Omba usishikwe na tumbo la kuharisha ukiwa katikati mjini na hakuna vyoo karibu

Omba usishikwe na tumbo la kuharisha ukiwa katikati mjini na hakuna vyoo karibu

Huu uzi nasubscribe kabisaaa ni hatareee....nacheka mwenyewe mpaka naonekana kichaa
 
Mi ilitokea nilipokwenda kwao na mchumba wangu siku hiyo kujitambulisha!
Ile tumemaliza kula tu hali ikagoma nikakimbilia chooni naharisha maji tu.!
Ile namaliza kurudi sebuleni nikabanwa tena safari hii nilijinyea nikiwa mlangoni mwa choo kumsubiri mtu atoke niingie.!
Ilikuwa aibu kubwa ya kufunga mwaka usiniulize kilichotokea baada ya hapo..!
Nnachokumbuka uchumba uliishia hapo kwani sikuwahi kurudi tena wala kumtafuta huyo binti na namba ya simu nilibadiri nikahama na mtaa maana watu wangeinyaka kuwa nilijinyea ukweni ingevuma kuliko ya Bashite na vyeti.
 
Hii yangu ni tofauti kidogo.

Ilikuwa ni siku ya Presentation, nipo zangu mbele kabisa natoa semina yangu mbele ya Wanafunzi wasiopungua 500.

Wakati nafika pale mbele, nikaanza kusikia hali ya tumboni inabadilika. Nikaendelea zangu kushusha madude, nafika katikati ya presentation naona kama vile nikiongea dude linashuka. Ikabidi nipunguze sauti ya kuongea, lecturer akadai niongeze sauti maana watu hawasikii. Nilipojaribu kuongeza sauti Salaleeh, naona kitu kabisa inaanza kutoka.

Nilipoona hivyo, nikanyamaza kimya kwa sekunde kadhaa huku nimeduwaa. Nikapiga mahesabu chap chap, nikasema ngoja nishuke taratibu.

Kushuka kwenyewe natembea taratibu, kama mtu ambaye mguu mmoja haujakaa sawa. Ile nafika mlangoni nikakimbia puuh! Haa, kitu kinanifata kabisa. Ikabidi nishikilie kwa mkono.

Nafika toilet, watu wamejaa. Ikanilazimu kumwaga uharo sehemu ya kukojoa. Nisingeweza kusubiri tena.

Huku Class watu wanakufa kwa vicheko wakati mwenzio naangamia.

Omba isikukute.

Kwa kweli umenivunja mbavu [emoji23][emoji23][emoji23]
Umenikumbusha movie ya zamani ya ki nigeria Usuofia in London!
 
Mi ilitokea nilipokwenda kwao na mchumba wangu siku hiyo kujitambulisha!
Ile tumemaliza kula tu hali ikagoma nikakimbilia chooni naharisha maji tu.!
Ile namaliza kurudi sebuleni nikabanwa tena safari hii nilijinyea nikiwa mlangoni mwa choo kumsubiri mtu atoke niingie.!
Ilikuwa aibu kubwa ya kufunga mwaka usiniulize kilichotokea baada ya hapo..!
Nnachokumbuka uchumba uliishia hapo kwani sikuwahi kurudi tena wala kumtafuta huyo binti na namba ya simu nilibadiri nikahama na mtaa maana watu wangeinyaka kuwa nilijinyea ukweni ingevuma kuliko ya Bashite na vyeti.
hahahhhh wee hii uongo
 
Show ilinikuta natoka lugalo niko ndani ya dala dala,,hapo nimetoka kumix mivyakula kibao,,sah nikashuka pale ubungo nilitembea kwa speed ya light huku viushuz vidogo vidogo vikisindikiza safari ,,,dah hii sitasahau
 
Aaaa ah mmenikumbusha mbali me nilibanwa na tumbo la kuhara kwenye daradara na palikuwa na foleni naelekea home mana nilibana kiasi kwamba nikinyenyuka kwenye seat mzigo unafuata
Aisee niliona bar moja nilishuka Kimya Kimya lakini tayari nilisha inyea boxer. Nilifika namalizia mzigo uliobaki na kuvaa suluari kavu kavu, boxer nikatia kwenye rambo then nikapeleka dump.
Hii kitu Balaaaa
 
Hadithi ya kweli;

Kuna mzee moja alibanwa na uharo akiwa safarini kule kijiji alikuwa anaenda mjini, kama kawaida wazee wa cal me j wanapenda kuvaa rain boot hata wakati wa kiangazi.

Nadhani aliona ni adha kumwita kondakta wa gari lile na kumwambia shida yake, alichokifanya akashusha uharo kwenye suruali.

Kwa vile ni majimaji yakatiririka hadi ndani ya rain boot zake, bhna wee mjini hapakutosha aliposhuka garini alikuwa akitembea unasikia, Chapii chapiii chapiii chapii.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Mwaka 2003 Nlikua ndo nimechaguliwa kujiunga kidato cha 5 Mkwawa School.Usiku kabla ya safari maza akaniandalia nyama mkaango na ndizi zilizopakwa ngano.Nilikula kwa uroho sana mana ndo naiaga Life ya home.Nikapanda hood bus Moshi kuelekea Iringa.Tumbo lilikata kuanzia Mwanga hadi nafika Liverpool nilikoma.Afu pembeni nilikaa na Dada mmoja nae akadai anaenda Mkwawa.Jicho lilinitoka mbaya mbovu aseee.
 
Hii yangu ni tofauti kidogo.

Ilikuwa ni siku ya Presentation, nipo zangu mbele kabisa natoa semina yangu mbele ya Wanafunzi wasiopungua 500.

Wakati nafika pale mbele, nikaanza kusikia hali ya tumboni inabadilika. Nikaendelea zangu kushusha madude, nafika katikati ya presentation naona kama vile nikiongea dude linashuka. Ikabidi nipunguze sauti ya kuongea, lecturer akadai niongeze sauti maana watu hawasikii. Nilipojaribu kuongeza sauti Salaleeh, naona kitu kabisa inaanza kutoka.

Nilipoona hivyo, nikanyamaza kimya kwa sekunde kadhaa huku nimeduwaa. Nikapiga mahesabu chap chap, nikasema ngoja nishuke taratibu.

Kushuka kwenyewe natembea taratibu, kama mtu ambaye mguu mmoja haujakaa sawa. Ile nafika mlangoni nikakimbia puuh! Haa, kitu kinanifata kabisa. Ikabidi nishikilie kwa mkono.

Nafika toilet, watu wamejaa. Ikanilazimu kumwaga uharo sehemu ya kukojoa. Nisingeweza kusubiri tena.

Huku Class watu wanakufa kwa vicheko wakati mwenzio naangamia.

Omba isikukute.
Nimecheka kwa sautiiiiii
 
Nakumbuka kipindi ni mdogo alikuja nyumbani pacha mwenzake na mama sasa mzee akanunua kondoo dume kubwa kwa ajili ya mgeni (nilikuwa na miaka kama 8-9 hivi).

Basi kwa vile mgeni alifika usiku na mambo yakafanyika usiku, nilishtushwa na sauti AMKA ULE nikaamka mwanaume nikapiga mkia wa kondoo bila kula ugali wala nini, baada ya mlo nikaenda zangu kitandani kuwazua maisha ya utoto maana nilikuwa nawaza sana enzi hizo.

Kiukweli sikujua kinachoendelea usiku ule nilishtukia kumekucha na nikavaa nguo za shule kwenda masomoni (shule) bila kunawa uso wala miguu.

Ile nafika mlangoni nikasikia mzee "Naombeni mmsaidie huyo tafadhali".

Kichwa kizima,miguu,mikono,shingo, ni uharo mtupu yaani nzi wako nyuma kama vile kuna maandamano.

Niliogeshwa na ndoo mbili za maji, kwenda kitandani walichokiona hakiwezi elezeka kwa awamu hii ya Tano.
Mkuu wewe hukuharisha ila ulijinyea kabisa!! Dah kazi ipo.
 
Hahaha! Pole sana!!!
Hiyo kitu ikukute chuo alafu ile unakimbilia chooni unakuta majangili washaharibu vyoo vyootee!!! Kudadeki... Huoni ajabu kuachia mzigo juu ya mzigo wa mwingine. I salute uharo aisee!!
Ahsante sana, japo ni miaka mingi iliyopita lakini bado tukio halifutiki kichwani mwangu....
 
Nilikuwa nasafari yakutoka Dodoma kwenda Dar asubuh nimegonga kiporo cha wali maharage swafi njian kuelekea stand tumbo likakoroga nikajikaza mpaka stand ya shabiby choon kuzama nikashusha mzigo mzito nikatoka kukaa dakika tano kitu tena dooh nikazama tena hapo naomba basi lisiondoke nikarud tena trip ya tatu sink likajaa nafkir lilikuwa limeziba kuingia kwenye basi siti za nyuma nyuma viti vya watu watatu me Niko katikati nitumbo kukoroma Kama radi nkaseme kufedheheka ndo huku nikajikaza likiyumba na Mimi nmeyumba kaza kalio mpaka jasho sizungumzi nikafanikiwa kufika Moro kushuka brake yakwanza toi nilishusha mzigo wa kutosha hapo cjala kitu mpaka nafika Dar chamoto nilikiona na sikutumia dawa yoyote nilipona tuu na nikafunga choo Kama siku nne
 
Back
Top Bottom