Oman: Rais Samia ataka kuwepo Maritime transport ya kusafirishia Wanyama wakiwa hai kutoka Tanzania kwenda Oman

Kwahiyo nchi kama Australia wanaosafirisha Kondoo huko ni wajinga ila wewe ndio una akili kuwazidi? Kama hao wahitaji wametaka Ng'ombe hai,wewe tatizo lako ni nini?
Kaangalie kwa mm Australia aliuza hao kondoo hai na kwa nn sasa hivi hauzi wakiwa hai
Pili, jiulize tumekosa soko la nyama hadi tuuze ng'ombe wakiwa hai?
 
2050 hakuna mtalii atakuja tanzania

Na bado kuwa wapuuzi wanasema mama anaupiga mwingi! Hii namna ya wao kuweza kuiba hawa simba tembo twiga Ila kusema sijui mbuzi hapa tumepigwa tena mkuu!! Watoto wetu sijui itakuwaje kila nikiwaza kuhusu badae nadata
 
Tunajilinganisha bado na Australia?
Tukishindwa kuwa na viwanda vya nyama ili tuuze nje tutakua na viwanda vya aina gani tena? Maana kwenye Teknolojia tulishafeli na hatuwezi.
Kama uwezo wetu upo kwenye kuzalisha ng'ombe , basi duniani tusifike kwa kuwa na viwanda vya nyama vya kisasa kwa kuwa hatuwezi kuwa na viwanda vya magari au simu au computer
 
Kwa hiyo haya machinjio mliyojenga yatafanya kazi gani?
Nilidhani mnauza mali zilizichakatwa kumbe sasa hata viwanda havitakiwi,
Malighafi ziwe zinaenda bila kuongezwa thamani?

Kazi ipo bado.
 
Acha utani

Sitanii Mkuu nilikuwa uarabuni miaka ya 80 na nilikuwepo kwenye sekeseke hilo
Utofauti tulianza kuujua kwa miguu ilikuwa mikubwa kuliko ya kondoo wa kawaida
Walitumwa wachunguzi kivyao kwenda kuona nini kunaendelea kumbe ni kangaroo
Kuanzia hapo wakawa wanakuja Hai na wamenyolewa manyoa yote
Wao wabaki na sufu [emoji23][emoji23]
 
13 June 2022
Muscat, Oman

KONGAMANO LA WAFANYABIASHARA WA OMAN NA TANZANIA


Bw. Paul Koyi kwa niaba ya TCCIA chemba ya wafanyabiashara waliopo Tanzania washukuru jinsi walivyopokewa na furaha tele kukutana na wafanyabiashara wenzao waliopo Oman.

TCCI wamekumbushia umuhimu wa kuwepo 'kuaminiana' na 'uwazi' katika namna nzima ya kufanya biashara baina ya makampuni yaliyopo Oman na Tanzania ili kuitumia fursa hiyo adhimu.
 
Kwa hiyo haya machinjio mliyojenga yatafanya kazi gani?
Nilidhani mnauza mali zilizichakatwa kumbe sasa hata viwanda havitakiwi,
Malighafi ziwe zinaenda bila kuongezwa thamani?

Kazi ipo bado.
Kwani soko litakua ni Oman tu? Sasa hivi hizo nyama zinauzwa nchi gani na nchi gani?
 
Ni kweli ndiyo maana Australia wanasafirisha wanyama hai baada ya Kulifahamu soko vizuri, na hii husaidia kuikamata fursa vizuri zaidi. Tunaweza kukazia mjadala huu kwa maneno matatu : Mteja Ni Mfalme.

Haswaaa
Mkuu mimi nataka mnyama hai kwa bei yamakubaliano na wewe eti unaniambia Hapana nakuchinjia nakutumi heee kwani lazima Basi baki nao sasa tunaenda Somalia na Kenya [emoji23]
 

Naunga mkono hoja yako Mkuu
Ila biashara ni makubaliano kwenye soko la nyama tupeleke nyama na wanaotaka wanyama hai wachinje wenyewe sawa pia
 
Kaka acha akili mgando Kama alikuwa nataka kuiba angetangaza ili iweje
Mama angesema mifugo angeeleweka kwa wepesi kuliko alivyosema wanyama mtu akitaja wanyama wabongo wanachojua ni Simba, chui, Nyati, Serikali ilishapiga Marufuku kusafirisha mbuzi na kondoo nje ya nchi, kuna viwanda vya nyama vipo mkuranga, Mama anataka awaambie Wa Omani waje kujenga viwanda vya nyama kuliko kuwapeleka mifugo uko kwa Waarabu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani soko litakua ni Oman tu? Sasa hivi hizo nyama zinauzwa nchi gani na nchi gani?
Kuna kiwanda cha nyama kipo mkuranga kizuri tu kimetoa ajira kwa wananchi sasa anataka kupeleka wanyama nje wakati ilishapigwa marufuku mbuzi na kondoo kuuzwa kenya tu, na kama ni fursa basi tuwaambie wakenya waje kununua kwetu kama zamani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Badala ya mzungu kuhangaika kuja Tanzania kwanini asiishie hapo Oman tu ambapo ni rahisi kufikika.

I wish aje rais mwingine anayejielewa afute mambo yote yasiyokuwa na faida kwa Taifa yanayofanyika sasa.

Kinachofanyika sasa ni mnada wa Hadhara wa Rasilimali za Taifa.
 
Naunga mkono hoja yako Mkuu
Ila biashara ni makubaliano kwenye soko la nyama tupeleke nyama na wanaotaka wanyama hai wachinje wenyewe sawa pia
Hao Sasa kunakua hakuna maana yoyote
Ukiuza ng'ombe bei itakua chini na faida kwa mnunuaji kuliko kumuuzia nyama.
Kwani kuwaomba waje wajenge viwanda vya nyama hapa ni tatizo? Ila mbona hata viwanda vilivyopo pale kibaha vinamilikiwa na wenye asili ya huko, au hawawaamini?
 
Yaani mnapeleka ajira nje wakati huku kunachangamoto ya ajira.wao waje wawekeze hapa nchini ili tutengeneze ajira hapahapa.mkipeleka wanyama hai tutakuwa tumetengeneza mazingira ya kutorosha maliasili zetu na tutarudishiwa tena kama finished goods kwa bei ya juu.Ifike mahali tubadilishe katiba kuwapa mwaka mmoja wanaopata urais kwa dharura.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nani kakwambia kua Australia hauzi Kondoo hai huko Uarabuni? Hivi hua mnajiandikia tu ili mradi na wewe usiachwe nyuma?
Nimekuambia kaangalie kwa nn walizuia
Alafu kwa nn tunajilinganisha na Australia? Wao Wana viwanda vya kila aina kuendesha uchumi wao mkubwa, huku sisi uwezo huo hatuna basi kwenye hivi vidogo tunavyomudu kwa nn tusiwekeze kwenye viwanda kwa kuanzisha viwanda vingi vya nyama?
 
Nchi Ina watu wengi wajinga hii, Kuna mmoja alikuwa anafurahia Kenya kuruhusiwa kutuletea maziwa huku ya brookside akasema ataanza kunywa hayo ikiwa huku kwetu tuna kila aina ya ngombe. Ila hapohapo wakenya hawaruhusu maziwa ya Asas kule kwao
 
Kina nani walizuwia? Mpaka leo Australia wanasafirisha Kondoo huko Uarabuni.
 
Hapa tusimame kidete tuseme HAPANA!! Tunataka kuhalalisha wizi wa mchana! Ukiruhusu kusafirisha wanyama hai tutabaki na mbuga zisizo na wanyama muda si mrefu!! Hii itakuwa kinyume na kanuni ya utunzaji wa mazingira!! Tutaua utengamano na ulinganifu wa viumbe hai kwenye mbuga zetu (killing the equilibrium balance of the ecosystem in our game reserves), na huo ndio utakuwa mwisho wa utalii!! Huyu mama lazima aambiwe kuwa sasa anataka KWENDA MBALI SANA na HAIVUMILIKI TENA!!
Waarabu wana uwezo wa kutengeneza meli maalumu ya kusafirisha wanyama iliyo kubwa kama viwanja viwili au vitatu vya mpira (kama vile aircraft carriers-ambazo huwa na uwanja wa kurusha na kutua ndege). Fikiria mameli hayo kama matano yafanye kazi hadi 2030 wakati mama anahitimisha awamu yake ya moto, atatuachia nini kwenye mbuga zetu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…