Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 17,047
- 63,206
Huku Donald Trump akitamba kuwa Wahouthi wamegwaya na wameufyata, kumbe hiyo ni kauli ya kujitoa kimasomaso ya mkubwa (face saving) baada ya mazungumzo ya nyuma ya pazia ya pande hizo mbili. Oman imejitokeza na kusema kuwa yenyewe ndiyo iliyokuwa msuluhishi baina ya pande hizo mbili behind the scenes.
Marekani ilijaribu kila aina ya mashambulizi ya Anga lakini wahouthi waliendelea kuzuia meli yoyote ya kwake au ya israel kupita katika eneo hilo, na mpaka sasa marekani imeshindwa kuondoa blockade hiyo ya meli kwa njia za kijeshi.
Wakati huohuo makamanda wa Marekani wakawa wanaonya kuwa Mashambulizi ya Marekani kwa Wahouthi yanaimalizia marekani silaha adimu ambazo ingeweza kuzihitaji kwa ajili ya mapambano mengine kama vile ikitokea mgogoro na China (rejea ishu ya Taiwan).
Baada ya Marekani kuona kuwa haina uwezo wa kuwapiga wahouthi kwa airpower pekee, na baada ya kugundua kuwa military assets za wahouthi ziko underground marekani ikaona itafute namna ya kufanya suluhu, kama nija ya kujitoa kimasomaso (Save face) kwa kumtumia Oman kuwa Msuluhishi,
Wahouthi wamesema kuwa baada ya mazungumzo hayo hawatashambulia meli zinazopita hapo, ila makubaliano yao na Marekani hayazuii wao kuendelea kuitandika Isrel kwa Hypersonic missiles.
Sasa ngoja tuje tuone hii ngoma itaunfold vipi, maana Israel pamoja na uwezo wake mkubwa wa airpower lakini tofauti na mission zake kwa nchi za jirani, Yemen iko mbali, ni ghali mno kupeleka ndege kupiga kila mara, na huwa inahitaji planning ya muda mrefu.
Wakati huohuo Inaelezwa kuwa kuna mategemeo ya cease-fire huko Gaza kabla Donald Trump hajafanya ziara yake kwenda kwenye nchi za kiarabu hivi karibuni. Huenda hata Wahouthi kukubali kusitisha uzuiaji wa meli kupita inatokana na ufahamu huu kuwa Marekani imewaahidi wahouthi kuwa cease-fire huko Gaza inakuja.
Operesheni za Wahouthi ndani ya Israel zimefanikiwa kuparalyse uchumi wa Israel kwa kiasi kikubwa, hofu ya raia iko juu, Mashirika mbalimbali ya ndege duniani yamesitisha safari zao ndani ya anga la Israel kwa sababu za kiusalama, Bandari za Israel ni kama zipo nusus kaputi ni meli chache sana zinazotia nanga.
Taarifa hii imeripotiwa na mashirika mengi makubwa ya habari ikiwemo Reuters.