Kwako,Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Samia Suluhu Hassan
YAH: MALALAMIKO JUU YA MKURUGENZI WA WILAYA YA BUSEGA NDUGU MAIKO RICHARD KACHOMA
Mheshimiwa Rais,
Kwa heshima na taadhima,Sisi walimu wa halmashauri ya wilaya ya Busega tunapenda kuwasilisha malalamiko yetu kwako, kuhusu hatua zinazochukuliwa na Mkurugenzi wa Wilaya, Ndugu Maiko Richard Kachoma. Tumepokea kwa masikitiko makubwa uamuzi wake wa kupuuza barua ya Katibu Mkuu Kiongozi - Ikulu pamoja na demand notice ya siku 90 inayohusu kututoa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) na kuelekeza makato yetu Chakuhawata.
Hatua hii imeleta changamoto nyingi kwetu walimu, ikiwemo vitisho vinavyotolewa na Mkurugenzi huyu dhidi ya wale taka kuhama CWT na kwenda chakuhawata .
Mheshimiwa Rais,Tunahisi haki yetu ya kuchagua chama cha kututetea masrahi yetu imekiukwa bila sababu za msingi, na hali hii imeleta msongo wa mawazo na hali ya hofu kazini.
Mheshimiwa Rais,Kwa heshima kubwa, tunakuomba Mheshimiwa Rais uchukue hatua stahiki kuhusu walimu waliopigwa marufuku kuhama CWT bila ridhaa yao kwa kitendo cha mkurugenzi ndugu Maiko Richard Kachoma kujifanya msemaji wa CWT,hivyo kufanya maamuzi anayoona yeye yanafaa
Mheshimiwa Rais,Pia, tunakuomba uzingatie hatua dhidi ya Mkurugenzi wa Wilaya, Ndugu Maiko Richard Kachoma, ambaye anaendelea kuchukua maamuzi yanayoathiri vikali ustawi wa walimu na mazingira ya kazi ndani ya wilaya yetu Ikiwemo vitisho,na hivi majuzi alimuandikia barua ya maelezo kaimu katibu wetu wa chakuhawata ndugu Raphael Omondi,yote hii ni kudhoofisha juhudi zetu
Mheshimiwa Rais,Nina imani kuwa, chini ya uongozi wako makini, haki itatendeka na walimu wa Busega wataendelea kufanya kazi kwa amani na ufanisi.
Ahsante