Omba omba wa Kidigitali ni balaa!! Leo nimetia akili!

Omba omba wa Kidigitali ni balaa!! Leo nimetia akili!

Kiraka Kikuu

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2011
Posts
5,903
Reaction score
2,001
Wandugu,leo nilikuwa nikipita pita katika mitaa ya jiji la Kijani,mitaa ya Uhindini.
Katika kutembea,nikakutana na mama omba omba,amevalia nadhifu kiasi;na anaonekana ni mlemavu wa macho(asiye ona).
Basi,huruma ikaniingia,nikaingia mfukoni na kumkabidhi noti ya sh. 500.
Mama yule aliipokea,akaitazama,kisha akaniambia,"Yaani umeona mimi thamani yangu ni sh. 500?
Nitafanyia nini sasa hiki ki hela?"
Kisha akafungua rambo yake akatupia mle.
Nilichoona mle,da!
Wekundu watupu!!
Ikabidi niondoke kwa aibu,nimekomaje!!
Najuuta!
 
yupo mama wa kiarabu..huwa anazunguka maofisini kuomba..yeye anapenda isiwe chini ya elfu 5 tu..na akifika anamuulizia bosi kama anamjua vile..
 
Hahahahaaah! Hapo ukute hiyo jero ndio ulikuwa unaitegemea kwa nauli....
 
yupo mama wa kiarabu..huwa anazunguka maofisini kuomba..yeye anapenda isiwe chini ya elfu 5 tu..na akifika anamuulizia bosi kama anamjua vile..

Yaani,afu mwenyewe nlikuwa na buku jero,nilijilaumuje!!
 
Kuna mdada anakaaga pale maeneo ua UDSM kituo cha daladala
ye kila siku ukimkuta anasema nisaidie nauli nimepungukiwa nauli!!!!!!!!
 
Wandugu,leo nilikuwa nikipita pita katika mitaa ya jiji la Kijani,mitaa ya Uhindini.
Katika kutembea,nikakutana na mama omba omba,amevalia nadhifu kiasi;na anaonekana ni mlemavu wa macho(asiye ona).
Basi,huruma ikaniingia,nikaingia mfukoni na kumkabidhi noti ya sh. 500.
Mama yule aliipokea,akaitazama,kisha akaniambia,"Yaani umeona mimi thamani yangu ni sh. 500?
Nitafanyia nini sasa hiki ki hela?"
Kisha akafungua rambo yake akatupia mle.
Nilichoona mle,da!
Wekundu watupu!!
Ikabidi niondoke kwa aibu,nimekomaje!!
Najuuta!

wala usijiskie vibaya umetoa kwa moyo ndio uliyokuwa nayo. umetoa zaidi kuliko waliotoa hizo elfu kumikumi.
 
Kuna mdada anakaaga pale maeneo ua UDSM kituo cha daladala
ye kila siku ukimkuta anasema nisaidie nauli nimepungukiwa nauli!!!!!!!!

Huyo hana kosa,ilibidi mumuulize anasafiri kuelekea wapi,labda mwenzenu anaelekea Mars!!
Ha ha ha!
Yaani tunako elekea omba omba wenye shida kweli watakosa msaada!
 
wala usijiskie vibaya umetoa kwa moyo ndio uliyokuwa nayo. umetoa zaidi kuliko waliotoa hizo elfu kumikumi.

Double K,noumdr sana ujue kuumbuliwa na omba omba!
Yaani ni kama anakwambia,"wewe ndio ilibidi uwe mfanyakazi wangu"!
 
Last edited by a moderator:
Agalia next time usije ukaachiwa manyoya
 
Hivi hata wale walinzi wanaojisimamisha kwenye parking na kuomba hela ya maji huwa ni omba omba wa white collar eh?
 
Mi siku hzi hata huwa siwaangalii....kuna chuma ulete ukimpa na za fukoni zenda....

Dunia imerudi kwao....siku hizi ombaomba wa ukweli humjui ni yupi, tapeli ni yupi wala wa mazingaombwe ni yupi.....balaaa tupu
 
inasemekana matonya anabonge la mjengo kwao dodoma kuliko hata akina sisi,
 
Back
Top Bottom