Ombi kwa Rais Samia, tunakushukuru kwa mahubiri mazuri kuhusu haki, tunakuomba utende unachohubiri yasibaki kuwa maneno tuu lakini vitendo ni tofauti

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi
Naomba kuanza kwa angalizo kwa mode kuhusu kuchanganya lugha.

Japo sasa jf ni mainstream media ukichanganya lugha kwenye heading mode ana edit, neno "Mama Don't Preach, practice what you preach " ukilibadili kwa Kiswahili linapoteza maana.
Update:
Mode tayari kafanya yake!
Heading imebadishwa imekuwa hivi
"Rais Samia utende unachohubiri yasibaki kuwa maneno pekee" yaani sasa mwananchi anatoa order kwa Rais wa nchi!. Yaani mimi namuamrisha Rais Samia!. Mode please!.

Jf ni user generated forum, na social media, kama user ametumia maneno ya tamathali za semi za kizungu, please mode, msizibadili! tamathali za semi za kizungu kuwa za Kiwahili!. Acheni members watumie maneno they are comfortable with!.
Na kama ikibidi sana ni lazima kubadili, then please change cautiously angalau basi iwe
"Ombi kwa Rais Samia, tunakushukuru kwa mahubiri mazuri kuhusu haki, tunakuomba utende unachohubiri yasibaki kuwa maneno tuu lakini vitendo ni tofauti "
Hili linakuwa ni ombi na sio amri!

Kama kawa kila nipatapo fursa huja na makala zangu elimishi za Kwa Maslahi ya Taifa.
Leo mada kuu ni kumshukuru Rais Samia kwa kuhubiri haki, yaani preaching kuhusu haki, tunamweleza tunajua kuwa ana nia njema na thabiti ya dhati watanzania wapate, haki zao, kama ni kuhubiri tuu, amehubiri sana!
Tunamshauri sasa kuhubiri tuu itoshe, "Mama Don't Preach, Practice What You Preach!"
Hili ni andiko la imani yangu kwa Rais Samia.
Wanabodi,
Kwa Maslahi ya Taifa kwenye Nipashe ya leo 5/02/2023
View attachment 2507414View attachment 2507416
Makala ya leo, ni kuhusu haki za binaadamu, na kwa wale wenye kumbukumbu mzuri ya safu hii, makala za mwanzo kabisa zilikuwa ni makala mfullulizo za “Kilio Cha Haki” ambazo nilizungumzia sana haki jinai.
  1. Ukosekanaji wa Haki kwenye Mhimili wa Mahakama, kunaweza kuwa kunachangiwa na Majaji/Mahakimu wenye uwezo mdogo kubaini haki?. Hoja hii imejibiwa kwa vitendo na matokeo yameonekana msikilize Rais Samia akizungumzia matokeo hayo
  2. Asante Rais Samia kwa kuwasisitiza watendaji wa vyombo vya haki kuwa haki sio hisani, bali ni stahiki. Watende haki, tubadili Katiba kurudisha haki
  3. Kumbe DPP kutenda haki kunawezekana! Hongera sana, kazi umeianza vizuri. Sasa haki sio tu inatendeka, inaonekana! Kazi Iendelee…
  4. Ushauri kwa DPP: Kutekeleza nia njema ya Rais Samia, kuona Haki ikitendeka; je, tumchagize DPP kutumia Nolle kufuta kesi zote zinazosuasua?
  5. Pongezi kwa DPP Mpya. Kama itampendeza, aanze kwa kutumia Nolle, kusafisha Uchafu wote wa mtangulizi wake...

Mtu unapozungumzia haki jinai namna hii, kisha ukasikia Rais ameunda timu kuangalia haki jinai, iwe makala zako zilichangia au hazikuchangia, haijalishi, lakini kitendo cha kukizungumza kitu kisha kikafanyiwa kazi ni faraja tosha kwako mwandishi.
  1. Rais Samia ana nia njema na ya dhati kwa kauli thabiti na matendo, Watanzania wapate haki, ila imetokea Watanzania hawajui haki zao!. Je tumsaidie Rais Samia na kuelimisha umma Katiba, Sheria na Haki au tuwaachie wenyewe?.
  2. Katiba japo ni kakitabu kadogo ka kurasa 143 tuu, lakini kukaelewa ni shughuli nzito!, ili Watanzania waielelewe katiba, kunatakiwa kufanyika kazi kweli kweli ya uelimishaji umma kuhusu Katiba, sheria na haki.
  3. Tanzania japo tuna wanasheria wengi ambao ni manguli wabobezi na wabobevu wa sheria, lakini wengi hawaijui katiba!.
  4. Serikali tunawasheria wengi manguli wabobezi na wabobevu wakiongozwa na Mwanasheria Mkuu wa serikali ambao walipaswa kuijua katiba vilivyo lakini wengi wao, hawaijui katiba, ndio maana serikali inaweza kutunga sheria batili inayokwenda kinyume cha katiba.
  5. Bunge letu nalo ambalo limeshehenezwa na wanasheria manguli wabobezi na wabobevu, lakini wametunga sheria batili inayokwenda kinyume cha katiba, hivyo Bunge letu na wabunge wetu nao hawaijui katiba kikamilifu.
  6. Mahakama ndio mhimili pekee ambao angalau angalau unaijua Katiba na kuliambia Bunge na Serikali kuwa sheria fulani ni batili kwasababu iko kinyume cha katiba, ila very unfortunately Mahakama haina meno, badala ya kubatilisha sheria batili, ndio kwanza inayarudishia yale yale majinga yaliyotunga sheria batili ndio yaibadilishe!. Hivyo mahakama kwenye kuitekeleza katiba nayo inashikwa na kigugumizi!.
  7. Lakini huku mitaani kuna wanasheshia wa kawaida tuu na taasisi za kisheria, wanaweza kabisa kusaidia kuelimisha umma elimu ya katiba sheria na haki, ili kumuwezesha Rais Samia kutimiza azma yake ya kutaka Watanzania kutendewa haki ni lazima kwanza hawa Watanzania wazijue haki zao.
  8. Hivyo hizi kauli dhabiti za Rais Rais Samia katika utoaji haki, nimeanza kuzifuatilia kwa muda mrefu, na wiki hii amezitoa tena katika matukio makubwa mawili, tukio la kwanza ni siku ya uzinduzi wa Tume ya Haki Jinai jijini Dodoma siku ya Jumatatu iliyopita ya tarehe 30 January na kesho yake tarehe mosi February kwenye Siku ya Sheria jijini Dodoma.
  9. Kwenye utetezi wa haki nchini Tanzania, tukubali tukatae, Rais Samia ana nia njema na ya dhati ya kuhakikisha Watanzania wanatendewa haki kwenye vyombo vya utoaji haki, na moja ya udhaifu mkubwa katika utoaji haki Tanzania, ni Watanzania, hawazijui haki zao!.
  10. Haki hailetwi kwenye kisahani cha chai, haki ni stahili na stahiki inayopaswa kutolewa bila wewe kuiomba, na ikitokea haki haikutolewa au haikutendeka, haki haiombwi, bali inapaswa kudaiwa, sasa ukiwa mtu hujui haki yako, huwezi kudai kitu usichokijua!
  11. Hiki kitu cha Watanzania kutokujua haki zao, nimesikia tena wiki hii, Rais Samia, akirudia kulisema jambo hili, kwenye kilele cha siku ya sheria iliyoadhimishwa kitaifa uwanja wa Chinangali, jijini Dodoma.
  12. Rais Samia, alisema mambo mengi makubwa mazuri katika utoaji haki nchini Tanzania, kubwa nililo ondoka nalo mimi leo katika makala hii ni hili la Watanzania hawajui haki zao!.
  13. Kwenye hili, Rais Samia amesema, na naomba nimnukuu “Wanasema, kuna msemo maarufu kwamba haki hupewi mkononi, lazima uitafute, lakini katika kutafuta haki kuna ujuzi, wananchi wetu wengi hawana ujuzi wa kutafuta haki zao kwa hiyo tuwasaidie kutafuta au kupata haki zao” mwisho wa kunukuu.
  14. Hii sii mara ya kwanza kwa Rais Samia kuzungumzia changamoto ya haki kwa Watanzania wengi wasiojua haki zao, mwaka jana siku maadhimisho ya miaka 10 ya taasisi ya mtandao wa watetezi wa haki za binaadam, THRDC inayoongozwa na mwanasheria, Onesmo Ole Ngurumwa.
  15. Rais Samia alisema, “Mtetezi mkubwa wa haki za binaadamu ndani ya Tanzania ni katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo serikali ndiyo inaitekeleza, ndio sheria mama ambayo haki zote za binadamu wanaoishi Tanzania”.
  16. Rais Samia anaendelea, “swala langu kwenu ni “jee hawa wanadamu tunao watetea, wanaijua hiyo katiba?, na nataka niache kazi kwenu katika eneo la elimu kwa umma, muifanye kazi hii ya kuwaelekeza watu waijue katiba yao, kwasababu wanapodai haki, lazima wajue na wajibu wao, haki ziko kwenye katiba na wajibu uko kwenye katiba wakielekezwa vizuri wataujua na wajibu wao nini kikatiba”, mwisho wa kunukuu. Msikilize Rais Samia mwenyewe
  17. Hivyo hiki ambacho makala hizi zinafanya, kuwaelimisha Watanzania kuhusu haki zao na katiba yao, ni kuwasaidia Watanzania, kulisaidia taifa, na kumsaidia Samia kutimiza nia Njema yake.
  18. Hivyo natoa wito kwa wanasheria kote nchini, haijalishi wewe ni nani kuanzia JM, majaji, mahakimu, mawakili na wasaidizi wa sheria, na bila kujali uko wapi ni mahakamani, serikalini, taasisi za umma, mashirika au wanasheria binafsi, tukiwemo sisi mawakili, sote tumuunge mkono Rais Samia katika kutimiza azma njema ya Rais Samia, kuhakikisha Watanzania wanatendewa haki.
  19. Tume hiyo ya haki jinai inayoongozwa na Jaji Mkuu mstaafu Othman Chande, akisaidiawa na Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu, Balozi Ombeni Sefue, ameipa tume hii miezi 4 kuangalia mifumo ya utendaji wa taasisi zote za utoaji haki na kuahidi kuyafanyia kazi matokea ya Tume hiyo,
  20. Yakiwemo lile “zumari” fulani ambalo Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Juma, alilizungumzia kuhusu zumari hilo lililopigwa kutokea Zanzibar, mlio wake ufike na huku bara,
  21. Rais Samia amesisitiza, kwa vile na yeye ametokea Zanzibar, “Lile zumari litalia, na mimi ni Mpemba, najua sana kupuliza zumari, kwa lile zumari litapulizwa, nitakapo pokea taarifa ya tume, na kusema ndio, mama puliza zumari, nitakwenda kufanya hivyo”,
  22. Hivyo sasa taasisi za haki serikali, pingeni kongole sana kwa Rais Samia, kusikia kilio chenu kilichowasilishwa kwa Rais Samia, na Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma, sasa kaeni mkao wa kula!.
  23. Kauli za vingozi wa kisiasa zinazotolewa kwenye hotuba, ziko za aina mbili, kwanza kiongozi anaandikiwa hotuba, kisha anapewa kuipitia, katika kuipitia huko, huongeza yale yak wake ya moyoni ambayo hakuandikiwa, na pili inawezekana hayo aliyoandikiwa, akakubaliana nayo na kuyangiza mayoni kwake hivyo akihutubia yanakuwa ni ya kwake.
  24. Sisi wasikilizaji wa hotuba za viongozi, pia tuko wa aina mbalimbali, kuna baadhi yetu tumejaaliwa uwezo wa ziada, unaposikiliza hotuba ya kiongozi, unakuwa na jicho la rohoni na sikio la ndani, ambapo kiongozi akisoma hotuba aliyoandikiwa, lakini anayoyasoma hayatoki moyoni kwake, baadhi yetu tunajua!.
  25. Kiongozi anayesoma hotuba aliyoandikiwa, huku hayo anayoyasema, hayatoki moyoni, bali yanatoka mdomoni tuu, wenzetu wazungu wanaita kwa Kiingereza, “paying lip services”, kuna wanasiasa wengi wanatoa hotuba za kuandikiwa, au hata bila kuandikiwa, bali wanasema kile kitu watu wanachotaka kusikia, lakini hakitoki moyoni mwao!.
  26. Ndio maana kwenye mikutano mingi ya kampeni, wanasiasa, wanaahidi vitu vingi, vingine ni vya uongo, au hata vya kweli lakini havitekelezwi!.
  27. Mimi nikimuangalia Rais Samia, na kusikiliza kauli za Rais Samia katika hili la haki, kusema la ukweli kabisa, Rais Samia, ana nia ya dhati kutoka moyoni mwake kuhakikisha Watanzania wanatendewa haki.
  28. Kauli za Rais Samia kuhusu haki sio paying lip services, anamaanisha kabisa hicho anachoongea.
  29. Na kuna msemo “haki huinuia taifa”, hivi hiki anachokifanya Rais Samia kwenye utoaji wa haki Tanzania, Rais Samia ataliinua sana Taifa la Tanzania, hivyo atabarikiwa sana, na Tanzania itabarikiwa sana!.

Mungu Mbariki Rais wetu Samia

Mungu Ibariki Tanzania

Paskali
Update
Hatimaye usaidizi huu, unakwenda kufanyika, kupitia kipindi cha TV kwenye kituo cha Channel Ten, kila siku za Jumapili Saa 3:00 usiku na marudio kila Jumatano saa 9:30 Alasiri.
View: https://youtu.be/ZJIKhnZCf04?si=IXfA8sZkNPxpaeZn
Usikose kuangalia!.
P

Wanabodi,
Nimelipitia bandiko hili na kuumia sana kwa kilichotokea hadi kifo cha huyu Mzee Kibao wa Chadema, ameuliwa kwasababu wananchi hawajui haki zao!. Kama Watanzania wangekuwa wanajua haki zao,
1. Mzee Kibao asingekubali kukamatwa na watu ambao hawatambuliki.
2. Kama Watanzania wangekuwa wanajua haki zao, dereva wa basi la Tashrif asinge kubali kusimamishwa na watu wasiotambulika.
3. Kama Watanzania wangekuwa wanajua haki zao, dereva wa Tashrif angekuwa anajua ile tiketi ya abiria, ni mkataba wa kisheria wa kumshusha abiria wake kituo alicholipia, dereva ana wajibu wa kisheria, duty of care, kuhakikisha usalama wa abiria wake na mali zake kwenye butt ya gari yake!. Mali pekee ambayo ni responsibility ya abiria ni mzigo wake wa mkononi, Hand luggage anaoingia nao ndani ya basi, ndio "abiria chunga mzigo wako" lakini jukumu la abiria kufika salama anapokwenda, dereva wa basi ana wajibu wa kisheria kumfikisha salama.
4. Tanzania hatuna wanasheria mahiri wanoujua haki, tungekuwa nao, familia ya Kibao, inalifungulia basi la Tashrif kesi ya madai ya criminal negligence kupitia vicarious liability kusababisha kifo cha abiria wake!.
5. Watanzania wangekuwa wanajua haki zao, abiria tuu wa kawaida akiwemo abiria aliyekaa seat no. 1 ya basi hilo ambaye ni traffic police, alikuwa na uwezo wa kuwabaini majambazi hao kuwa sio askari police wa kweli na kuwahamasisha abiria wengine wote wasikubali abiria mwenzao atekwe!.
6. Watanzania wangezijua haki zao, wangejua Police haruhusiwi kumkamata mtu yoyote bila kwanza kujitambulisha yeye ni nani na ametokea kituo gani kwa kuonyesha kitambulisho cha polisi.
7. Watanzania wangejua haki zao, wangejua mtu anayekamatwa ana haki ya kusoma number ya kitambulisho na kuihakiki number ya askari police kwenye mfuko wa kushoto wa nguo ya polisi.
8. Wakija polisi ambao ni askari kanzu, hawa hawana uniform hivyo hawavai numbers, hawaruhusiwi kumkamata mtuhumiwa bila kuandamana na polisi wenye uniforms!.
8. Mtu yeyote kabla hajakamatwa lazima awe na arrest warrant na lazima aripoti ofisi ya serikali ya mtaa husika!, aonyeshe arrest warrant atasibdikizwa na mtendaji wa mtaa kuja kukukamata.
10. Baada ya polisi kujitambulisha kwa kuonyesha kitambulisho, kitu cha pili ni kuonyesha arrest warrant na kukumbia
11. "Uko chini ya ulinzi, lazima aseme unakamatwa kwa kutuhumiwa kwa kosa gani?.
12. Polisi atatamka maneno haya " You have the right to remain silent, anything you say may be used for you or against you before the court of law"
Hii maana yake una haki ya kunyamaza kimya, chochote utakachosema kinaweza kutumiwa kama ushahidi wa kukusaidia au kukuangamiza mahakamani!.
13. Kitu cha tatu atakueleza "you have the right to legal representation", una haki ya uwakilishi wa kisheria.
14. Hapo atatoa pingu na kukufunga.
15. Kisha polisi hao watawaeleza hao mashuhuda wanakupeleka kituo gani ili ndugu zako wakufuatilie!.

Na ukifikishwa kituoni kabla hujaandikishwa maelezo unaaelezwa haki zako ikiwemo haki ya legal representation.
Hitimisho
Haki hizi zikifundishwa kwa wananchi, 'wasiojulikana' watapungua, watabaki tuu wale wa pyu pyu kama wa Lissu.

Sote tunajua kwa kauli na matendo, Rais Samia ana nia thabiti na ya dhati watu wapate haki zao, amekuwa akilihubiri hili kwa maneno na vitendo, preaching and preaching and preaching na kuanzisha vitendo, kikosi kazi, tume ya haki jinai, sasa tufike mahali tumshauri Rais wetu, "we had enough of preaching, now she should practice what she preach".

Kwenye kikosi kazi, Watanzania walitaka tufanye mabadiliko madogo ya katiba, minimum reforms ili haki zilizoporwa kinyume cha Katiba zirudishwe, hili Rais Samia ameli Preach, practice ni zero!, ila hajachelewa, there is still room for this kabla ya uchaguzi mkuu wa 2025!.

Watanzania wametaka Tume Huru na Shirikishi ya Uchaguzi, Rais Samia ameibadilisha jina Tume ya Uchaguzi NEC na kuiita jina jipya sasa inaitwa Tume Huru ya Uchaguzi, ila tume bado ni ile ile!. Watanzania hawakuomba jina la Tume ya Uchaguzi libadilishwe kutoka kuitwa Tume ya Uchaguzi na sasa kuitwa Tume Huru ya Uchaguzi, wanataka Tume ibadilishwe iwe ni Tume Huru na Shirikishi ya Uchaguzi na sio kubadilishwa jina lakini Tume ni ile ile, watu ni wale wale na uchaguzi utaendelea kusimamiwa na makada kinda kinakiuka wa chama kubwa ndani ya kofia za ukurugenzi !.

Watanzania walitaka sheria mpya ya uchaguzi yenye kutoa haki sawa kwa wote na uwanja sawa wa uchaguzi, kwasababu sheria ikiyokuwepo ilikuwa ni sheria batili inayokwenda kinyume cha Katiba ya JMT, tumeletewa sheria mpya ya uchaguzi yenye ubatili ule ule ulioshabatilishwa na Mahakama Kuu ya Tanzania kwa kwenda kinyume na katiba!.

Rais Samia, Watanzania tunakupenda, tunakukubali, tunakuomba mahubiri yako ya falsafa yako ya 4R, yasiwe ni mahubiri tuu, preaching only, please put to practice what you preach 🙏
Mungu Akubariki uyaweze yote katika YEYE!.
Mungu Ibariki Tanzania

Paskali
 
Wanabodi,
Nimelipitia bandiko hili na kuumia sana kwa kilichotokea hadi kifo cha huyu Mzee Kibao wa Chadema, ameuliwa kwasababu wananchi hawajui haki zao!.
1. Police haruhusiwi kumkamata mtu yoyote bila kwanza kujitambulisha yeye ni nani na ametokea kituo gani kwa kuonyesha kitambulisho cha polisi.
2. Mtu anayekamatwa ana haki ya kusoma number ya kitambulisho na kuihakiki kwenye mfuko wa kushoto wa nguo ya polisi.
3. Wakija polisi ambao ni askari kanzu, hawa hawana uniform hivyo hawavai numbers, hawaruhusiwi kumkamata mtuhumiwa bila kuandamana na polisi wenye uniforms!.
4. Mtu yeyote kabla hajakamatwa lazima awe na arrest warrant na lazima aripoti ofisi ya serikali ya mtaa husika!, aonyeshe arrest warrant atasibdikizwa na mtendaji wa mtaa kuja kukukamata.
5. Baada ya polisi kujitambulisha kwa kuonyesha kitambulisho, kitu cha pili ni kuonyesha arrest warrant na kukumbia
6. "Uko chini ya ulinzi, lazima aseme unakamatwa kwa kutuhumiwa kwa kosa gani?.
7. Polisi atatamka maneno haya " You have the right to remain silent, anything you say may be used for you or against you before the court of law"

8. Kitu cha tatu atakueleza "you have the right to legal representation", una haki ya uwakilishi wa kisheria.
9. Hapo atatoa pingu na kukufunga.
10. Kisha polisi hao watawaeleza hao mashuhuda wanakupeleka kituo gani ili ndugu zako wakufuatilie!.

Polisi waliokushikia AK47 kwenye paji la uso ambao wanaweza kukuua na kukupa kesi ya ujambazi unaweza kuwaambia maneno hayo?
 
Advocate umeandika utafikiri mgeni na hii nchi!!!!.
Police hawa hawa wa Tz wafate hizo procedure???
 
Sio kwa Tanzania hii mzee...
 
Attachments

  • downloadfile-23.jpg
    downloadfile-23.jpg
    39.6 KB · Views: 5
Wanabodi,
Nimelipitia bandiko hili na kuumia sana kwa kilichotokea hadi kifo cha huyu Mzee Kibao wa Chadema, ameuliwa kwasababu wananchi hawajui haki zao!.
1. Police haruhusiwi kumkamata mtu yoyote bila kwanza kujitambulisha yeye ni nani na ametokea kituo gani kwa kuonyesha kitambulisho cha polisi.
2. Mtu anayekamatwa ana haki ya kusoma number ya kitambulisho na kuihakiki kwenye mfuko wa kushoto wa nguo ya polisi.
3. Wakija polisi ambao ni askari kanzu, hawa hawana uniform hivyo hawavai numbers, hawaruhusiwi kumkamata mtuhumiwa bila kuandamana na polisi wenye uniforms!.
4. Mtu yeyote kabla hajakamatwa lazima awe na arrest warrant na lazima aripoti ofisi ya serikali ya mtaa husika!, aonyeshe arrest warrant atasibdikizwa na mtendaji wa mtaa kuja kukukamata.
5. Baada ya polisi kujitambulisha kwa kuonyesha kitambulisho, kitu cha pili ni kuonyesha arrest warrant na kukumbia
6. "Uko chini ya ulinzi, lazima aseme unakamatwa kwa kutuhumiwa kwa kosa gani?.
7. Polisi atatamka maneno haya " You have the right to remain silent, anything you say may be used for you or against you before the court of law"
Hii maana yake una haki ya kunyamaza kimya, chochote utakachosema kinaweza kutumiwa kama ushahidi wa kukusaidia au kukuangamiza mahakamani!.
8. Kitu cha tatu atakueleza "you have the right to legal representation", una haki ya uwakilishi wa kisheria.
9. Hapo atatoa pingu na kukufunga.
10. Kisha polisi hao watawaeleza hao mashuhuda wanakupeleka kituo gani ili ndugu zako wakufuatilie!.

Na ukifikishwa kituoni kabla hujaandikishwa maelezo unaaelezwa haki zako ikiwemo haki ya legal representation.

Haki hizi zikifundishwa kwa wananchi, 'wasiojulikana' watapungua, watabaki tuu wale wa pyu pyu kama wa Lissu.

Paskali
Hayo uliyosema yako “applicable “ hapa bongo?

Haya kwa hapa bongo labda uwe unatizama “law and order”

Otherwise uwe umeshatembea “mambele”
 
Nimefikiria Jambo lakini niseme tu kama waliomkamata huyo mzee kwenye bus wanahusiana na vyombo vya dolla basi nchi iko salama kabisa labda alilengwa yeye , lakini kwani vyombo vya dolla vinaua watu ?? (Sijui)

Kama waliomkamata hawana uhusiano na vyombo vya dolla basi ni mbaya zaidi sababu hatuko salama. Kwamba pamoja na uwepo wa dolla kuna watu ambao sio dolla wanaweza kufanya kitendo cha hatari kama hicho bila kujificha yani peupe na wasikamatwe wala kujulikana!

Hii inaogopesha sana sana .

Mama Samia katoa maelekezo yake kama amiri jeshi Mkuu ni imani taarifa ya kiuchunguzi itakuja ili kutenda haki na kutupa waTZ Amani .
 
Tatizo hao wanafunzi wenyewe, wengi uwa hawapendi information ambazo zinaweza wanawasaidia siku moja. Sanasana watajibu kwa hoja hayo mambo hayana faida kwao. Wakati safari ya mile 1000 inaanza na hatua moja kwanza.

Kama Tanzania kuna ‘Miranda rights’ ni jukumu la IGP kuhakikisha askari wanafuata hizo taratibu na hatua zina chukuliwa kwa wanaokamata watu bila ya kufuata taratibu.
 
Wanabodi,
Nimelipitia bandiko hili na kuumia sana kwa kilichotokea hadi kifo cha huyu Mzee Kibao wa Chadema, ameuliwa kwasababu wananchi hawajui haki zao!.
1. Police haruhusiwi kumkamata mtu yoyote bila kwanza kujitambulisha yeye ni nani na ametokea kituo gani kwa kuonyesha kitambulisho cha polisi.
2. Mtu anayekamatwa ana haki ya kusoma number ya kitambulisho na kuihakiki kwenye mfuko wa kushoto wa nguo ya polisi.
3. Wakija polisi ambao ni askari kanzu, hawa hawana uniform hivyo hawavai numbers, hawaruhusiwi kumkamata mtuhumiwa bila kuandamana na polisi wenye uniforms!.
4. Mtu yeyote kabla hajakamatwa lazima awe na arrest warrant na lazima aripoti ofisi ya serikali ya mtaa husika!, aonyeshe arrest warrant atasibdikizwa na mtendaji wa mtaa kuja kukukamata.
5. Baada ya polisi kujitambulisha kwa kuonyesha kitambulisho, kitu cha pili ni kuonyesha arrest warrant na kukumbia
6. "Uko chini ya ulinzi, lazima aseme unakamatwa kwa kutuhumiwa kwa kosa gani?.
7. Polisi atatamka maneno haya " You have the right to remain silent, anything you say may be used for you or against you before the court of law"
Hii maana yake una haki ya kunyamaza kimya, chochote utakachosema kinaweza kutumiwa kama ushahidi wa kukusaidia au kukuangamiza mahakamani!.
8. Kitu cha tatu atakueleza "you have the right to legal representation", una haki ya uwakilishi wa kisheria.
9. Hapo atatoa pingu na kukufunga.
10. Kisha polisi hao watawaeleza hao mashuhuda wanakupeleka kituo gani ili ndugu zako wakufuatilie!.

Na ukifikishwa kituoni kabla hujaandikishwa maelezo unaaelezwa haki zako ikiwemo haki ya legal representation.

Haki hizi zikifundishwa kwa wananchi, 'wasiojulikana' watapungua, watabaki tuu wale wa pyu pyu kama wa Lissu.

Paskali
Asante kwa kutujulisha mambo haya muhimu kabisa ila CCM lazima waondoke jamani tumechoka.
 
Hadi tutakapojua tofauti ya mtekaji na mkamataji tungali tupo tupo sana.

Mtekaji anaelewa lugha ya mmasai Ngorongoro siyo hii ya kuwatuliza waombolezaji waziri amalize hotuba.
 
Inaumiza sana kwa kweli!! Dah! But why? Kwa nn umuue mwenzako? Why?

Utaishi milele? Miaka yetu yenyewe ni mifupi tu kwa nn kuingiza laana kwenye familia yako? Why?
 
Wanabodi
Naomba kuanza kwa angalizo kwa mode kuhusu kuchanganya lugha.

Japo sasa jf ni mainstream media ukichanganya lugha kwenye heading mode ana edit, neno "Mama Don't Preach, practice what you preach " ukilibadili kwa Kiswahili linapoteza maana.
Update:
Mode tayari kafanya yake!
Heading imebadishwa imekuwa hivi
"Rais Samia utende unachohubiri yasibaki kuwa maneno pekee" yaani sasa mwananchi anatoa order kwa Rais wa nchi!. Yaani mimi namuamrisha Rais Samia!. Mode please!.

Jf ni user generated forum, na social media, kama user ametumia maneno ya tamathali za semi za kizungu, please mode, msizibadili! tamathali za semi za kizungu kuwa za Kiwahili!. Acheni members watumie maneno they are comfortable with!.
Na kama ikibidi sana ni lazima kubadili, then please change cautiously angalau basi iwe
"Ombi kwa Rais Samia, tunakushukuru kwa mahubiri mazuri kuhusu haki, tunakuomba utende unachohubiri yasibaki kuwa maneno tuu lakini vitendo ni tofauti "
Hili linakuwa ni ombi na sio amri!

Kama kawa kila nipatapo fursa huja na makala zangu elimishi za Kwa Maslahi ya Taifa.
Leo mada kuu ni kumshukuru Rais Samia kwa kuhubiri haki, yaani preaching kuhusu haki, tunamweleza tunajua kuwa ana nia njema na thabiti ya dhati watanzania wapate, haki zao, kama ni kuhubiri tuu, amehubiri sana!
Tunamshauri sasa kuhubiri tuu itoshe, "Mama Don't Preach, Practice What You Preach!"
Hili ni andiko la imani yangu kwa Rais Samia.

Wanabodi,
Nimelipitia bandiko hili na kuumia sana kwa kilichotokea hadi kifo cha huyu Mzee Kibao wa Chadema, ameuliwa kwasababu wananchi hawajui haki zao!. Kama Watanzania wangekuwa wanajua haki zao,
1. Mzee Kibao asingekubali kukamatwa na watu ambao hawatambuliki.
2. Kama Watanzania wangekuwa wanajua haki zao, dereva wa basi la Tashrif asinge kubali kusimamishwa na watu wasiotambulika.
3. Kama Watanzania wangekuwa wanajua haki zao, dereva wa Tashrif angekuwa anajua ile tiketi ya abiria, ni mkataba wa kisheria wa kumshusha abiria wake kituo alicholipia, dereva ana wajibu wa kisheria, duty of care, kuhakikisha usalama wa abiria wake na mali zake kwenye butt ya gari yake!. Mali pekee ambayo ni responsibility ya abiria ni mzigo wake wa mkononi, Hand luggage anaoingia nao ndani ya basi, ndio "abiria chunga mzigo wako" lakini jukumu la abiria kufika salama anapokwenda, dereva wa basi ana wajibu wa kisheria kumfikisha salama.
4. Tanzania hatuna wanasheria mahiri wanoujua haki, tungekuwa nao, familia ya Kibao, inalifungulia basi la Tashrif kesi ya madai ya criminal negligence kupitia vicarious liability kusababisha kifo cha abiria wake!.
5. Watanzania wangekuwa wanajua haki zao, abiria tuu wa kawaida akiwemo abiria aliyekaa seat no. 1 ya basi hilo ambaye ni traffic police, alikuwa na uwezo wa kuwabaini majambazi hao kuwa sio askari police wa kweli na kuwahamasisha abiria wengine wote wasikubali abiria mwenzao atekwe!.
6. Watanzania wangezijua haki zao, wangejua Police haruhusiwi kumkamata mtu yoyote bila kwanza kujitambulisha yeye ni nani na ametokea kituo gani kwa kuonyesha kitambulisho cha polisi.
7. Watanzania wangejua haki zao, wangejua mtu anayekamatwa ana haki ya kusoma number ya kitambulisho na kuihakiki number ya askari police kwenye mfuko wa kushoto wa nguo ya polisi.
8. Wakija polisi ambao ni askari kanzu, hawa hawana uniform hivyo hawavai numbers, hawaruhusiwi kumkamata mtuhumiwa bila kuandamana na polisi wenye uniforms!.
8. Mtu yeyote kabla hajakamatwa lazima awe na arrest warrant na lazima aripoti ofisi ya serikali ya mtaa husika!, aonyeshe arrest warrant atasibdikizwa na mtendaji wa mtaa kuja kukukamata.
10. Baada ya polisi kujitambulisha kwa kuonyesha kitambulisho, kitu cha pili ni kuonyesha arrest warrant na kukumbia
11. "Uko chini ya ulinzi, lazima aseme unakamatwa kwa kutuhumiwa kwa kosa gani?.
12. Polisi atatamka maneno haya " You have the right to remain silent, anything you say may be used for you or against you before the court of law"
Hii maana yake una haki ya kunyamaza kimya, chochote utakachosema kinaweza kutumiwa kama ushahidi wa kukusaidia au kukuangamiza mahakamani!.
13. Kitu cha tatu atakueleza "you have the right to legal representation", una haki ya uwakilishi wa kisheria.
14. Hapo atatoa pingu na kukufunga.
15. Kisha polisi hao watawaeleza hao mashuhuda wanakupeleka kituo gani ili ndugu zako wakufuatilie!.

Na ukifikishwa kituoni kabla hujaandikishwa maelezo unaaelezwa haki zako ikiwemo haki ya legal representation.
Hitimisho
Haki hizi zikifundishwa kwa wananchi, 'wasiojulikana' watapungua, watabaki tuu wale wa pyu pyu kama wa Lissu.

Sote tunajua kwa kauli na matendo, Rais Samia ana nia thabiti na ya dhati watu wapate haki zao, amekuwa akilihubiri hili kwa maneno na vitendo, preaching and preaching and preaching na kuanzisha vitendo, kikosi kazi, tume ya haki jinai, sasa tufike mahali tumshauri Rais wetu, "we had enough of preaching, now she should practice what she preach".

Kwenye kikosi kazi, Watanzania walitaka tufanye mabadiliko madogo ya katiba, minimum reforms ili haki zilizoporwa kinyume cha Katiba zirudishwe, hili Rais Samia ameli Preach, practice ni zero!, ila hajachelewa, there is still room for this kabla ya uchaguzi mkuu wa 2025!.

Watanzania wametaka Tume Huru na Shirikishi ya Uchaguzi, Rais Samia ameibadilisha jina Tume ya Uchaguzi NEC na kuiita jina jipya sasa inaitwa Tume Huru ya Uchaguzi, ila tume bado ni ile ile!. Watanzania hawakuomba jina la Tume ya Uchaguzi libadilishwe kutoka kuitwa Tume ya Uchaguzi na sasa kuitwa Tume Huru ya Uchaguzi, wanataka Tume ibadilishwe iwe ni Tume Huru na Shirikishi ya Uchaguzi na sio kubadilishwa jina lakini Tume ni ile ile, watu ni wale wale na uchaguzi utaendelea kusimamiwa na makada kinda kinakiuka wa chama kubwa ndani ya kofia za ukurugenzi !.

Watanzania walitaka sheria mpya ya uchaguzi yenye kutoa haki sawa kwa wote na uwanja sawa wa uchaguzi, kwasababu sheria ikiyokuwepo ilikuwa ni sheria batili inayokwenda kinyume cha Katiba ya JMT, tumeletewa sheria mpya ya uchaguzi yenye ubatili ule ule ulioshabatilishwa na Mahakama Kuu ya Tanzania kwa kwenda kinyume na katiba!.

Rais Samia, Watanzania tunakupenda, tunakukubali, tunakuomba mahubiri yako ya falsafa yako ya 4R, yasiwe ni mahubiri tuu, preaching only, please put to practice what you preach 🙏
Mungu Akubariki uyaweze yote katika YEYE!.
Mungu Ibariki Tanzania

Paskali
Paskali at his best!
 
Back
Top Bottom