Wandugu,leo nilikuwa nikipita pita katika mitaa ya jiji la Kijani,mitaa ya Uhindini.
Katika kutembea,nikakutana na mama omba omba,amevalia nadhifu kiasi;na anaonekana ni mlemavu wa macho(asiye ona).
Basi,huruma ikaniingia,nikaingia mfukoni na kumkabidhi noti ya sh. 500.
Mama yule aliipokea,akaitazama,kisha akaniambia,"Yaani umeona mimi thamani yangu ni sh. 500?
Nitafanyia nini sasa hiki ki hela?"
Kisha akafungua rambo yake akatupia mle.
Nilichoona mle,da!
Wekundu watupu!!
Ikabidi niondoke kwa aibu,nimekomaje!!
Najuuta!