Olympiki - Target 2012 - Medali 20

Nyani na Pundi, hoja zenu nakubaliana nazo kabisa. Lakini mnafanya makosa makubwa matatu.

a. Mnachukulia kana kwamba napendekeza tutilie mkazo kujiandaa kwa ajili ya Olympiki na tuache kufanya shughuli nyingine za kijamii na kiuchumi. Nitakuwa sina akili timamu nikipendekeza hivyo. Katika kujiandaa kufikia ndoto yetu suala hili la maandalizi ya olympiki ni sehemu ya shughuli za kijamii na kiuchumi siyo nje yake. Ninachopendekeza ni kwamba pamoja na mambo mengine na miradi mingine tunayoifanya tuongeze mradi huu maalumu wa kujiandaa na Olympiki 2012 kule London.

b. Kwamba napendekeza kiwango kikubwa cha fedha ambacho hatuwezi kukitumia kwenye michazo na kitasababisha dent kubwa kwenye uchumi wetu. Si kweli. Nimependekeza Shilingi bilioni moja kwa mwaka. Hizi shilingi bilioni moja kwa mwaka sisemi zitoke kwenye wizara ya elimu, au zitoke wizara ya afya, au wizara ya ulinzi au wizara nyingine yoyote ile. Hizi ni fedha ambazo zitatoka kwenye wizara ambayo tayari inapewa bajeti na wizara hiyo inaitwa ni WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI NA MICHEZO.

Sasa utaona siyo mimi ambaye ni Mtanzania wa Kwanza duniani kuleta michezo na kutaka itengewe fedha. Hata nchi maskini zinastahili kuwa na michezo. Tukifuata mtiririko wa hoja zenu ina maana tufute wizara ya michezo hadi tuwe na GDP kubwa zaidi na ya kuwa tufute michezo ili tujenge hospitali n.k.

Bajeti ya Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo tayari imeshatengwa na kupitishwa na Bunge ina Shs. Bilioni 21 kati ya hizo Bilioni karibu 10 ni za maendeleo. Sasa katika mipango ya maendeleo ya wizara hiyo tutumie basi angalau 'ka bilioni" moja kwa ajili ya kuanza kujiandaa na Olympiki. Ubaya wa hili ni nini? Kama fedha zimetengwa kwa ajili ya maendeleo ya michezo, kwanini zisitumike kuendeleza michezo?

c. Kosa la tatu ambalo mnalifanya ni kufikiri kuwa hatuwezi kumudu (afford) kutumia bilioni moja kwenye michezo kwa sababu ni nyingi sana na sisi ni masikini tuna vipaumbele vingine. Hoja hii inaweza kuwa kweli lakini ukija kuiangalia kwa karibu utaona haina nguvu sana. Tanzania inapoteza kwa mwaka asilimia 20 ya fedha yake ya fedha ya misaada kwenye ufisadi (corruption) (takwimu za USAID).

Kwa mwaka tunapoteza karibu Shs. Bilioni 400 kwenye manunuzi mabaya, kutofauta taratibu, mikataba mibovu ukosefu wa mapato kutokana ni misamaha ya kodi n.k Fedha zetu nyingi zinavuja kutokana na usimamizi mbaya wa fedha. Kimsingi hatuitaji kuomba fedha hizo bilioni moja kutoka nje au hata kuongeza kodi; tunachohitaji ni usimamizi mzuri wa fedha na kuhakikisha fedha zinazoibwa zinarudishwa na katika hizo tuzitenge kuendeleza michezo na kujiandaa kwa Olimpiki ya London 2012. Hapa kuna tatizo gani?

Shilingi bilioni moja siyo fedha nyingi ukizingatia matumizi yetu ya ajabu na usimamizi wetu wa fedha.

Mimi naamini tukitaka tunaweza. Tukitaka kutenga Bilioni moja kila mwaka kujiandaa kwa Olimpiki ya 2012 tunaweza. Na tukijiwekea lengo la medali 20 ingawa kwa wengine (kama Mtanzania) ni lengo gumu kwangu mimi nasema ni lengo halisia. Tukijiandaa na ikifika Olimpiki hiyo tukapata medali tano tu tutaona fahari kwani tumevuna tulichopanda na itaonesha kujiandaa kunalipa. Hizo medali tano zinaweza kuwa chachu ya sisi kufanya vizuri zaidi 2016.

Hivyo, tuungane mkono kujiandaa kwa Olimpiki 2012 kwa kuboresha mkakati nilioupendekeza hapo juu iili hatimaye Tanzania na yenyewe irudi kwenye medali za Olimpiki. Tukitaka tunaweza.
 
Watawala wetu wako bize kulogana Bagamoyo tu, maendeleo hakuna mabadiliko hakuna, kazi kusengenyana tu na kutafutana uchawi huku wakijisifia kuwa wanakubalika sana na wananchi, wa majimbo yao ya uchaguzi,

Nikiwa mdogo nilikuwa nikimuona Filbert Bay, akifanya mazoezi kila siku asubuhi na jioni akishirikina na washikaji wake Mbeleka na Amarido waliokuwa wakicheza mpira wa miguu sana timu ya Mzizima, yaani mkoa wa Dar, ninasema hivi leo hakuna mbongo anaweza fanya yale mazoezi ya Bay no way, hakuna mbongo anaweza kujituma namna ile tena,

Nimeyaona kwa macho yangu mazoezi ya timu ya Watoto Wa Yanga, under Cocha M-Rumania kwa jina la Victor, kina Pondamali, Mkweche, Adolf Rishad, Kassim Manara, Gordian Mapango, Omyy, Patric Rugaimukamu, Rashid Idd "Chama", Tostao, Kaburu, na wengineo wallahi yale mazoezi enzi zile uwanja wa Kaunda hakuna timu ya mpira bongo inaweza kuyafanya leo,

Watawala na wachezaji wenyewe wote ni wazembe, wa kuridhika na sifa uchwara, I mean michezo iliisha na kina Mogella, Malota Soma, Omari Hussein, Peter Tino, Said Mwamba Kizota "Maswali Hakuna Khakha", Makumbi Juma, Ikangaa, na Nyambui baada ya pale basi ikawa ndio mwisho wa yote, sasa imebaki hadithi tu!

Labda tupige marufuku kujihusisha na mashindano ya kimataifa mpaka tutakapokuwa tayari tena, kwa sasa tunapoteza bure time na hela zinaoweza kutumika kwa maendeleo mengine muhimu kwa taifa!
 
Topic nzuri lakini ipelekwe kwenye MICHEZO.

FP.. hii topiki siyo ya michezo hasa ni ya siasa! think about it...

Ndio yale yale ya wanasiasa kutafuta ujiko kupitia michezo.... Hii ni topiki ya michezo na ilifaa kuwepo kwenye ukumbi wa michezo ili iweze kujadiliwa na wapenda michezo na sio wanasiasa.

Matokeo yake, tayali kadhia za kisiasa zimeshaingia ndani ya bandiko hili. Ni ukweli usio fichika kuwa tunaweza kushinda medali pale tu siasa itakapotenganishwa na michezo.
 
Titus Simba alipostaafu kulusha masumbwi, alikiri kuwa siasa na michezo ni vitu viwili tofauti, na kusema kuwa anaachana na ndondi akiwa lofa kwa kuchanganya siasa na michezo.

Marehemu Titus ni mmoja wa wanamichezo ambae aliweza kutangaza jina la Tanzania kupitia michezo wa ngumi, na kuweza kushinda medali katika michezo ya commonwealth miaka ile ya sabini. Aliwahi kusema kuwa wanasiasa wanarudisha nyuma juhudi binafsi za wanamichezo.

Tanzania ilikuwa ikivuma wakati ule wa Ujamaa, baada ya ujamaa kujiondokea kimyakimya na ushindi kwenye olimpiki ukafa nao kimyakimya. Mabadiliko ya mfumo wa kisiasa yamekuwa na manufaa kwa wanasiasa pekee.

Ni vema kwa wanamichezo kuanza kutafuta mapromoter ili waweze kufaidika na juhudi zao.
 
Kibunango, ili mapromota wafanye kazi yao vizuri wanasiasa itabidi watengeneza sera nzuri ya kupromota na kutunga sheria nzuri ya kuinua michezo.. so bado wanasiasa wanahusika...
 
Mzee Mwanakijiji,

Naomba malipo ya hati miliki ya mawazo niliyokuwa nayawaza tangu juzi nilipoona tulivyoboronga mita 10000!

Niliona baada ya mizunguko kama 10, jamaa wa Tanzania akakimbilia maji, nikajiuliza kunkuaje ati mwenzetu anakimbilia maji, je hakujianda kuvunguka uwanja mara 26 bila kunywa maji?

Nikasikia eti waliweka kambi Arusha, nikajiuliza hali ya hewa ya Arusha na Beijing ni sawa? tunajua Beijing ni jua kali na humidity kama Dar, Tanga au Zanzibar, kwa nini hatukuweka kambi kwenye mazingira ya hali ya hewa na muinuko sawa na Beijing ili wachezji wetu wasikimbilie kunywa maji kwa kiu baada ya raundi kumi za kukimbia?

The Idea is great and I hope people will take it positively and be creative enough to capitalize on this!

Pundit na Nyani,

Ama kweli Ujamaa umewakomaa, pamoja na nia njema kabisa ya kudai mengine ya muhimu. Mi nilifikiri nyie mshakuwa Mabepari fulani hivi, kumbe yale maji ya Nyerere bado hamjapata hengiova?

Ninachojiuliza kwa kauli zenu, nimekuwa katika forum hizi za kupiga kelele kwa miaka 10, mpaka leo Ujinga, Maradhi na Umasikini haujaondoka au kupungua, bado tunadidimia kwenye udongo tifutifu!

Yes there is a need to have priorities on things that matter, and athleticism is something that we should take it seriously just like Machinga welfare and others.

Mentality za Kitanzania ni kuwa only Udaktari, Ukulima, Uhandisi, Ualimu, Ufanyabiashara ndio kazi.

We can invest heavily on Michezo, Utamaduni na Sanaa na kuwa other sources of income and employment.

We are failing because we are sluggish in being creative!

If we had strong will, Umasikini, Maradhi na Ujinga would have been on their way out and become a vocabulary, lakini we a dwelling on unyonge that we can not think of anything else to rescue us.

Kama binadamu, we have to find alternatives za kujiimarisha. Kama hao CCM na Serikali wakiona kuwa hili lawezekana na wakashaurika na matokeo tukayaona na tukajinufaisha wote, hamuoni kuwa huo ni mwanzo wa kuanza kusikilizwa na ushauri wetu kuheshimika?

As far as the talk in here kila siku kuhusu Ufisadi and whatever, tunayoyapiga makelele huishia kuwa mapovu and honestly no body in leadership circles gives a crap anymore.

We may assume we are a threat, but we are being treated like Mbwa Koko, kubweka lakini mwepesi kufyata mkia.

So the idea of Kijiji cha Michezo na Project Michezo kama kuvutia utalii na uwekezaji, should be promoted by us as an investment and economic idea.
 

Sawa nimekuelewa unatoka wapi na unakwenda wapi. Kuhusu hako "ka bilioni" kamoja kama katakuwa ndani ya bajeti ya wizara husika basi sina ugomvi. Wasiwasi wangu unakuja kwenye kiasi cha fedha. Sidhani kama unataka kuandaa wanaspoti wa calibre ya olimpiki "ka bilioni" kamoja tu kwa mwaka katatosha. Ukiweka lengo la kushinda medali 20 ni lazima upeleke contingent kubwa. Siwezi kutoa idadi lakini najua lazima iwe kubwa. Sasa maandalizi ya contingent kubwa si mchezo. Kuna mashindano na trials nyingi sana zinazo precede olimpiki. Kuna mambo ya vifaa, facilities, makocha, na wataalamu wengine wengi tu. Sasa kweli "ka bilioni" kamoja tu kwa mwaka kataweza kweli kugharamia maandalizi ya uhakika ya olimpiki?
 

Rev.,
Mwanakijiji hakuwa clear mwanzoni. Kaja kufafanua na sasa sidhani kama ni wazo baya kama nilivyokuwa nadhania mwanzoni. Tatizo nilionalo sasa ni uwezo wa maandalizi ya uhakika yatayozalisha wanamichezo wenye calibre ya kwenda kuchuana na mijitu kama Usain Bolt au Michael Phelps. Si ulisikia mwenyewe jinsi menu ya Michael Phelps ilivyokuwa ya nguvu? 12,000 calories a day!! Hata Mr. Olympia mwenyewe hafukii calories kama hizo. Sasa usikute maandalizi ya Phelps peke yake kwa mwaka yanakaribia hako "ka bilioni" kamoja alikopendekeza Mwanakijiji.....unless aniambie alikuwa anarusha namba tu katika ku-brainstorm ideas....
 

Mtani Ngosha,

Hizo bilioni si za Serikali, je watu binafsi na mashirika nayo si yatahamasishwa yasaidie?

Plani ni kuwa na mikakati ya muda mrefu, ndio maana inasema tunaanza kuunda timu na kuhimiza michezo mashuleni kwa vijana na watoto kuanzia umri wa miaka 12 na kuendelea.

Ndio 2012 inaonekana karibu sana, lakini kumbuka China na Project 119 walioanza baada ya Athens 2004. Sasa hivi angalia nani anaongoza kwa medali za dhahabu.

Tuna michezo mingi sana tunaweza shiriki kama tutakuwa na nia ya kushinda na si kwenda kushiriki na kutalii.

It is all about science, money, will and management!
 

Bana acha unoko, si kuna manumbu, mitambaa na nsansa! hizo hazitoshi kutoa kalori 10000?
 
Tena nimesahau, ongeza matembele, mtama na Zimpoku( Punda au Musuli wa Mpopo)!
 
Nyani, hako "kabilioni" kamoja ni namba ya hewani tu; kama kweli tunataka kuwa a Sports power house we have to pay for it; it won't be cheap. Na hapa siangalii upande wa serikali tu nazungumzia (kama Mchungaji alivyoonesha) ushirikiano na taasisi binafsi na vikundi mbalimbali vya kijamii. Inatakiwa kuwa na mpango na kama ramani ya nyumba.

Tunasema tunataka kujenga nyumba ya aina gani, yenye vyumba vingapi, ghorofa ngapi n.k na tukichora ramani tunaangalia mifuko mingapi ya sementi, nondo, n.k na pia wafundi wa aina gani watahitajika kufanikisha na kwa muda gani. Tukishapiga hesabu za chini za nyumba hiyo tunafanya makisio ya juu na kuweka "the Unknown factor" ndani na hatimaye tuna mahali pa kuanzia.

Kama tunataka kufanya vizuri Olimpiki ya London 2012 hatuna budi kuchora ramani hiyo sasa, kugawana majukumu sasa na kuanza kuchimba msingi sasa; Ili tutakapofika 2012 hata kama hatujapaua, ulimwengu wataona kuwa kuna msingi na muundo wa nyumba unaonekana vipi. We have to prepare for victory tusisubiri nasibu. Na katika hilo nafasi ya wanasiasa haiwezi kupuuzwa.

Vinginevyo tukubali tu kuwa wasindikizaji, kulalamika watu wakifanya vibaya na kukinga mikono kuombea mavuno ya vitu tusivyopanda.
 
Asante Mmkjj kwa changamoto hii uliyoileta hapa

nashindwa kuelewa kwa nini tulipeleka timu kule Beijing

miaka miwili ya kwanza kutafuta vipaji, halafu kushikiriki mashindano ya kimataifa ndani ya mwaka mmoja ni muda mfupi..watu wanajinoa kwa miaka hata nane kabla ya kuwa na uhakika wa leta angalau ka medali kamoja, wale wachina wadogo wadogo walioshinda dhahabu walianza kukunjwa tangu 2001

Hizo bilioni moja zitaliwa tu...

...nimeona watu wazima tu wanarusha visahani na mikuki pale, kwa hiyo na mimi nina mpango wa kuingia mtaani haraka iwezekanavyo..kutafuta kisahani changu, venue ya mazoezi etc...halafu ntajiandaa kivyangu vyangu kushindana Olympic 2012....

nawashauri na wengine wafuate plan kama yangu...
 

Mzee Mwanakijiji,

I would rather be a realistic than a dreamer. Kama kutoka kwenye sifuri mpaka medali 20 ingelikuwa rahisi hivyo, waarabu wangelikuwa na medali nyingi tu kufikia sasa.

Unahitaji long term strategy kufikia malengo ambitious kama hayo. Lazima uanzie chini kabisa, lazima utayarishe walimu kwanza, maeneo ya michezo, lazima ubadili culture ya vijana ili waone kuna umuhimu na haja ya kufanya michezo, culture ya wazee ili waone michezo inaweza kuwa na faida sawa na elimu nyingine.

Haitoshi kumwaga mapesa tu, itaishia kuwa kama mabilioni ya JK. Si tumeona hata kwenye mpira wa miguu? Hao wachezaji wetu wa taifa, wamelipwa pesa, wameletewa coach wa maana lakini bado tumebaki kichwa cha mwenda wazimu, kila mtu anatunyoa tu.

Hakuna short kati mkuu, ndio maana wajamaa wa njozi walishindwa, walikuwa na nia lakini hawakuwa na uvumilivu wa kusubiri mhindi uanze kutoka mbegu mpaka kufikia mhindi uliokamaa, walikuwa wanataka maajabu leo.

Binafsi ningependa hata leo tuwe na medali 100 lakini je is it possible? Tatizo kwa Tanzania hata pesa zikiwepo bado wajanja watakula.

Labda sisi wote tuna wajibu kwa njia moja ama nyingine kusaidia kukuza michezo hata kama ni kwa kuwasaidia vijana wanaocheza barabarani ili wawe na mipira au kuzuia ufisadi wa kuchukua viwanja vya michezo.
 
If we change our mentalities, we can become competitive and great in sports.

Nakumbuka nikiwa mdogo nakuwa na napenda michezo, si wazazi tuu bali hata marafiki na jamaa walisema Michezo, Sanaa na Utamaduni ni kupoteza muda na havina manufaa wala Prestige!

Same mentality still prevails today!
 
Mzee Mwanakijiji,

I would rather be a realistic than a dreamer. Kama kutoka kwenye sifuri mpaka medali 20 ingelikuwa rahisi hivyo, waarabu wangelikuwa na medali nyingi tu kufikia sasa.

Kwa sababu waarabu wao kama sisi hawataki kutumia utajiri wao kujiandaa na michezo na zaidi ya yote michezo haina umuhimu kama vile sisi. Ila siku wakiamua kuja na mkakati kama ninaoupendekeza utashangaa. The same applies to India.

Unahitaji long term strategy kufikia malengo ambitious kama hayo.

Mtanzania, mimi nimekuja na short term strategy ya miaka minne na mwingine anaweza kuja na ya muda mrefu siyo lazima tufute mpango wa muda mfupi kwa sababu hatuna mpango wa muda mrefu. The two are not exclusive of each other but fundamentaly complimentary.

Lazima uanzie chini kabisa, lazima utayarishe walimu kwanza, maeneo ya michezo, lazima ubadili culture ya vijana ili waone kuna umuhimu na haja ya kufanya michezo, culture ya wazee ili waone michezo inaweza kuwa na faida sawa na elimu nyingine.

Mtanzania, tayari kuna michezo mashuleni imesharudishwa; tayari facilities zipo tena nyingi tu (angalau kila shule kina kiwanja cha mpira) walimu wa michezo wapo wengine tena wamesomea kozi za michezo. Siyo kwamba tunaanza kwenye sifuri. La hasha.

Haitoshi kumwaga mapesa tu, itaishia kuwa kama mabilioni ya JK. Si tumeona hata kwenye mpira wa miguu? Hao wachezaji wetu wa taifa, wamelipwa pesa, wameletewa coach wa maana lakini bado tumebaki kichwa cha mwenda wazimu, kila mtu anatunyoa tu.

Hatumwagi mapesa tu kama walivyofanya kina JK na "mabilioni" yake. Tunapanga mkakati na tunauexecute fully. Tunahitaji mabadiliko makubwa. Mfano wako wa soka ni mzuri kwa kiasi lakini pia unaonesha tatizo letu bado tunataka kupanda tusichovuna. Ningekuwa mimi ningepanga mkakati tofauti kabisa wa kuibadilisha soka yetu. It is all about daring, planning, and executing.

Hakuna short kati mkuu, ndio maana wajamaa wa njozi walishindwa, walikuwa na nia lakini hawakuwa na uvumilivu wa kusubiri mhindi uanze kutoka mbegu mpaka kufikia mhindi uliokamaa, walikuwa wanataka maajabu leo.

Tofauti yangu na wewe ni kuwa mimi nimependekeza njia na mahali pa kuanzia; sijaona mtu yeyote aliyekuja na pendekezo la kuboresha michezo na kuifanya Tanzania kuwa power House zaidi ya kuombea kuwa siku moja tutakuwa na long term plan. Tunachoweza kufanya leo, tusisubiri kesho. Tukitaka kujiandaa vizuri na Olimpiki 2012, tuanze leo tusitubiri long term za vitu gani; let us focus and do it.

Binafsi ningependa hata leo tuwe na medali 100 lakini je is it possible? Tatizo kwa Tanzania hata pesa zikiwepo bado wajanja watakula.

Haitoshi kupenda. Hilo ndilo tatizo letu tungependa tufanye vizuri katika soka, tungependa tufanye vizuri katika riadha n.k Kama kweli tungependa tungejiandaa kupata tunavyotaka. Mimi ningependa tuwe na medali angalau 20 lakini sijaishia nimetoa pendekezo la nini kifanyike. Kama tukituata mpango nilioupendekeza (with modifications of course) na 2012 tukapata medali 5 tu tutakuwa tumefanikiwa mno. Kwangu haitakuwa disappointment bali ni kuonesha kuwa tukitaka tuvune na tule, hatuna budi tupande, tumwagilie, tung'oe magugu na kuhakikisha mimea yetu inakuwa katika ardhi yenye rutuma na vinunurisho vyote.

Labda sisi wote tuna wajibu kwa njia moja ama nyingine kusaidia kukuza michezo hata kama ni kwa kuwasaidia vijana wanaocheza barabarani ili wawe na mipira au kuzuia ufisadi wa kuchukua viwanja vya michezo.

Hilo ndilo lililotufikisha hapa; kuendelea kufanya yale yale (ya kusaidia watoto kucheza mitaani, vimashindano uchwara n.k) na kutarajia matokeo tofauti mazuri una tafsiri yake. Hatuwezi kufanya vile vile (kama unavyopendekeza) na kutegemea matokeo tofauti. Ni lazima tufikiri nje ya sanduku la "vile vile". Kusaidia vijana "wanaocheza barabarani ili wawe na mipira na kuzuia ufisadi wa kuchukua viwanja vya michezo" ni yale yale. Watu wakiona mafanikio ya michezo na ya kuwa tumepanga kufanya vizuri kwenye Olimpiki na mpango wetu ulivyo, watakataa kunyang'anywa viwanja!
 
Haya kaeni mkao wa kula maana Usain Bolt leo anakimbia mita 200....
 
Mwanakijiji,

..hivi Kenya na Ethiopia wametumia kiasi gani cha fedha kufikia viwango walivyonavyo.

..miaka ya Filbert Bayi,Suleiman Nyambui,na Gidamis Shahanga, Tanzania ilikuwa inaongoza tukifuatiwa na Ethiopia[Miruts Yifter] na Kenya kwa mbali.

..nafikiri tuanze na mbio ndefu na za kati ambazo tuna historia na uzoefu nazo. lets build on that first. sidhani kama zinahitajika fedha nyingi sana kuandaa wanariadha wa mbio ndefu.

..vilevile kinachokosekana ni fedha peke yake, au kuna matatizo mengine yamejificha?
 

Joka Kuu, tatizo siyo fedha. Tatizo ni mkakati wa ushindi. Hatujajiandaa kushinda. Wenzetu Kenya na Ethiopia wana programu za ushindi na wamewekeza kweli kwenye mbio ndefu.

Naamini hata kwa pendekezo lako tunaweza kuweka maeneo matatu ya kutilia mkazo. Mbio fupi (tunaziweza vizuri tu kama Jamaica, kama umewahi kushiriki Umiseta utajua tunavyo vipaji) na mbio ndefu )(kuanzia 800 hadi Marathoni) tunaweza vizuri tu. Mifano ya kina Shahanga n.k si kwa sababu tulikuwa tumejiandaa sana ni kwa sababu tulisukumwa na vipaji vyao (na kumbuka kati yao waliingia riadha wakajifunza vizuri hapa Marekani) na pia uzalendo. Tuliona fahari kupeperusha bendera yetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…