Nakumbuka kipindi ni mdogo alikuja nyumbani pacha mwenzake na mama sasa mzee akanunua kondoo dume kubwa kwa ajili ya mgeni (nilikuwa na miaka kama 8-9 hivi).
Basi kwa vile mgeni alifika usiku na mambo yakafanyika usiku, nilishtushwa na sauti AMKA ULE nikaamka mwanaume nikapiga mkia wa kondoo bila kula ugali wala nini, baada ya mlo nikaenda zangu kitandani kuwazua maisha ya utoto maana nilikuwa nawaza sana enzi hizo.
Kiukweli sikujua kinachoendelea usiku ule nilishtukia kumekucha na nikavaa nguo za shule kwenda masomoni (shule) bila kunawa uso wala miguu.
Ile nafika mlangoni nikasikia mzee "Naombeni mmsaidie huyo tafadhali".
Kichwa kizima,miguu,mikono,shingo, ni uharo mtupu yaani nzi wako nyuma kama vile kuna maandamano.
Niliogeshwa na ndoo mbili za maji, kwenda kitandani walichokiona hakiwezi elezeka kwa awamu hii ya Tano.