Pole na majukumu mheshimiwa Rais na pole pia kwa msiba wa kuondokewa na watanzania wenzetu 14 huko mkoa wa SIMIYU. Mheshimiwa Rais naandika ombi hili nikiwa na masikitiko ya kuwapoteza hao ndugu zetu. Binafsi sina ninayemjua lakini wale ni watanzania wenzetu na huo ndiyo msingi wa maumivu yangu.
Naandika kukuomba wewe kwa sababu mambo yamekuwa yakizungumzwa kwa muda mrefu bila utekelezaji. Mosi, ni juu ya spidi kali ya magari ya serikali barabarani bila kujali alama za usalama. Hawa wanaopanda magari haya ni ndugu zetu tunawapenda sana lakini pindi wanapopata haya matatizo tunaumia sana. Ikikupendeza utolewe mwongozo tafadhali juu ya uendeshaji wa haya magari. Nasema hivyo kwani pia hata ndugu zetu jeshi la polisi wanaosimamia usalama barabarani hawana muda wa kubishana na hawa watu kwani wengi wao wanatumia madaraka yao.
Pili, naomba kuwepo kwa sheria inayomubana mpita kwa miguu barabarani kwani kwa upande mwingine wapita kwa miguu wamekuwa chanzo cha matatizo ya ajali. Utakuta mpita kwa miguu anakatiza barabara akipiga simu....hii ni hatari sana ...mataifa ya wenzetu mambo kama hayo yanaendana na charges. Unakuta watu wamewekewa vivuko mfano zebra au fly over, mtu hataki kupita ana create njia yake.... napendekeza pwekwe charges dhidi ya watumiaji waenda kwa miguu wasiojali alama za barabarani. Nitatoa mfano mwingi, baruabara zetu baadhi zina taa, utakuta taa ya kijani imewaka inaruhusu magari kupita lakini mwenda kwa miguu hazingatii hata taa.
Tatu, naomba waendesha bodaboda wabanwe kwa sheria kali sana dhidi ya matumizi yasiyo sahihi barabarani. Hwa nao ni chanzo kikubwa sana cha ajali. Serikali itizame watu hawa kwa jicho kali. Kufanya hivyo siyo kuwakomoa , la hasha ni kulinda usalama wao.
Nne, bado kuna shida kwa madereva wa mabasi hususani pindi yarejeapo kutoka mikoani au yafikapo mikoani ile mida ya jioni. Mabasi haya hayazingatii kabisa matumizi sahihi ya barabara.
Naomba kuwasilisha.
AHSANTE