Ombi kwa Mohammed Said kuhusu Saigon Club

Saul,
Club ya Saigon haijafa sasa ina umri wa nusu karne.
Hatuchezi tena mpira kwa kuwa tushakuwa sisi si vijana tena.

Baada ya kutoka katika ujana club imebaki kama barza yetu.
Dar Islamic Club ni kitu mbali sana na Saigon.
 
Inna li Llahi wa Inna Ilayhi Rajiun.

Hussein amefariki?

Kuhusu Chico nilipata habari, Allah amrehemu yeye na aturehem nasi pia.
Maalim Faiza,
Hussein yu hai na anasali sala zake hapo Manyema siku zote.
 
Aisee unajua najaribu kukufananisha , mwandiko na hoja zako, sasa ndio nimekuelewa, kumbe ni mdaslaam mwenzetu tena wa mjini sasa ndio nimethibitisha,
Cha kujiuliza mbona alikuwa akija klabuni hapa Pan Africa hakai?
 
Saigoni ya Sasa imebaki kijiwe cha Drafti tu kikiongozwa na Pambwe hakosi (Makosela Draw), Namkumbuka Rafiki yangu Marehemu Maneno...Na Mastory yake Lukuki nasikitika nasikitika nilichelewa kupata habari za kifo chake sababu nilikata mguu kwa muda kiasi... Ila Wamama wa Kariakoo wabaya Sana ndio kina FaizaFoxy wakamuumiza tumbo(Chango?) Masikini alifariki kwa Maumivu sana. Kuna Picha tulipiga pale iliharibika baada ya kulowana na maji... ila Hamisi Msukuma ana copy..
 

Inna li Llahi wa Inna Ilayhi Rajiun.
 
Mlaleo hivyo ndivyo tunavyoitaka club iwe tukutane tucheze draft na dhumna.
Hatujataka iwe kinyume cha hivyo.
 
Mlaleo hivyo ndivyo tunavyoitaka club iwe tukutane tucheze draft na dhumna. Hatujataka iwe kinyume cha hivyo.
Huwa siwaelewi sometimes unakuta mtu ni Imam lakini ana mdomo mchafu wa Matusi hayahadithiki why! au kijiweni ni sehemu ya kupunguzia stress...!

Kinachonifurahisha kukiwa na wazee na muda wa Swala ukifika watu hutawanyika muelekeo wa Masjid...

Ila Mwambieni Funza Yahaya aache Pombe na Awe ana Swali! na awe Msafi
 
Mumba...
Allahuma Amin.

Mumba...
Amin.
yawezekani nimeandika sivyo hiyo sentensi.

Hussein yu hai na Allah ampe maisha tawil.

Waliofariki ni Chico na Garincha..
Hussein yuko msikiti wa Manyema vipindi vyote anaswali hapo.

Humkosi.

AlhamduliLlah ala kuli hal.
 



Kutoka kushoto katibu msaidizi wa Saigon wakati huo marehem Kitwana Mwanamboka (r.i.p) katibu Boi Risasi. Makamu mwenyekiti Juma Spencer. Na Treasurer Mussa Shagow akitoa taarifa ya fedha katika mkutano mkuu 2010
 


Ilikuwa mwaka 2010 wanachama wa Dar es Salaam Saigon wazee wetu waliokaa mbele ya viti kutoka kulia ni katibu Boi Risasi . Mohamed Kiaratu. Mzee Abbas Sykes. Mzee Iddi Simba. Mzee smart Issa Ausi. Sheikh Zubeir na wengineo

 
 
Inasemekana RPC Mohamed Chicco alikuwa na ushirikiano mzuri sana na kunguru ni kweli, na hata mali zake nyingi kazipata kupitia hao kunguru
 
Inasemekana RPC Mohamed Chicco alikuwa na ushirikiano mzuri sana na kunguru ni kweli, na hata mali zake nyingi kazipata kupitia hao kunguru
Ebaeban,
Kuna mtu aliandika maneno mfano ya kwako kuhusu Mohamed Awadh (Chico).
Huyu ndugu yetu akaambiwa kuwa ni uungwana kutomsema maiti.

Maalim Faiza akaongezea akasema taazia huwa haijibiwi lakini lau kama unalo la
kusema ni bora ukafungua uzi mpya.
 


Maalim mohammed said asalam alykum

Ebu naomba unisaidie maelezo ya hiyo picha manake nakuona nawe katika picha hiyo ukiwa pamoja na rais mstaafu alhaj alli hassan mwinyi.

Nimeiokoteza mahali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…