Ombi kwa Mohammed Said kuhusu Saigon Club

Leo ilikuwa ni KHITMA kwenye club yetu SAIGON social club, kurehemu wazee na ndugu zetu wa Kariakoo waliotangulia kwa Mwenyeenzi. Mungu aendelee kutusitiri kwa rehma zake, Amin
 

Attachments

  • 6ea42e21-6439-435b-a295-9263168442d6.jpg
    106.2 KB · Views: 147
  • 2a48462c-f567-484f-a042-56896ce2c88f.jpg
    109.6 KB · Views: 108
  • b17ba052-7484-42e0-a80a-db136a550e91.jpg
    83.5 KB · Views: 134
  • 6ea42e21-6439-435b-a295-9263168442d6.jpg
    106.2 KB · Views: 120
  • b191d9d6-8838-4746-bc01-2f2d04ce7759.jpg
    97.3 KB · Views: 133
  • 925e4f1a-0e3a-4e80-960f-8204c67c18c5.jpg
    121.7 KB · Views: 104
Ndahani,
Naomba ukamilishe swali lako ili nipate kukujibu kwa kuwa
sentensi ya pili hukuikamilisha.
mzee wangu mimi naomba kuuliza hii Saigon club inauhusiano gani na dini ya kiislam?
kwanini function zenu zinafanyika kwa kufuata tamaduni za kiislam?
Je unaona mnawatendea haki wanachama wenu walio na imani tofauti?
 
mzee wangu mimi naomba kuuliza hii Saigon club inauhusiano gani na dini ya kiislam?
kwanini function zenu zinafanyika kwa kufuata tamaduni za kiislam?
Je unaona mnawatendea haki wanachama wenu walio na imani tofauti?
Kayaman,
Saigon asili yake ni Everton na tukivaa jezi za bluu kama Everton
ya Liverpool, Uingereza.

Katika miaka ya 1960 tukiwa watoto wadogo wa Karikaoo wastani
wa umri wetu ulikuwa kiasi miaka 12 mchezo ukiokuwa mashuhuri
kwa watoto wa Kariakoo ilikuwa ni mpira.

Kama unavyojua hii Karikaoo waliokuwa wanaishi hapo walikuwa
Waislam.

Hii club ya Saigon hadi leo unavyoiona wanachama ni walewale
watoto wa 1960 ambao sasa tumekuwa watu wazima.

Sasa sisi ni Waislam na tumeenea katika club yote ingawa hatubagui
wanachama wa dini nyingine kwani wamekuwapo siku zote.

Kuwarehemu wanachama na wazee wetu waliotangulia mbele ya haki
hii ni ada yetu na haikuanza leo ni kitu kipo katika mila na utamaduni
wetu ambao kwa kuwa sisi ni Waislam basi inabidi tufanye shughuli
yetu kama ada yetu ilivyo.

Ndugu zetu wasio Waislam si kama wanajumuika nasi katika hili bali
wanatoa michango ya hali na mali kufanikisha hii dua tuifanyayo kila
mwaka.

Imekuwa hivi miaka yote na wala hawajaonyesha dalili za kukereka.
Waungwana ndivyo walivyo.

Si hili ti bali hata Mwezi Mtukufu wa Ramadhani tunafanya futari na
sote tunakuwa pamoja katika kufuturu.

Hii ndiyo, ''spirit,'' ya Saigon na haijawa tatizo sasa inakaribia nusu
karne.

Inashangaza kuwa wewe si mwanachama lakini roho inakuuma na
unakuja na fitna.

Fitna ni mbaya kuliko kuua.
Fitna inaigawa jamii.
 
Cc.mohammed said
Thomas...
Hii picha ilipigwa mwanzoni 1987 katika kumbukumbu ya Azimio la Arusha
na hapo ni Arusha International Conference Centre (AICC).

Wakati ule nilikuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
Mimi niko karibu ya Abdulrahman Babu kwa nyuma yake.

 

Saul,
Hizi picha ulizoweka hapo juu ni za khitma ya mwaka wa 2010.
Captain Malik ni huyo wa pili kulia hebu angalia picha niliyompiga leo hapo chini.
Naomba radhi ya tarehe katika camera yangu inaonyesha 8 May 2017:

 
Ahsante sana mwalim wangu MS allah endelee kukuweka tuendelee kuchota hekma na historia toka kwenye mohammed said Encyclopidia (MSE)
 
Mchango wowote wa kiuchumi kwa taifa!?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…