mapori tengefu ni ardhi halali za vijiji iliweka utaratibu katika kifungu cha 16 (4) hadi 16 (5) kwa waziri kutambua maeneo yote yenye mapori tengefu yaliyoko katika ardhi za vijiji na kutangaza ndani ya mwaka mmoja toka baada ya kuanza kutumika kwa sheria hii kuwa yamekosa hadhi ya kuwa mapori tengefu. “ For the purpose of sub-section 4 , The Minister shall ensure that no land falling under the village land is included under the game controlled areas’ Section 16 (5)”.

Tafsiri yake ni kuwa , kwa kutambua kuwa maeneo mengi karibu asilimia 60 ya mapori tengefu hapa nchini yalikuwa katika ardhi za vijiji, watunzi wa sheria hii waliona ni muhimu kuondoa mapori tengefu katika maeneo ambayo yalikuwa ni ardhi za vijiji kama ilivyokuwa kilometa za mraba 4000 za Loliondo na Sale. Bahati mbaya zoezi hili kwa upande wa Loliondo halikufanyika kama sheria ilivyoagiza, badala yake pamekuwepo na maneno mengi kuwa bado Loliondo nzima ni GCA kinyume na utaratibu wa sasa wa kisheria ambao hauruhusu mapori tengefu kuchangamana na shughuli za kibadamu. Matokeo yake ni kwamba kwa mujibu wa sheria ya Wanyamapori ya sasa Loliondo hakuna tena pori tengefu linalotambulika kisheria.

Nafasi ya Taratibu za Kimila

Pamoja na kwamba sheria za kikoloni na hata za Tanzania baada ya Uhuru zilitungwa ili kuweza kusimamia sekta ya ardhi na uhifadhi, ni muhimu kwa wadau wote kufahamu kwamba Mila, utamaduni na elimu ya asili zimekuwa nguzo kuu na muhimu katika kuendeleza ardhi na maliasili katika tarafa za Loliondo na Sale. Jamii ya wafugaji wa Kimaasai inategemea mfumo wa asili wa matumizi ya ardhi unaotegemea misingi ya maarifa, desturi na mila za jadi.

Ardhi inatumiwa kulingana na mahitaji ya pamoja ikiwepo ufugaji, makazi na matambiko. Kwa utaratibu wa maarifa ya jadi, nyanda za malisho zinasimamiwa kwa aina ya matumizi kulingana na msimu (kiangazi, masika na kipupwe). Matumizi ya ardhi yanasimamiwa kwa kutumia mifumo ya asili ya mila na desturi chini ya uratibu na miongozo ya viongozi wa mila (Ilaigwanak). Mila na desturi ya jamii huzingatia uhifadhi wa mazingira, matumizi ya nyanda za malisho (maji na malisho) kwa ajili ya matumizi ya mifugo na wanyamapori. Mfumo huu ulijenga mahusiano mazuri ya asili baina ya wanyamapori, mifugo na watu tangu enzi na enzi.

Mahusiano baina ya mifugo na wanyamapori; mila na desturi ni nguzo kuu katika kuendeleza wanyamapori na rasilimali za asili katika tarafa ya Loliondo na Sale. Licha ya uendelevu wa utaratibu huu, mfumo wake wa usimamizi wa ardhi kwa mifumo ya asili ya nyanda za malisho umekumbwa na migongano mingi ya kisheria na kisera ya uhifadhi wa wanyamapori.

Misimamo ya Baadhi ya Viongozi kuhusu ardhi ya Vijiji Loliondo

Zimekuwepo jitihada hasa zilizoonyesha kwa namna fulani serikali ilikuwa inaashiria kitu gani pamoja na kwamba ni baada ya makele yaliyopigwa na wananchi wa Loliondo na Sale na watetezi wa Haki za Binadamu ndani na nje ya nchi. Mfano mojawapo ni andiko la Rais wa Awamu ya Nne, Mhe Kikwete katika mtandao wa Kijamii wa Twitter akisema kwa kunukuu.
“There has never been, or will there ever be any plan by the Government of Tanzania to evict the Maasai people from their ancestral land”. Kwa Kiswahili “Hakujawahi kuwa na wala hakutakuwa na mpango wowote wa serikali wa kuwafukuza watu wa jamii ya Kimaasai kutoka katika ardhi ya mababu zao.”
Wakati huo huo Waziri Mkuu Mizengo Pinda alitoa msimamo wa Serikali ya Awamu ya nne kuhusu Loliondo Mei 2013 kwa kuandika barua iliyotambua kuwa pamoja na kwamba nia ya serikali ni nzuri ukweli unabaki kuwa hii ni ardhi ya Vijiji na ni lazima kujipanga upya kama serikali kuona ni kwa njia gani maeneo haya yatahifadhiwa bila kuathiri haki za wanavijiji wa eneo hilo. Barua hii ilisitisha zoezi la kutwaa eneo la kilometa za mraba 1,500 kama ilivyo tangazwa na waziri wa Maliasili wa wakati huo , Balozi Hamisi Kagasheki. Hi inaonyesha kuwa serikali ya awamu ya sita inapingana hata na serikali ya awamu iliyopita kuhusu ardhi ya Loliondo.

Hitimisho
Sio tu viongozi wa awamu zote zilizopita kuanzia Marais, Mawaziri wakuu wameendelea kutambua kuwa ardhi yenye mgogoro ni ardhi ya vijiji lakini yenye rasilimali za umma (Wanyama) , lakini hata wananchi wenyewe wanatambua hilo na wamebakia na msimamo huo kuwa ardhi ni yao. Tunazungumzia kilometa za mraba 4000 maana yake ni ardhi yote ya Tarafa ya Loliondo ikiwemo mji mdogo wa Loliondo ambapo ndipo kuna makao makuu ya Wilaya. Sasa sote tujiulize , inawezekanaje kuwa tarafa nzima na sehemu ya tarafa ya Sale kuwa sio ardhi za vijiji wakati humo humo pamekuwepo na vjiji halali vilivyoanzishwa na kusajiliwa na serikali na vyenye hati za umiliki wa ardhi?

Kabla ya uhuru wananchi walikuwa wanakalia na kutumia maeneo hayo kimila ambapo walipata haki ya kisheria na ndiyo maana wakoloni miaka kati ya 1940-1950 walipokuwa wanataka kuanzisha hifadhi ya Serengeti walikuwa na majadiliano ya muda mrefu na viongozi wa mila wawakilishi wa jamii na hatimae kuingia makubaliano ya kuhama mwaka 1958, ambapo inathibitisha pasipo shaka kuwa hiyo ilikuwa ni ardhi yao na walikuwa wakimiliki kimila.

Vilevile baada ya uhuru, Vijiji hivi vimeendelea kutambuliwa na Serikali kwa kusajiliwa kwa mujibu wa Sheria mbalimbali ikiwa ni pamoja na Sheria ya Serikali za Mitaa [Mamlaka za Wilaya] Na.7 ya mwaka 1982, kupimwa na kupatiwa hati/vyeti kwa mujibu wa Sheria za ardhi ya mwaka 1923, na Sheria ya Ardhi ya Vijiji Na.5 ya mwaka 1999. Soma zaidi sura ya pili ya taarifa hii. Ni muhimu serikali na jamii ya watanzania kuelewa kuwa kihistoria eneo hili halikuwahi kuwa wazi tangu enzi za mababu, wakati wa Ukoloni, baada ya Uhuru hadi sasa. Kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha kuwa eneo la Loliondo sio ardhi ya vijiji inapotosha na huenda amepotoshwa pia kuhusu uhalali wa ardhi ya vijiji vya Loliondo na Sale.

Serikali itangaze rasmi kuwa ardhi za vijiji vilivyokuwa na mapori tengefu kabla ya sheria ya mwaka 2009 kwa sasa havina hadhi tena ya mapori tengefu ili kuondoa usumbufu unaondelea kwa sasa . Vilevile sheria hii inatarajiwa kuibua migogoro katika maeneo mengi nchini kwa kuwa mapori tengefu yalianzishwa katika ardhi za Vijiji vilivyosajiliwa, kupimwa kupata hati za ardhi/Vyeti vya ardhi za Vijiji na kufanya Mipango ya matumizi ya ardhi. Aidha kwa tafsiri ya Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori Na.5 ya mwaka 2009 katika kifungu cha 16(5), hakuna pori tengefu lolote Loliondo kwa kuwa haikuwahi kutangazwa kwenye Gazeti lolote la Serikali (GN) tangu kuanza kutumika kwa Sheria hiyo.

Kinachoonekana kwa sasa ni kuwa serikali inakwepa kuanzisha mchakato wowote wa kisheria na kushirikisha wananchi endapo wanahitaji hizo kilometa za mraba 1,500. Wanatambua kuwa kuchukua hilo eneo la vijiji kwa utaratibu wanaotumia sasa wa kusema tunawagawia ardhi kilometa za mraba 2,500 kutoka kwenye kilometa za mraba 4000 hakutakuwa na gharama zozote za fidia. Wananchosisitiza wananchi wa Loliondo ni uwepo wa meza ya majadiliano ili kutoa nafasi ya kutatua mgogoro huu. Nashauri Serikali chini ya Uongozi wa Mama Samia waondoe vikosi Loliondo na kurudi kwenye meza ya majadiliano na jamii kuhusu namna ya kuhifadhi maaeneo ya Loliondo. Michakato hii izingatie haki za binadamu na ushirikishwaji mpana wa wananchi ambao ni wakazi wa maeneo hayo.

Wakili Onesmo Kasale Olengurumwa, Mwanalolindo- 8/6/2022
chawa wa HANGAYA anakutafuta huku
 
Wakili Onesmo K. O, hujui kwamba ardhi yote iko chini ya rais na kwamba anaweza kufuta hati za umiliki na kubadili matumizi, kwa maslahi mapana ya nchi?

Mbona kule Ujiji, Ihefu Mbalali, na Katavi watu walifurushwa hamkujitokeza kuwatetea?
enh! nahuko nako ni nani aliewafurusha!!?? mbona mtatajana mwaka huu!!
 
Additional Facts:

1. Ngorongoro ni jina la wilaya

2. Ngorongoro ni jina la tarafa iliyopo ndani ya wilaya ya Ngorongoro yenye tarafa tatu

3. Ngorongoro ni jina la kreta (caldera) iliyomo ndani ya tarafa ya Ngorongoro

4. Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro ni eneo lote la tarafa ya Ngorongoro

5. Wafugaji wanaohamasishwa kuhamia Msomera ni wale wanaoishi ndani ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (Tarafa ya Ngorongoro ) na kwamba si Wafugaji wote katika eneo hilo wanatakiwa kuhama

5. Si mara ya kwanza serikali kuchukua hatua ya kupunguza idadi ya wafungaji ndani ya hifadhi ya eneo la Ngorongoro (Tarafa ya Ngorongoro) kwani serikali iliwahi kuwahamisha wafungaji wa jamii ya kabila la Wamag'hati au Watatoga kwenda maeneo mengine nje ya hifadhi hatukusikia kelele
Naona suala limeingiliwa na wanasiasa wa kimataifa. Wanataka watalii waipoteze TZ. Naamini SSH na serikali yake watasimama kidete kama lile suala la kuhamisha wamachinga.

SSH hakurupuki, huwa ni fundi sana ya kufanya kazi chini kwa chini, kama hayupo fulani ghafla unaona suala zima limekwisha.
 
Wakili Onesmo K. O, hujui kwamba ardhi yote iko chini ya rais na kwamba anaweza kufuta hati za umiliki na kubadili matumizi, kwa maslahi mapana ya nchi?

Mbona kule Ujiji, Ihefu Mbalali, na Katavi watu walifurushwa hamkujitokeza kuwatetea?
 
Naona suala limeingiliwa na wanasiasa wa kimataifa. Wanataka watalii waipoteze TZ. Naamini SSH na serikali yake watasimama kidete kama lile suala la kuhamisha wamachinga.

SSH hakurupuki, huwa ni fundi sana ya kufanya kazi chini kwa chini, kama hayupo fulani ghafla unaona suala zima limekwisha.

Ukweli uliojificha. Jambo hili lina pande mbili: Mosi, ongezeko la watu na mifugo ni hatari kwa uhifadhi, hii nadhani inatokana na wenyeji kutokuwa waminifu na wazalendo.

Wamekaribisha mifugo ya Wakenya na wanafanya siasa hifadhini, na ndiyo unaona leo kelele zinapigwa sana Kenya. Hatujiulizi maeneo yale yana Wabunge na Bunge lipo on! Kwanini Wabunge hawasimami? Ila Kenya wanamuomba Mh Uhuru aje aongee na Rais Samia. Kwa lipi? Wote tujiulize.

Pili, uhifadhi wa mazingira wa Ngorongoro ni mkubwa sana, na ndiyo maana kila mfugaji tajiri awe Kenya au Tanzania atapeleka mifugo kule kwani nyasi ni nyingi sana kwa ajili ya wanyama pori na maji yapo throughout the year, na ndiyo ugomvi, wameharibu mazingira katika maeneo yao wanaingiza mifugo yao kwenye hifadhi.

Hifadhi ni km 1,500 za mraba, eneo la wamasai wamepewa km 2,500 za mraba kwa ajili yao na mifugo. Sasa wanataka zile km 1,500 za mraba na wao wawepo! Kama umefuatilia jana yupo Mkenya ametoa kauli ya serikali kuacha mara moja uwekaji wa alama za mawe kuzunguka hifadhi.
 
UFAFANUZI WA KISHERIA KUHUSU ARDHI YA LOLIONDO

Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na taarifa zisizo sahii zinazotolewa na baadhi ya viongozi kwa ushirika na wale wenye kutamani ardhi ya Loliondo kuwa ardhi yote ya Loliondo na Sehemu ya Tarafa ya Sale ni ardhi ya hifadhi. Wanaodai kuwa kilometa za mraba 4000 za Tarafa ya Loliondo na Sale sio ardhi ya vjijiji, huenda hawajui wanachosema au wameamua kutumia nafasi zao kuchukua ardhi ya vijiji kwa nguvu. Naomba ifahamike pia kuwa sio viongozi wote wanaamini kuwa eneo lote la Loliondo sio ardhi ya vjijiji bali wanaotangaza kuwa kilometa za mraba 4000 si za ardhi ya vjiji ni wachache kwa maslahi ya wachache. Natumia nafasi hii kufafanua kisheria kuhusu hadhi ya ardhi ya Loliondo na Sale kisheria ili kubaini ukweli kuhusu hadhi ya ardhi ya Loliondo kisheria.

Baada ya uhuru, serikali iliendeleza mfumo wa utawala ambapo wilaya na vijiji viliendelea kuwa sehemu ya utawala wa Serikali za Mitaa ambapo eneo la wilaya ya Ngorongoro ilikuwa chini ya utawala wa Wilaya ya Maasai. Wilaya ya Maasai ilijumuisha Wilaya za sasa za Kiteto, Simanjiro, Monduli, Longido na Ngorongoro na makao makuu ya wilaya ikiwa ni Monduli. Baadae mwaka 1979, Wilaya mpya ya Ngorongoro ilianzishwa ili kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi. Wilaya ya Ngorongoro ina Tarafa tatu ambazo ni; Tarafa za Ngorongoro, Loliondo na Sale. Jumla ya kilimeta za Mrabza za Wilaya ni 14,036 ambapo Tarafa ya Ngorongoro ina kilometa za mraba 8,300, Sale 3,500 na Loliondo 2,200. Manake kilometa za mraba za lililokuwa Pori Tengefu la Loliondo lilichukua kilometa za mraba zote 2,200 za Loliondo pamoja na kilometa za mraba 1800 za Tarafa ya Sale.

Ikumbukwe kwamba kabla ya uanzishwaji wa Wilaya ya Ngorongoro, wananchi katika tarafa za Loliondo na Sale walikuwa wakiishi na kumiliki ardhi katika vijiji vyao vilivyosajiliwa ndani ya iliyokuwa Wilaya ya Maasai. Baadhi ya vijiji katika tarafa vilisajiliwa kabla ya kuanzishwa kwa Wilaya mpya ya Ngorongoro. Mgogoro uliopo wa sasa ni kuhusu mpango wa serikali wa kutaka kuchukua ardhi ya vijiji yenye ukubwa wa kilometa za mraba 1500 kuwa sehemu ya hifadhi pekee na kuwaondoa wananchi pamoja na kuzuia kazi za ufugaji. Mkuu wa Mkoa wa Arusha pamoja na viongozi wengine tangu mwaka huu uanze wamekuwa wakisisitiza kuwa ni lazima serikali itenge ardhi hiyo ya vijiji kwa shughuli za uhifadhi pekee. Wamekuwa wakisisitiza kuwa hilo eneo si la vivjiji bali ni eneo lilikuwa pori tengefu ambapo serikali inataka kuchukua kilometa za mraba 1500 na kugawia wananchi kilometa za mraba 4000.

Hadhi ya Ardhi ya Loliondo ilikuwaje wakati wa Ukoloni

Matokeo ya majadiliano na mapitio ya nyaraka mbalimbali yanaonyesha kuwa kabla ya ujio wa wakoloni wa Kijerumani na baadae Waingereza jamii ya kimasai ilikuwa inamiliki na kutumia ardhi hii kwa taratibu za kimila chini ya usimamizi na uangalizi wa viongozi wa mila kwa niaba ya jamii.

Ujio wa wakoloni ulileta utaratibu mwingine ambao ulikuwa chini ya sheria za kikoloni hasa wakati wa Wajerumani na baadae Waingereza walipokuja na sheria ya Ardhi namba 3 ya mwaka 1923 na kufuatiwa na sheria zingine ikiwemo za Uhifadhi wa Wanyamapori. Umiliki wa ardhi kimila ulitambuliwa pia na Sheria ya Ardhi ya mwaka 1923 na iliyofanyiwa marekebisho mwaka 1928, ili kutambua zaidi haki za wenyeji.

Pamoja na kutungwa kwa sheria mpya ya Ardhi, wakati huo wa utawala wa waingereza ni wakati huo pia zilitungwa sheria zinazo husiana na usimamizi, ulinzi wa wanyamapori na uhifadhi. Uwepo wa mapori ya wanyama katika eneo la Sale na Loliondo ulikuwa ni wa muda mrefu tangu miaka ya wakoloni wa Kijerumani hadi wakoloni wa Kiingereza. Ilipofika miaka ya 1930, Serikali ya kikoloni ya Waingereza waliona umuhimu wa kuanza kutunga sheria za kulinda maeneo ya wanyamapori hapa nchini na pia kuweka utaratibu wa kisheria wa kufanya shuguli za uwindaji. Kwa miaka yote hiyo ya nyuma wakati wa ukoloni maeneo haya ya Loliondo na Sale yalikuwa katika maeneo ya wananchi yanayomilikiwa kisheria kama ilivyofafanuliwa hapo juu kwa lengo la kulinda na kuratibu shughuli za Wanyama pekee.

Jitihada za kutaka kuanzisha maeneo ya uhifadhi na mapori tengefu kisheria zilianza rasmi na Wajerumani mwanzoni mwa karne ya 20. Mikakati yote hii zilijaribu kwa kiasi fulani kutambua umiliki wa kimila wa ardhi wa jamii asili. Mikakati hii kwa maeneo mengi ya Afrika Mashariki zilianzisha taratibu za kuweka mazingira ya jamii ya wamaasai kuanza kusumbuliwa katika maeneo yao. Pamoja na kwamba ardhi ya wamasai Tanzania haikukaliwa na wakoloni, tishio kubwa lilikuja kuwa baadae ni taratibu za kisheria za uhifadhi wa rasilimali asili na mbuga za Wanyama kuanza kupewa kipaumbele na serikali za wakoloni na baadae serikali zetu.

Himaya ya Wajerumani (German East Africa ) ilianza kuweka mikakati ya kumiliki maeneo kuanzia mwaka 1885 hadi 1914 walipovamiwa na kuondolewa na Waingereza. Mfano mwanzoni mwa karne ya 20, Wajerumani walianzisha Sheria ya kusimamia Wanyama Pori iitwayo Game Preservation Ordinance ya mwaka 1908 hadi 1911.Baadae baada ya vita ya kwanza ya Dunia Waingereza walikuja na kutunga sheria zingine nyingi baada ya vikao huko Waingereza kuamua kulinda Wanyama na maeneo yao kama ifuatavyo zenye kulenga kwenye usimamizi wa wanyamapori na uhifadhi

i. Kuanzishwa kwa Idara ya Wanyamapori (Tanganyika Game Department in 1919)
ii. Sheria ya Wanyamapori (The Game Preservation Ordinance 1921) iliyoanzisha pia Pori la Akiba la Serengeti kwa wakati huo wa 1929.
iii. Sheria ya Ardhi ( Land Ordinance 1923 )
iv.Sheria mpya ya wanyamapori ( New Game Ordinance ya 1948), Sheria hii ndiyo iliokuja na utaratibu wa kuanzishwa Hifadhi ya Serengeti (Serengeti National Park). Hii ndiyo sheria ya kwanza iliyoanza kuleta maumivu makubwa hasa kwa ardhi za Wamaasai waliokuwa wanaishi Serengeti, Ngorongoro na Loliondo. Mwaka 1959 Kutokana na sheria hii, Wamaasai wakaondolewa maeneo ya Serengeti Mwaka 1959 na kuhamishiwa maeneo ya Ngorongoro na Loliondo na kuungana na ndugu zao wengine.
v.Sheria ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ya mwaka 1959- Sheria hii ilianzishwa na watawala wa kikoloni ili kuhifadhi eneo la Ngorongoro na pia kuwalinda na kuendeleza jamii ya wamaasai waliokuwepo na waliohamishiwa eneo la Ngorongoro kupisha uanzishwaji wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Sheria mpya ya wanyamapori (New Game Ordinance ya 1948), ndiyo iliyokuja na utaratibu wa kuanzisha Hifadhi ya Serengeti (Serengeti National Park). Hii ndiyo sheria ya kwanza iliyoanza kuleta maumivu makubwa hasa kwa ardhi za Wamasai waliokuwa wanaishi Serengeti, Ngorongoro na Loliondo. Mwaka 1959 Kutokana na sheria hii Wamasai wakaondolewa maeneo ya Serengeti Mwaka 1959 na kuhamishiwa maeneo ya Ngorongoro na Loliondo na kuungana na ndugu zao wengine. Sheria ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ya mwaka 1959 ilitungwa na watawala wa kikoloni ili kuhifadhi eneo la Ngorongoro na pia kuwalinda na kuendeleza jamii ya wamaasai walikuwepo na waliohamishiwa eneo la Ngorongoro kupisha uanzishwaji wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Hadhi ya Ardhi ya Loliondo Baada ya Uhuru

Baada ya uhuru, serikali ya Tanzania ilitunga sheria ya Uhifadhi wa wanyamapori ya mwaka 1974 na kuanzisha mapori tengefu ambapo Loliondo na Sale yalitangazwa kwenye Gazeti la Serikali Na. 269 la mwaka 1974. Sheria ya Wanyamapori ya mwaka 1974, imechambuliwa zaidi kwa lengo la kubainisha uhusiano na uwepo wa sheria hii na ardhi za vijiji. Uchambuzi wa sheria hii unaonyesha jinsi mapori tengefu na mapori ya akiba yalivyoanzishwa kwa lengo la kusimamia rasilimali za wanyama pori kipindi cha nyuma bila kuathiri milki za kimila za ardhi katika ardhi za Vijiji wakati wa ukoloni na baada ya Uhuru. Kabla ya sheria hii ya wanyamapori kutungwa baada ya uhuru, kulikuwa na sheria ya Ukoloni iliyoitwa Fauna Game Ordinance, iliyoanzisha pori la akiba la Loliondo katika ardhi ya vijiji ambayo ilikuwa inatumika kwa taratibu za kimila na tamaduni zao kama ilivyokuwa nchi nzima kabla ya ukoloni. Sheria ya Wanyamapori ya mwaka 1974 ilitambua aina tatu za mfumo wa ulinzi. Mapori tengefu pekee ndiyo yalianzishwa katika maeneo ya Vijiji ambapo hayakuwa na mgogoro kwa kuwa hayakugusa milki ya ardhi ya Vijiji.

Kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi ya mwaka 1923 katika kifungu cha 9, ilitoa mamlaka kwa Mkurugenzi wa Huduma za Maendeleo ya Ardhi kutoa hati za kumiliki ardhi za Vijiji. Baada ya mabadiliko ya sheria za Ardhi za Tanzania hasa mwaka 1999, Sheria Mpya ya Ardhi ya Vijiji Na.5 ya mwaka 1999 illibainisha kuwa, kutakuwa na Vyeti vya ardhi vya Vijiji tofauti na hati za kumiliki ardhi zilizotolewa kwa Vijiji kwa mujibu wa Sheria ya ardhi ya mwaka 1923.Vilevile Sheria hizo mpya za ardhi zimeendelea kutambua hati hizo ambazo zilitolewa kwa Mujibu wa Sheria zingine kabla ya kutungwa kwa Sheria hiyo.

Kipindi hiki itakumbukwa kutokana na jitihada za mageuzi makubwa ya upimaji wa Vijiji vya wafugaji katika Tarafa za Loliondo na Sale kwa kupitia viongozi wa Vijiji, Kata, Wilaya na mashirika ya kiraia ambapo vijiji mbalimbali vilipimwa na kupata Hati za kumiliki ardhi katika Vijiji vyao kama ilivyoelezwa katika Taarifa ya Jamii kuhusu mgogoro huu. Mchakato wa upimaji na hatimaye kutolewa kwa hati za kumiliki ardhi hizi, ulisimamiwa na Halimashauri ya wilaya ya Ngorongoro kwa msaada wa mashirika ya KIPOC na ADDO.

Jumla ya ardhi ya vijiji vyenye ukubwa wa Hekta 346,672 za tarafa ya Loliondo zilipimwa na kupatiwa hati za umiliki wa ardhi. Baadhi ya vijiji vilivyoweza kupata hati hizo ni pamoja na Arash, Loosoito/Maaloni, Olorien/ Magaidur, Oloipiri, Soitsambu na Ololosokwan, kwa mujibu wa sheria ya ardhi ya mwaka 1923. Jitihada zote hizi zinabainisha kuwa eneo la kilometa za mraba 4000 za Loliondo na Sale ni ardhi halali za vijjiji zilizokuwa zinatumika pia kama pori tengefu.

Usajili wa Vjijiji Loliondo na Sale

Kifungu cha 7 (12) cha sheria ya Ardhi ya Vijiji kinatambua hati zote za milki ya ardhi ya Vijiji vilivyotolewa kwa mujibu wa sheria zingine kabla ya kutungwa kwa sheria hiyo. Hivyo kwa mujibu wa sheria ya Ardhi ya Vijiji ya mwaka 1999, Vijiji vyote vya tarafa za Loliondo na Sale vilivyosajiliwa kwa Mujibu wa Sheria ya Serikali za mitaa [Mamlaka za wilaya] Na. 7 ya 1982 na kupata hati za kumiliki ardhi ni halali na vinaendelea kutambulika kisheria. Aidha ni dhahiri kuwa hatua ya Serikali ya kutaka kumega ardhi ya Vijiji kiasi cha kilomita za mraba 1,500 inavunja Ibara ya 24 ya katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sheria za ardhi ambazo zinatoa haki ya msingi ya kumiliki mali ambapo ni pamoja na ardhi kama rasilimali kuu.

Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori ya mwaka 1974, ilianzisha mapori tengefu ambapo Loliondo na Sale ilitangazwa kwenye Gazeti la Serikali Na. 269 la mwaka 1974. Kabla ya sheria hii ya wanyamapori kutungwa baada ya uhuru, kulikuwa na sheria ya Ukoloni iliyoitwa Fauna Game Ordinance iliyoanzisha pori la akiba la Loliondo katika ardhi ya vijiji ambayo ilikuwa ikitumika kwa taratibu za mila na tamaduni zao kama ilivyokuwa nchi nzima kabla ya ukoloni ambapo haikuwa na madhara katika milki ya ardhi ya Vijiji kwa kuwa ilitumika kulinda na kuratibu shughuli za wanyamapori. Baada ya miaka kadhaa baadae baada ya uhuru, mwaka 1974, Sheria hiyo ikafutwa baada ya kutungwa sheria mpya tajwa hapo juu ya wanayamapori. Sheria hii pia ilitangaza maeneo ya mapori tengefu katika maeneo ya Vijiji na haikuondoa haki ya milki ya ardhi ya wananchi katika ardhi ya Vijiji.

Ikumbukwe pia kwamba eneo hili la Loliondo ndilo ambalo wakoloni walionyesha kuwa makazi ya wenyeji baada ya uanzishwaji wa Hifadhi ya Serengeti. Lakini wakati wa ukoloni dhana ya mapori ya akiba yalianzishwa kwa lengo la kusimamia wanyamapori bila kuathiri matumizi na mila za usimamizi wa ardhi za wenyeji. Hata hivyo, changamoto za kimaslahi kati ya vijiji vya wafugaji na makampuni binafsi ya kitalii na kiuwindaji zilianza pale Tanzania ilipoingia katika sera za mfumo wa soko huria na kuanza kubinafsisha hadi mashirika yaliyokuwa yanaratibu maswala ya rasilimali asili hapa nchini. Serikali iliruhusu hadi makampuni binafsi kuanza kusimamia shughuli za uwindaji.

Miaka hiyo kabla ya ubinafsishaji mfano kazi za uwindaji zilikuwa chini ya Tanzania Wildlife Company (TAWICO) lakini baada ya miaka 1990 makampuni binafsi yalishamiri katika utalii wa uwindaji na ndio ujio wa Kampuni ya Kiarabu ya Kiwindaji ya Ottero Business (OBC) katika eneo la Loliondo mwaka 1992, na kupewa eneo lote la kilometa za mraba 4000 la Vijiji vya Loliondo na sale. Ujio wa Kampuni hii ya Kiarabu ulianzisha changamoto ya wananchi kutumia maeneo yao ya vijiji kinyume na sheria za ardhi na pia sheria hii ya Wanyamapori ya mwaka 1974. Migogoro mingi ilianza kuzuka baina ya kampuni hii na wananchi na pia baina ya kampuni hii ya OBC na watumiaji wengine wa ardhi ya vijiji kama makampuni mengine yanayofanya kazi za kitalii eneo hili.

Lililokuwa Pori Tengefu (GCA) la Loliondo lilifutwa na Sheria ya Wanyamapori ya mwaka 2009

Mwaka 2009, Sheria mpya ya wanyamapori ilitungwa ambapo pia ilifuta Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori ya mwaka 1974. Mabadiliko ya Sheria ya Wanyamapori yalibadili hadhi ya mapori tengefu na kuondoa shughuli zote za kibinadamu kama ilivyokuwa awali. Sheria hii kwa kutambua kuwa maeneo mengi yaliyokuwa na mapori tengefu ni ardhi halali za vijiji iliweka utaratibu katika kifungu cha 16 (4) na 16 (5) kwa Waziri mwenye dhamana (Maliasili na Utalii) kufanya mapitio upya na kuondoa mapori tengefu katika ardhi za Vijiji ndani ya mwaka mmoja baada ya Sheria hiyo kuanza kutumika (“ For the purpose of sub-section 4 , The Minister shall ensure that no land falling under the village land is included under the game controlled areas’ Section 16).

Sheria hii imepiga marufuku shughuli zote za kibinadamu katika maeneo ya mapori tengefu ambayo kimsingi yalikuwa yamepachikwa katika ardhi za Vijiji kwa kuwa lengo lake lilikuwa ni kusimamia rasilimali za wanyamapori na sio milki ya ardhi. Tafsiri yake ni kuwa, kwa kutambua kuwa maeneo mengi karibu asilimia 60 ya mapori tengefu hapa nchini yalikuwa katika ardhi za vijiji, Bunge ambalo ni muhimili wa kutunga Sheria liliona umuhimu wa kuondoa mapori tengefu katika maeneo ambayo ni ardhi za vijiji kama ilivyokuwa kilometa za mraba 4000 za pori tengefu la Loliondo. Bahati mbaya zoezi hili kwa upande wa Loliondo halikufanyika kama sheria ilivyoagiza, badala yake kumekuwemo na maneno mengi kuwa bado Loliondo nzima ni pori tengefu kinyume na utaratibu wa sasa wa kisheria ambao hauruhusu pori tengefu kuchangamana na shughuli za kibadamu.

Matokeo yake ni kwamba kwa mujibu wa sheria ya Wanyamapori ya sasa Loliondo hakuna tena pori tengefu linalotambulika kisheria. Kwa uchambuzi huu ni wazi kuwa eneo lote la kilometa za mraba 4000 za Loliondo na Sale ni ardhi halali ya vijiji.

Pamoja na uwepo wa mgogoro wa ardhi ya Vijiji katika Tarafa za Loliondo na Sale kuanzia miaka ya 1992, mabadiliko hayo ya kisheria yamechochea kasi ya mgogoro baada ya kutekelezwa kwa jaribio la kutenga eneo halali la Vijiji lenye ukubwa wa kilomita za mraba 1500, kupitia Mpango wa Matumizi ya Ardhi ya wilaya ambayo ilifadhiliwa na Kampuni ya uwindaji ya OBC mwaka 2010, kwa lengo la kulinda maslahi yake ya uwindaji katika eneo hilo. Baada ya wananchi kugundua nia ya Kampuni ya OBC kumegewa ardhi ya Vijiji, mgogoro mpya uliibuka ambapo Kijiji cha Soitsambu mwaka 2010 kilitoa Notisi ya kusudio la kumuondoa OBC kwenye ardhi ya Kijiji kwa barua yenye kumbukumbu namba AR/KJ/55/402/4/1331, kwamba ifikapo mwezi Desemba Kijiji hicho kitakuwa huru kupangia matumizi mengine katika ardhi hiyo ya Kijiji.

Matokeo ya Mabadiliko ya Sheria ya mwaka 2009 kwa pori tengefu la Loliondo Sheria iliyokuwa imetambua mapori tengefu ndani ya ardhi za wananchi ilibadili hadhi ya mapori tengefu na kuondoa shughuli zote za kibinadamu bila kutambua eneo lote la Loliondo na sehemu ya Sale yalikuwa ni ardhi za vjijiji vilivyokuwa na mapori haya tengefu. Wilaya zingine za kifugaji ambazo zimekuwa na mapori tengefu ndani ya ardhi ya vijiji ni Pamoja na Longido, Monduli na Simanjiro na vijjiji vingi katika wilaya hizi vimepatiwa hati za umiliki.

Sheria hii kwa kutambua kuwa maeneo mengi yaliyokuwa na mapori tengefu ni ardhi halali za vijiji iliweka utaratibu katika kifungu cha 16 (4) hadi 16 (5) kwa waziri kutambua maeneo yote yenye mapori tengefu yaliyoko katika ardhi za vijiji na kutangaza ndani ya mwaka mmoja toka baada ya kuanza kutumika kwa sheria hii kuwa yamekosa hadhi ya kuwa mapori tengefu. “ For the purpose of sub-section 4 , The Minister shall ensure that no land falling under the village land is included under the game controlled areas’ Section 16 (5)”.

Tafsiri yake ni kuwa , kwa kutambua kuwa maeneo mengi karibu asilimia 60 ya mapori tengefu hapa nchini yalikuwa katika ardhi za vijiji, watunzi wa sheria hii waliona ni muhimu kuondoa mapori tengefu katika maeneo ambayo yalikuwa ni ardhi za vijiji kama ilivyokuwa kilometa za mraba 4000 za Loliondo na Sale. Bahati mbaya zoezi hili kwa upande wa Loliondo halikufanyika kama sheria ilivyoagiza, badala yake pamekuwepo na maneno mengi kuwa bado Loliondo nzima ni GCA kinyume na utaratibu wa sasa wa kisheria ambao hauruhusu mapori tengefu kuchangamana na shughuli za kibadamu. Matokeo yake ni kwamba kwa mujibu wa sheria ya Wanyamapori ya sasa Loliondo hakuna tena pori tengefu linalotambulika kisheria.

Nafasi ya Taratibu za Kimila

Pamoja na kwamba sheria za kikoloni na hata za Tanzania baada ya Uhuru zilitungwa ili kuweza kusimamia sekta ya ardhi na uhifadhi, ni muhimu kwa wadau wote kufahamu kwamba Mila, utamaduni na elimu ya asili zimekuwa nguzo kuu na muhimu katika kuendeleza ardhi na maliasili katika tarafa za Loliondo na Sale. Jamii ya wafugaji wa Kimaasai inategemea mfumo wa asili wa matumizi ya ardhi unaotegemea misingi ya maarifa, desturi na mila za jadi.

Ardhi inatumiwa kulingana na mahitaji ya pamoja ikiwepo ufugaji, makazi na matambiko. Kwa utaratibu wa maarifa ya jadi, nyanda za malisho zinasimamiwa kwa aina ya matumizi kulingana na msimu (kiangazi, masika na kipupwe). Matumizi ya ardhi yanasimamiwa kwa kutumia mifumo ya asili ya mila na desturi chini ya uratibu na miongozo ya viongozi wa mila (Ilaigwanak). Mila na desturi ya jamii huzingatia uhifadhi wa mazingira, matumizi ya nyanda za malisho (maji na malisho) kwa ajili ya matumizi ya mifugo na wanyamapori. Mfumo huu ulijenga mahusiano mazuri ya asili baina ya wanyamapori, mifugo na watu tangu enzi na enzi.

Mahusiano baina ya mifugo na wanyamapori; mila na desturi ni nguzo kuu katika kuendeleza wanyamapori na rasilimali za asili katika tarafa ya Loliondo na Sale. Licha ya uendelevu wa utaratibu huu, mfumo wake wa usimamizi wa ardhi kwa mifumo ya asili ya nyanda za malisho umekumbwa na migongano mingi ya kisheria na kisera ya uhifadhi wa wanyamapori.

Misimamo ya Baadhi ya Viongozi kuhusu ardhi ya Vijiji Loliondo

Zimekuwepo jitihada hasa zilizoonyesha kwa namna fulani serikali ilikuwa inaashiria kitu gani pamoja na kwamba ni baada ya makele yaliyopigwa na wananchi wa Loliondo na Sale na watetezi wa Haki za Binadamu ndani na nje ya nchi. Mfano mojawapo ni andiko la Rais wa Awamu ya Nne, Mhe Kikwete katika mtandao wa Kijamii wa Twitter akisema kwa kunukuu.
“There has never been, or will there ever be any plan by the Government of Tanzania to evict the Maasai people from their ancestral land”. Kwa Kiswahili “Hakujawahi kuwa na wala hakutakuwa na mpango wowote wa serikali wa kuwafukuza watu wa jamii ya Kimaasai kutoka katika ardhi ya mababu zao.”
Wakati huo huo Waziri Mkuu Mizengo Pinda alitoa msimamo wa Serikali ya Awamu ya nne kuhusu Loliondo Mei 2013 kwa kuandika barua iliyotambua kuwa pamoja na kwamba nia ya serikali ni nzuri ukweli unabaki kuwa hii ni ardhi ya Vijiji na ni lazima kujipanga upya kama serikali kuona ni kwa njia gani maeneo haya yatahifadhiwa bila kuathiri haki za wanavijiji wa eneo hilo. Barua hii ilisitisha zoezi la kutwaa eneo la kilometa za mraba 1,500 kama ilivyo tangazwa na waziri wa Maliasili wa wakati huo , Balozi Hamisi Kagasheki. Hi inaonyesha kuwa serikali ya awamu ya sita inapingana hata na serikali ya awamu iliyopita kuhusu ardhi ya Loliondo.

Hitimisho
Sio tu viongozi wa awamu zote zilizopita kuanzia Marais, Mawaziri wakuu wameendelea kutambua kuwa ardhi yenye mgogoro ni ardhi ya vijiji lakini yenye rasilimali za umma (Wanyama) , lakini hata wananchi wenyewe wanatambua hilo na wamebakia na msimamo huo kuwa ardhi ni yao. Tunazungumzia kilometa za mraba 4000 maana yake ni ardhi yote ya Tarafa ya Loliondo ikiwemo mji mdogo wa Loliondo ambapo ndipo kuna makao makuu ya Wilaya. Sasa sote tujiulize , inawezekanaje kuwa tarafa nzima na sehemu ya tarafa ya Sale kuwa sio ardhi za vijiji wakati humo humo pamekuwepo na vjiji halali vilivyoanzishwa na kusajiliwa na serikali na vyenye hati za umiliki wa ardhi?

Kabla ya uhuru wananchi walikuwa wanakalia na kutumia maeneo hayo kimila ambapo walipata haki ya kisheria na ndiyo maana wakoloni miaka kati ya 1940-1950 walipokuwa wanataka kuanzisha hifadhi ya Serengeti walikuwa na majadiliano ya muda mrefu na viongozi wa mila wawakilishi wa jamii na hatimae kuingia makubaliano ya kuhama mwaka 1958, ambapo inathibitisha pasipo shaka kuwa hiyo ilikuwa ni ardhi yao na walikuwa wakimiliki kimila.

Vilevile baada ya uhuru, Vijiji hivi vimeendelea kutambuliwa na Serikali kwa kusajiliwa kwa mujibu wa Sheria mbalimbali ikiwa ni pamoja na Sheria ya Serikali za Mitaa [Mamlaka za Wilaya] Na.7 ya mwaka 1982, kupimwa na kupatiwa hati/vyeti kwa mujibu wa Sheria za ardhi ya mwaka 1923, na Sheria ya Ardhi ya Vijiji Na.5 ya mwaka 1999. Soma zaidi sura ya pili ya taarifa hii. Ni muhimu serikali na jamii ya watanzania kuelewa kuwa kihistoria eneo hili halikuwahi kuwa wazi tangu enzi za mababu, wakati wa Ukoloni, baada ya Uhuru hadi sasa. Kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha kuwa eneo la Loliondo sio ardhi ya vijiji inapotosha na huenda amepotoshwa pia kuhusu uhalali wa ardhi ya vijiji vya Loliondo na Sale.

Serikali itangaze rasmi kuwa ardhi za vijiji vilivyokuwa na mapori tengefu kabla ya sheria ya mwaka 2009 kwa sasa havina hadhi tena ya mapori tengefu ili kuondoa usumbufu unaondelea kwa sasa . Vilevile sheria hii inatarajiwa kuibua migogoro katika maeneo mengi nchini kwa kuwa mapori tengefu yalianzishwa katika ardhi za Vijiji vilivyosajiliwa, kupimwa kupata hati za ardhi/Vyeti vya ardhi za Vijiji na kufanya Mipango ya matumizi ya ardhi. Aidha kwa tafsiri ya Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori Na.5 ya mwaka 2009 katika kifungu cha 16(5), hakuna pori tengefu lolote Loliondo kwa kuwa haikuwahi kutangazwa kwenye Gazeti lolote la Serikali (GN) tangu kuanza kutumika kwa Sheria hiyo.

Kinachoonekana kwa sasa ni kuwa serikali inakwepa kuanzisha mchakato wowote wa kisheria na kushirikisha wananchi endapo wanahitaji hizo kilometa za mraba 1,500. Wanatambua kuwa kuchukua hilo eneo la vijiji kwa utaratibu wanaotumia sasa wa kusema tunawagawia ardhi kilometa za mraba 2,500 kutoka kwenye kilometa za mraba 4000 hakutakuwa na gharama zozote za fidia. Wananchosisitiza wananchi wa Loliondo ni uwepo wa meza ya majadiliano ili kutoa nafasi ya kutatua mgogoro huu. Nashauri Serikali chini ya Uongozi wa Mama Samia waondoe vikosi Loliondo na kurudi kwenye meza ya majadiliano na jamii kuhusu namna ya kuhifadhi maaeneo ya Loliondo. Michakato hii izingatie haki za binadamu na ushirikishwaji mpana wa wananchi ambao ni wakazi wa maeneo hayo.

Wakili Onesmo Kasale Olengurumwa, Mwanalolindo- 8/6/2022
Blah blah ardhi yote Tanzania ni mali ya seriikali na inatumika kwa manufaa ya nchi nzima
Hadithi na hekaya za ukoloni hazina maana tena kwa sasa
Muulizeni Ole Ngurumwa nani aliwapa Wamaasai ruhusa ya kuhamia Tanga, Kilimanjaro,Pwani,na sehemu za Arusha toka kwenye hiyo anayoita ardhi yao ya asili
NB; LOLIONDO KWA ASILI NI ARDHI YA WASONJO SIO NA WAMASAAI NI WAVAMIZI TUU.
 
Hivi hii kauli ya shamba kukutwa na bangi ni mali ya mwenye shamba na shamba kukutwa na dhahabu ni mali ya serikali. je siku hizi haifanyi kazi???
NB: Nimeuliza tuu hasa baada ya kuona hili la ngorongoro limekuwa la kipekee kabisa.
Bangi imepandwa/lindwa/inatunzwa mbegu na mjani/inavunwa/inapogolewa/inawekewa dawa na lazima ipaliliwe ili ikue! kama ukiyafanya haya Bangi ni yako....

lkn pia dhahabu inapandwa na nani??? ina paliliwa/tunzwa/lindwa na nani?wapi/lini?? km ukifanya haya bila shaka Dhahabu ni yako!
 
Hivi ulishawahi kuona bangi ikipuliziwa dawa??

Nijuavyo katika mimea isiyokuwa na mahitaji ya dawa mmoja wapo ni bangi.

Kule kwetu usandaweni tunaitumia kama mboga zingine na huku isibania ni kitu inatupa sana pesa hatuna mpango wa kulima mahindi na mazao mengine.
Madini wakiyakuta kwenye shamba unalolilipia na kulima siku zote huwa wanagharamikia wao?
Ni utani tuu kwenye swali lililo kwenye bolded mkuu.
Tuna sheria ya ajabu ya umiliki wa radhi kwa Tanzania.
 
Back
Top Bottom