Ombi kwa Sitta, ongea na UKAWA warudi kwa faida ya taifa zima, katiba ni ya wote sio upande mmoja tu

Ombi kwa Sitta, ongea na UKAWA warudi kwa faida ya taifa zima, katiba ni ya wote sio upande mmoja tu

Chris Lukosi

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2012
Posts
4,583
Reaction score
2,944
Ndugu zanguni,

Wabunge karibia 146 wamesusia kikao cha katiba baada ya kuonekana kuwa wale walio wengi wanawabeza na kuwaburuta walio wachache.

Mimi ni CCM damu lakini nimekerwam kuona katiba inayoandaliwa sasa ni kwa ajili ya manufaa ya upane mmoja na sio wote.

Kitendo cha kuwabeza wawakilishi 146 ambao wanawakilisha watanzania si chini ya milioni kumi ni dharau kubwa sana na ni ubakaji wa demokrasia.
Ninaamini kuwa pale bungeni kuna wengine wanakwenda kusaini posho tu hata hawajui nini kimewapeleka , bora wamelipwa basi.

Ni aibu kubwa kuona mbunge anakwenda bungeni kwa shuguli maalum ya kuzomea badala ya kutoa hoja

Hii katiba ni ya wote sio ya chama kimoja ni kwa ajili yetu na vizazi vyetu.

Upinzani sio uadui bali ni emokrasia ambapo kila raia ana haki ya kufuata siasa za chama akipendacho.

Mimi leo naweza kuwa CCM kesho NCCR Mageuzi au hata CUF na hakuna wa kuniuliza kwa sababu ni haki yangu.

Namuomba mwenyekiti wa bunge Mheshimiwa Sita akae chini na ukawa wamalize tofauti warudi bungeni kwa faida ya taifa.

Katiba ikitungwa bila kushirikisha upinzani itakuwa ni kinyume na demokrasia na sio haki kwa watanzania wengine zaidi ya milioni kumi wanaowakilishwa na upinzani.

Tukumbuke kuwa hii ni historia na tuweke historia kwa heshima kila mtu aridhike hata kama wasipopata wakitakacho wawe wameshindwa kihalali bila kinyongo.

Mungu Ibariki Tanganyika...
 
Aongee nao warudi au abebe jukumu kuweka mazingira ya kupatikana kinachokosekana???!!!
 
Nimesoma hoja.
imenifurahisha sana.
imejaa busara na uzalendo mwingi.
lakini siamini kama imeletwa na Chriss.
chriss Lukozi huyu ninayemjua ama mwingine.
jamani wengine igeni. Kwa ajili ya katiba wote tutumie busara na tuweke tofauti zetu chini.
mwigulu najua uko huku. Angalia wanaCCM wenzako wenye akili wanazungumza nini.
Ukiweza waige!
 
Mkuu mimi na wewe tunaimba wimbo mmoja, tofauti sauti tu...

Labda ila wako hauoneshi nini kifanyike na unasisistiza kuongea wakati wangu unataka mwenye nyumba afanye wajibu wa kuondoa,lugha chafu,kuzomeana utoro wa wajumbe na kama hayo!!!!
 
Labda ila wako hauoneshi nini kifanyike na unasisistiza kuongea wakati wangu unataka mwenye nyumba afanye wajibu wa kuondoa,lugha chafu,kuzomeana utoro wa wajumbe na kama hayo!!!!
Mimi nimejumlisha, wewe umenyumbulisha.

Kwa kifupi hili bunge limpoteza heshima kwa lugha zinazotumika
 
Ulichokieleza mleta mada ni kitu cha kiungwana na kinatakiwa kutekelezwa kwa manufaa ya taifa letu bila kujali itikadi za kivyama. Sote tuwe kitu kimoja tubainishe na kuainisha mapungufu na uimara wa rasimu kwa makubaliano yenye hoja za msingi kisha sote tuikie lengo moja kwa pamoja la kuunda katiba yetu.

Kama kuna uwezekano ndugu Chris Lukosi nakushi ujaribu kufanya mawasiliano na viongozi wa ccm hasa kina Wassira, Sitta, Lukuvi, Pinda na wengieo ili uwape ushari huu murua, haijalishi wataupokea ama wataukataa lakini ipo siku watakukumbuka kwa ushari utakaowapa.

Asante kwa mawazo huru.
 
Last edited by a moderator:
Some time kuzungumza na watu kama hawa nai hasara tupu nadhani hakuna haja ya kuhangaika nao wao wanajifanya hawanazo kwa nini wabembelezwa.
 
#chris umeandikiwa au! Sijawahi kupata andiko linalofanana na hili toka kwako.hongera kwa kujitbua. Karibu ukawa.
Mkuu leo umekuwa na akili siku zote unaandika vituko kweli nadhani sasa umeanza kukomaa.
 
Ndugu zanguni,

Wabunge karibia 146 wamesusia kikao cha katiba baada ya kuonekana kuwa wale walio wengi wanawabeza na kuwaburuta walio wachache.

Mimi ni CCM damu lakini nimekerwam kuona katiba inayoandaliwa sasa ni kwa ajili ya manufaa ya upane mmoja na sio wote.

Kitendo cha kuwabeza wawakilishi 146 ambao wanawakilisha watanzania si chini ya milioni kumi ni dharau kubwa sana na ni ubakaji wa demokrasia.
Ninaamini kuwa pale bungeni kuna wengine wanakwenda kusaini posho tu hata hawajui nini kimewapeleka , bora wamelipwa basi.

Ni aibu kubwa kuona mbunge anakwenda bungeni kwa shuguli maalum ya kuzomea badala ya kutoa hoja

Hii katiba ni ya wote sio ya chama kimoja ni kwa ajili yetu na vizazi vyetu.

Upinzani sio uadui bali ni emokrasia ambapo kila raia ana haki ya kufuata siasa za chama akipendacho.

Mimi leo naweza kuwa CCM kesho NCCR Mageuzi au hata CUF na hakuna wa kuniuliza kwa sababu ni haki yangu.

Namuomba mwenyekiti wa bunge Mheshimiwa Sita akae chini na ukawa wamalize tofauti warudi bungeni kwa faida ya taifa.

Katiba ikitungwa bila kushirikisha upinzani itakuwa ni kinyume na demokrasia na sio haki kwa watanzania wengine zaidi ya milioni kumi wanaowakilishwa na upinzani.

Tukumbuke kuwa hii ni historia na tuweke historia kwa heshima kila mtu aridhike hata kama wasipopata wakitakacho wawe wameshindwa kihalali bila kinyongo.

Mungu Ibariki Tanganyika...

Chris Lukosi kwa mara ya kwanza nakushukuru kwa maneno ya busara yenye mwelekeo wa kujenga taifa letu na si kuvunja. Mimi ni mwanaCCM mfu, lakini nakubaliana nawe kwamba wajumbe walio wengi kutoka CCM au wenye mrengo na itikadi ya CCM hawajui kabisa nini hasa kimewapeleka ndani ya bunge maalumu! Wapo wasioweza kuchangia hoja iliyopo mezani! Kazi kubwa kwao ni zomeo zomeo, matusi, jeuri ya chama tawala na uchafu mwingine mwingi ambao kila mtu anayefuatilia bunge maalumu tumeushuhudia! In fact kwa mambo yanayoendelea pale Dodoma ndani ya bunge maalumu naona wajumbe hawa hawastahili hata kidogo kututungia katiba ambayo ni sheria mama.

Ndg yangu Chris Lukosi, katiba ya nchi haina chama, dini, kabila, rangi wala eneo atokako mtu. Leo unashabikia mrengo wa CCM, kesho umepigwa chini na CCM! Katiba sio ya kizazi cha leo utunge katiba ukilenga uchaguzi mwakani 2015! Katiba zaidi ni ya kizazi kijacho miaka 50 au 100 na zaidi ijayo. Kwahiyo mjumbe wa bunge maalum kusema eti anataka apige kura ya wazi ili wapiga kura wake waone amepuga kura ya NDIYO au HAPANA ni kutojua kwa hali ya juu malengo na madhumuni ya kutunga katiba ya nchi.

Katiba haiwezi kutungwa kwa mawazo ya upande mmoja la asha! Watu kwa uhuru bila uwoga wowote wawe na uwezo wa kuchangia hoja zao na mwisho wa siku kwa hoja yenye nguvu ipite bila kujali imetolewa na mjumbe kutoka upande gani.

Juzi kwenye bunge maalumu mjumbe mmoja Mhe. Ismail Raghe amenisikitisha sana pale alipoomba mwongozo kwa Makamu Mwenyekiti wa Bunge maalumu bila kutaja kanuni gani akimtaka kiongozi huyo ya bunge kutowaruhusu tena wajumbe wa UKAWA kurudi ndani ya bunge maalumu! Hata Makamu Mwenyekiti alimpuuza! Hii yote inaonesha kuwa wajumbe wengi kutoka CCM aidha hawaelewi majukumu yao na kwanini wako ndani ya bunge maalumu.

Mungu Ibariki Tanganyika, mungu Ibariki Zanzibar, mungu Ibariki Tanzania.
 
Mkuu mimi na wewe tunaimba wimbo mmoja, tofauti sauti tu...

Chris unadai wewe ni CCM damu unajua maana yake? Yaani kwamba piga ua garaza garaza wewe na ccm ccm na wewe. Ndivyo unavyoamaanisha au lugha tu imeteleza? Infact mabandiko mengi ambayo umekuwa unaweka hapa kwa siku za karibuni yanaonesha kwamba una damu asili ya upinzani. Yaani wewe ni mpinzani kwa asili. Inaonekana kabisa kam kweli upo CCM ni kwa kujilazimisha na si kwa kuwa unaipenda kwa dhati. Wewe ni mpinzani na ingefaa uitendee dhamira yako haki badala ya kuilazmisha iamini kitu ambacho haimini?
 
Ndugu zanguni,

Wabunge karibia 146 wamesusia kikao cha katiba baada ya kuonekana kuwa wale walio wengi wanawabeza na kuwaburuta walio wachache.

Mimi ni CCM damu lakini nimekerwam kuona katiba inayoandaliwa sasa ni kwa ajili ya manufaa ya upane mmoja na sio wote.

Kitendo cha kuwabeza wawakilishi 146 ambao wanawakilisha watanzania si chini ya milioni kumi ni dharau kubwa sana na ni ubakaji wa demokrasia.
Ninaamini kuwa pale bungeni kuna wengine wanakwenda kusaini posho tu hata hawajui nini kimewapeleka , bora wamelipwa basi.

Ni aibu kubwa kuona mbunge anakwenda bungeni kwa shuguli maalum ya kuzomea badala ya kutoa hoja

Hii katiba ni ya wote sio ya chama kimoja ni kwa ajili yetu na vizazi vyetu.

Upinzani sio uadui bali ni emokrasia ambapo kila raia ana haki ya kufuata siasa za chama akipendacho.

Mimi leo naweza kuwa CCM kesho NCCR Mageuzi au hata CUF na hakuna wa kuniuliza kwa sababu ni haki yangu.

Namuomba mwenyekiti wa bunge Mheshimiwa Sita akae chini na ukawa wamalize tofauti warudi bungeni kwa faida ya taifa.

Katiba ikitungwa bila kushirikisha upinzani itakuwa ni kinyume na demokrasia na sio haki kwa watanzania wengine zaidi ya milioni kumi wanaowakilishwa na upinzani.

Tukumbuke kuwa hii ni historia na tuweke historia kwa heshima kila mtu aridhike hata kama wasipopata wakitakacho wawe wameshindwa kihalali bila kinyongo.

Mungu Ibariki Tanganyika...

Well said mkuu, uchache isiwe hoja kwani hata RAIS wa JMT Mh. Jakaya Kikwete ktk uchaguzi wa 2010 hata kama alishinda lakini idadi iliyojitokeza kupiga kura na hatimaye kuchaguliwa kuwa RAIS ni ndogo sana ukilinganisha na idadi ya watanzania wenye umri wa kupiga kura kisheria (18+ years). Je tumbeze kwamba hastahili kuwa RAIS?. Busara inatakiwa kutumika kuliko nguvu.
 
Kwa muelekeo huu mimi binafsi sintaikubali hii katiba mpya kwasababu pamoja na kuwa na mapungufu mengine ila kama ukawa hawatashiriki, pia kama wakipendekeza serikali 2 au 3 na kama hakutakuwa na kifungu kitakachompa haki mwananchi yeyote kumshitaki kiongozi yeyote endapo amekiuka katiba ama sheria yoyote ya inchi wakati wowote na popote ndani ya inchi husika. Pia kuwepo vifungu vitakavyoonesha makosa ya viongozi na adhabu zao. MIMI NI MUUMINI WA SERIKALI 1 KWASABABU NI WAZI KUWA UKIUNGANISHA INCHI 2 UTAPATA INCHI 1 TAIFA 1 SERIKALI 1 KATIBA 1 ARIDHI 1 UZALENDO 1 MTAZAMO 1 NA MUUNGANO HUU DAIMA HUDUMU MILELE! MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Sina chama na sitarajii kuwa mwanachama wa chama chochote ila NINGEPENDA KUFAHAMU HAYA YANAYOJADILIWA HUMU YANAWAFIKIAJE WALENGWA?ME MWENYEWE NILIKUA NAJIULIZA KAMA TZ NI MUUNGANO WA NCHI 2 NYINGINE NI IPI?NASIKIA MOJA INAITWA ZANZIBAR
 
Aongee nao warudi au abebe jukumu kuweka mazingira ya kupatikana kinachokosekana???!!!

Sitta mwenyewe MNAFIKI tu, hana lolote la maana, kwani hujui auma ilhaal akipuliza...!?

Kama ulimfuatilia jana alichoongea kabla au baada ya yule pimbi / hasadi / fatani Lukuvi tayari utakuwa uishakubaliana nami.

Hana lolote yule, alisimama na kuwananga/ kuwaponda na dhihaka nyingi kisha kupigiwa mikofi na wale Kenge wanyonya damu mule kwenye jumba la starehe.
 
Sina chama na sitarajii kuwa mwanachama wa chama chochote ila NINGEPENDA KUFAHAMU HAYA YANAYOJADILIWA HUMU YANAWAFIKIAJE WALENGWA?ME MWENYEWE NILIKUA NAJIULIZA KAMA TZ NI MUUNGANO WA NCHI 2 NYINGINE NI IPI?NASIKIA MOJA INAITWA ZANZIBAR

Pole sana, watakujibu maana wangine wamo humu na kwa kuchelea aibu hawaingii kwa majina yao kamili/ halisi.

Unaposikia wanakuambia maneno haya yameishaenea kwenye mitandao, ilitakiwa hapo uiname na kisha ufikiri na utie akili.

Ama unaye mmoya ambaye waamini ni mlengwa na humu hakuna wa kumfikishia ujumbe....!?

Kama ndivyo tusaidie jina ili ujumbe umfike kwa njia nyangine.

Na ntarejea.
 
ukawa ni ubaguzi kwa watanzania wenye kuona mbali kwani hawa ukawa kila tukio ni lazima waje na jina jipya tunawajua. pia wewe kujiita ccm ni unafiki sawa na wanaukwa tu. ukwa wamehisi kushindwa sasa wanatangulia aibu isiwapate, walitarajia tofauti na wanavyooona sasa acha kumsumbua mh. sita kwa sababau ya hawandugu.
 
Sina chama na sitarajii kuwa mwanachama wa chama chochote ila NINGEPENDA KUFAHAMU HAYA YANAYOJADILIWA HUMU YANAWAFIKIAJE WALENGWA?ME MWENYEWE NILIKUA NAJIULIZA KAMA TZ NI MUUNGANO WA NCHI 2 NYINGINE NI IPI?NASIKIA MOJA INAITWA ZANZIBAR
Kwa njia hiihii ya mtandao wa jf ka kuthibitisha hili nenda kapitie hansards za bunge la Jamhuri ya Muungano nafikiri baada ya uteuzi wa Nkamia kuwa waziri/naibu waziri(?), utajiridhisha na nilihokisema. Kwa kifupi ni kwamba Nkamia alitaka mtandao wa jf ufungiwe kwa sababu alizozitaja mwenyewe (sizikumbuki), na siyo yeye tu pia kuna wana ccm wengi waliwahi kuiponda jf na kupendekeza ifungiwe.
 
Back
Top Bottom