Omba usishikwe na tumbo la kuharisha ukiwa katikati mjini na hakuna vyoo karibu

Omba usishikwe na tumbo la kuharisha ukiwa katikati mjini na hakuna vyoo karibu

Usiombe uingie choo cha ugenini alafu uanze kufanya yako kabla hujakagua uwepo wa maji,unamaliza unafungua bomba unasikia upepo tu.ilintokea hyo alafu hakukuwa na wakumuomba maji,nkawaza na kuwazua nkapata akili ya kuvuta maji kwenye bomba kwa mdomo namiminia kwenye kopo mpaka yakatosha
 
Aisee nimecheka ile mbaya lol! Hahahahaha hii funga kazi maana uharo mwili mzima halafu mwenyewe wala hukujistukia! Dah! Chezeya mkia wa kondoo weye!

Nakumbuka kipindi ni mdogo alikuja nyumbani pacha mwenzake na mama sasa mzee akanunua kondoo dume kubwa kwa ajili ya mgeni (nilikuwa na miaka kama 8-9 hivi).

Basi kwa vile mgeni alifika usiku na mambo yakafanyika usiku, nilishtushwa na sauti AMKA ULE nikaamka mwanaume nikapiga mkia wa kondoo bila kula ugali wala nini, baada ya mlo nikaenda zangu kitandani kuwazua maisha ya utoto maana nilikuwa nawaza sana enzi hizo.

Kiukweli sikujua kinachoendelea usiku ule nilishtukia kumekucha na nikavaa nguo za shule kwenda masomoni (shule) bila kunawa uso wala miguu.

Ile nafika mlangoni nikasikia mzee "Naombeni mmsaidie huyo tafadhali".

Kichwa kizima,miguu,mikono,shingo, ni uharo mtupu yaani nzi wako nyuma kama vile kuna maandamano.

Niliogeshwa na ndoo mbili za maji, kwenda kitandani walichokiona hakiwezi elezeka kwa awamu hii ya Tano.
 
Nilibanwa na tumbo la kuhara nafika tu kazini tumekaa kusubiri kupangiwa root ya kwenda tumbo likavuruga nilikimbia mpaka choo mtu binafsi nikazama bila kuuliza yule mama alivyoniona naingia akaenda kuita watu jamani kuna jambazi limekimbilia chooni walipofika mlangoni waliduwaa maana ilikuwa ni paaaptaaaatataa pypyeeeee peyeee nikatoka kimya bila kuongea na mtu
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Inashauriwa kutembea na dawa za kuzuia kuharisha na panadol
Siku hizi nimeanza kutembea na za kuzuia kuharisha aisee!!!
Yaani upo kwenye daladala haswa ile foleni ya kutoka tabata mpaka tazara, sometimes mnawea kaa ata masaa mawili foleni haiendi... Sa ndo hiyo kitu ikukamate hapo... Jamani nilisali Mungu azuie mzigo usishuke mpaka nifike gmboto, watu wanadhani sijui nimefiwa huko...[emoji23][emoji23][emoji23] hapo kijasho chembambaaa kinatiririka toka kichwani...
 
Hii yangu ni tofauti kidogo.

Ilikuwa ni siku ya Presentation, nipo zangu mbele kabisa natoa semina yangu mbele ya Wanafunzi wasiopungua 500.

Wakati nafika pale mbele, nikaanza kusikia hali ya tumboni inabadilika. Nikaendelea zangu kushusha madude, nafika katikati ya presentation naona kama vile nikiongea dude linashuka. Ikabidi nipunguze sauti ya kuongea, lecturer akadai niongeze sauti maana watu hawasikii. Nilipojaribu kuongeza sauti Salaleeh, naona kitu kabisa inaanza kutoka.

Nilipoona hivyo, nikanyamaza kimya kwa sekunde kadhaa huku nimeduwaa. Nikapiga mahesabu chap chap, nikasema ngoja nishuke taratibu.

Kushuka kwenyewe natembea taratibu, kama mtu ambaye mguu mmoja haujakaa sawa. Ile nafika mlangoni nikakimbia puuh! Haa, kitu kinanifata kabisa. Ikabidi nishikilie kwa mkono.

Nafika toilet, watu wamejaa. Ikanilazimu kumwaga uharo sehemu ya kukojoa. Nisingeweza kusubiri tena.

Huku Class watu wanakufa kwa vicheko wakati mwenzio naangamia.

Omba isikukute.
 
Back
Top Bottom