Hii yangu ni tofauti kidogo.
Ilikuwa ni siku ya Presentation, nipo zangu mbele kabisa natoa semina yangu mbele ya Wanafunzi wasiopungua 500.
Wakati nafika pale mbele, nikaanza kusikia hali ya tumboni inabadilika. Nikaendelea zangu kushusha madude, nafika katikati ya presentation naona kama vile nikiongea dude linashuka. Ikabidi nipunguze sauti ya kuongea, lecturer akadai niongeze sauti maana watu hawasikii. Nilipojaribu kuongeza sauti Salaleeh, naona kitu kabisa inaanza kutoka.
Nilipoona hivyo, nikanyamaza kimya kwa sekunde kadhaa huku nimeduwaa. Nikapiga mahesabu chap chap, nikasema ngoja nishuke taratibu.
Kushuka kwenyewe natembea taratibu, kama mtu ambaye mguu mmoja haujakaa sawa. Ile nafika mlangoni nikakimbia puuh! Haa, kitu kinanifata kabisa. Ikabidi nishikilie kwa mkono.
Nafika toilet, watu wamejaa. Ikanilazimu kumwaga uharo sehemu ya kukojoa. Nisingeweza kusubiri tena.
Huku Class watu wanakufa kwa vicheko wakati mwenzio naangamia.
Omba isikukute.