THE SHADOW ONE
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 1,201
- 1,974
Wanabodi,
Leo nimepata tena fursa kuendelea na makala zangu za Kwa Maslahi ya Taifa, natoa wito kwa viongozi wetu, wawe wanasikiliza kauli za watu wadogo na wa kawaida kama akina sisi, baadhi yetu japo we are nobodies lakini baadhi ya kauli zetu ni very powerful, tukisikilizwa sio tuu tutawasaidia sana, bali pia tutawaepusha na mengi na kulisaidia taifa kwa kuliumbia mema, kwani baadhi ya kauli zetu zina powers za uumbaji na huumba!.
Siku za Jumapili nitakuwa nikipandisha threads za mambo ya powers za imani, kauli na wishes ili kuwajengea watu uwezo wa kutumia nguvu iliyo ndani yao kufanya mambo huku tukiikamilisha Easy Sunday, at easy kwa kuainisha baadhi ya kauli ambazo ni very powerful zenye powers zilitolewa kuzungumzia mambo mbalimbali na kauli hizo zikaja kuyaumba hayo mambo yaliyozungumzwa na yakatokea kweli.
Mada hii ni abstract ya vitu vya kufikirika, vikasemwa na vikaja kutokea kweli. Lengo la kuileta mada hii ni tusidharau watu, wala tusidharau kauli za baadhi ya watu, zina nguvu ya kuumba!.
Kwa sisi Wakristu, kuna mahali Bwana wetu Yesu Kristo, ametufundisha "Ombeni Mtapewa", Tafuteni Nitapata", "Bisheni Hodi Mtafunguliwa"
Anaendelea kufundisha kuwa jambo lolote utakalo omba kwa Baba yangu, kwa jina langu, utapewa, lakini kwa sababu jf ni ukumbi wa dini zote, naomba kuwajulisha kuwa Mungu sio wa dini yoyote, Mungu hana dini, wala hakuna Mungu wa Wakristo, Mungu wa Waislamu, miungu ya Wahindu, Wapagani na wengine wote, Mungu ni mmoja tuu, omnipotent, omnipresent, na omniscience.
Kuna watu waliaminishwa na mafundisho ya dini zao kuwa Mungu yuko juu mbinguni, ameketi kwenye kiti chake cha enzi huko mawinguni, na kwamba mbinguni au peponi ni juu mawinguni. It's not true.
Mungu yuko ndani yetu ndani ya kila binadamu haijalishi ni wa dini gani, baada tuu ya kuumbwa kwa udongo Mungu alitupulizia ile pumzi ya uhai, pumzi ile, life force, ndio yenye Umungu ndani yake.
Hivyo sii kweli mbinguni ni kule juu, mbinguni na duniani ni hapa hapa, ila hii dunia tuliyopo sasa ni ulimwengu wa mwili, na kuna ulimwengu wa Roho, huko ndiko mbinguni, peponi na motoni.
Hivyo ili kuomba chochote kwa Mungu, unaweza kutazama popote sio lazima juu, na unaweza kuomba chochote kwa Mungu bila kulitaja jina lolote na ukapewa!.
Hii maana yake, Mungu ni msikivu sana, ukiwaza tuu kuwa unataka jambo fulani, Mungu tayari anakuwa amesikia, hivyo kuomba kwa kauli hata kwa kuandika tuu popote, kwenye simu, kwenye SMS, kwenye mitandao ya kijamii, etc, huko ni kuliongezea tuu nguvu hilo jambo lako.
Je wajua kuwa baadhi ya kauli za baadhi ya watu zina nguvu ya kuumba?. Niulize mimi!. Mwezi June mwaka 2008, kuna mtu alipandisha uzi humu JF, kuhusu uendeshaji wangu wa piki piki, kwenye uzi huo, kulitolewa kauli mbaya kuhusu uendeshaji wangu wa pikipiki na kuhusishwa na ajali!, huwezi amini mwezi uliofuata, mwezi Julai, nilikula mziga wa kwanza, na mwezi August nikala mziga wa pili wa haja!. Lile bandiko la mwanzo kuhusu uendeshaji wangu wa pikipiki, likafutwa ndipo bandiko la ajali yangu ya pikipiki likapandishwa Pascal Mayalla apata ajali..... hivyo huu ni uthibitisho kuwa kuna baadhi ya kauli huumba!. Nimeanza kuendesha pikipiki 1993, hivyo hiyo 2008 ni miaka 15!, huo ndio ulikuwa uendeshaji wangu na sikuwahi kipata ajali!. Ila baada ya watu wenye kauli za kuumba, kuandika humu JF kuwa naendesha mbio pikipiki nitapata ajali, kauli hizo ziliniumbia hiyo ajali na kweli nikapata ajali!.
Hivyo amini usiamini kauli huumba?. Angalia baadhi ya kauli hizi ziliumba nini?. Laiti wahusika waliotajwa kwenye kauli hizi, wangezingatia haya yaliyosemwa, yaani kauli umba hizi zingesikizwa, labda matokeo yangekuwa ni mengine...
Binadamu tuna mtindo wa kuheshimu hoja zinazotolewa na watu muhimu kwenye jamii na kudharau watu ambao ni nobody. Kwa vile kauli hizi zilitolewa na mtu ambaye ni nobody, no one paid any attention kwa kauli hizi, mpaka pale kauli hizi zilipoumba ndipo watu angalau wakafahamu, lakini very unfortunately, walengwa wa kauli hizi, kama wangezingatia hoja za kauli hizo, labda baadhi yao wangeliwepo hadi leo!.
Naomba nianze na tukio la hivi karibuni.
Mfano Spika JYN, baada ya kuusoma uzi huu Voices from within: Nimesikia sauti, Dr. Tulia Ackson ndiye Spika ajaye! Sauti hiyo imenieleza Ndugai, japo atatamani aendelee lakini... Iwapo JYP angesoma bandiko hilo na kuamua kutogombea Uspika Kwa term nyingine, angeondoka Uspika kwa kuagwa kwa heshima na sio kwa fedheha kama alivyoondoka!.
Hata sasa Spika Tulia, anaweza asijue kuwa usikute yeye kupata Uspika huu alionao sasa ulitokana na kauli ya kwenye bandiko hilo!.
Mwaka 2014, humu JF, kulipandishwa bandiko hili
Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli, by that time, JPM wala hakujua kuwa atakuja kugombea urais.
Muda wa kuchukua fomu za urais CCM ulipowadia JPM alijitokeza kuchukua fomu kwa ku beep tuu, simu ikaitika!.
Hivyo JPM alikuja kuupata urais wa JMT akijijua ni yeye ndiye aliye u beep urais akaupata, bila kujua kuna watu waliishamtolea kauli za kumuumbia urais wa JMT!.
Hata hoja ya udikiteta, baadhi yetu bila kujijua kumuita mtu fulani ni Dikiteta, kumbe ndio tumemuumbia huo udikiteta!. Kauli huumba! Je, ni kweli Magufuli ni dikiteta? Kama ni kweli, ni kosa la nani kati yake na aliyetoa kauli hii?
Amini usiamini, baada ya kupindua kauli, kiukweli kabisa JPM alinza kubadilika, Magufuli is Getting Better and Better, He is Changing for The Better!. Hongera Sana!
Hivyo nikarejea humu JF na kuwaeleza watu humu Trends, Visions: Watanzania msitatizwe na kauli zake kuhusu Katiba, baada ya Nyerere, ni Magufuli ndiye ataacha legacy kubwa ikiwemo Katiba Mpya!.
Baadae Rais Magufuli, so far, is the best president this country has ever had. Msikivu, ana upendo na huruma. Atabarikiwa sana. Tanzania itabarikiwa!
And by the time anatwaliwa from huu ulimwengu wa Mwili kwenda ulimwengu wa Roho, he was almost a saint! Voices From Within: Je, wajua yuko Peponi, Mbinguni, Kwa Baba yake? Why kumshutumu, kumsakama na kumsimanga? Aachwe apumzike kwa amani
The same applies to urais wa Samia, hakuna mtu yoyote alijua kuwa kuna siku rais wa JMT anaweza kufa akiwa madarakani!, hivyo siku zote Makamo wa rais alikuwa anateuliwa tuu bila kumhesabia anaweza kuja kuwa rais wa JMT kwasababu hakuna aliyewahi kufikiri rais wetu anaweza kufa!.
Hivyo naamini hata wakati Samia ni Makamo wa JPM, hakuwahi kuwaza kuwa kuna siku JPM anaweza kuitwa kwa Baba yake na yeye kuwa rais wa JMT!, hivyo ilivyotokea JPM akaitwa Baba yake na Samia kawa rais, watu wote wanajua imetokea tuu, ni mipango ya Mungu, lakini hakuna watu wanaojua kumbe kuna watu, walitoa kauli zenye nguvu ya kuumba, waliomuomba Mungu, wakamuumbia urais wa JMT ili Samia awe rais na kweli Mungu akasikia hivyo kauli hizo zikamuumbia Samia urais, hivyo usikute hata Samia mwenyewe anajihesabu amekuwa rais wa JMT kwa kudra tuu za Mwenyeenzi Mungu, kumbe hajui sio kudra tuu, kuna watu waliomba, na wakapewa!.
Kwanza anza kuangalia ni lini watu walianza kumspot Mama Samia, mimi nilimspot 2010 New Cabinet: Baadhi ya Majina ni Haya Hapa!.
Kisha 2015 Siku ya Wanawake Duniani: Je, tuna Wanawake wenye sifa za Presidential Material?
Then Siku ya Wanawake Duniani: VP Samia Suluhu: "Womanly, Genuine, Humble, Simple na Down To Earth!”
na hili "Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza
Naamini kama JPM angesoma hapa, halafu akaamua tangu ile ile ,2020 angempisha Samia, you never know by now labda...
Hitimisho
Kulikamilisha bandiko na kukuacha na burudani ya easy Sunday, naomba nikuache na kibao hiki cha DDC Mlimani, wana Sikinde ngoma ya ukae, kiitwacho "Utu ni Tabia Njema na Wala Sio Pesa"'
Mtunzi ni Shabani Dede, Mwimbaji ni Cosmas Thobias Chidumule, baadhi ya maneno ya wimbo huo ni
"Nimekumbuka yangu Dunia"
"Maneno Baba alio niambia"
"Fukara Hapendezi mbele za watu hata kidogo"
" Lolote asemalo wao watacheka"
"Na kumuona bure tena hayawani"
Sasa nini maana watadharau na kupuuza"
Chorus
"Utu ni Tabia Njema na wala sio pesa" X 2
Haja ya Mja hunena muungwana ni kitendo
"Dharau Haifai na tena mbaya sana"
"Mtu muone kama mtu sio mpaka awe na kitu"
When you are nobody, hata ukisema kitu, hakitiliwi maanani, natoa wito kwa viongozi wetu, lisemwalo lipo, kama halipo linakuja, mkishauriwa kitu hata na mtu mdogo, ambaye ni nobody,
hakuna ubaya, sio lazima kufuata kila ushauri, ila ni muhimu kuuzingatia ushauri wowote wenye logic ndani yake, unasaidia, unalisaidia taifa na besides everything, unaokoa na unaponya!.
Wasalaam
Paskali.
Maneno huumba hatupaswi kujiambia maneno mabaya, hata kama ni ya utani. Tumeona kauli za watu wa chini zikipelekea anguko kwa serikali tena hata viongozi. Muda unaponya !