Chris Lukosi
JF-Expert Member
- Aug 23, 2012
- 4,583
- 2,944
Ndugu zanguni,
Wabunge karibia 146 wamesusia kikao cha katiba baada ya kuonekana kuwa wale walio wengi wanawabeza na kuwaburuta walio wachache.
Mimi ni CCM damu lakini nimekerwam kuona katiba inayoandaliwa sasa ni kwa ajili ya manufaa ya upane mmoja na sio wote.
Kitendo cha kuwabeza wawakilishi 146 ambao wanawakilisha watanzania si chini ya milioni kumi ni dharau kubwa sana na ni ubakaji wa demokrasia.
Ninaamini kuwa pale bungeni kuna wengine wanakwenda kusaini posho tu hata hawajui nini kimewapeleka , bora wamelipwa basi.
Ni aibu kubwa kuona mbunge anakwenda bungeni kwa shuguli maalum ya kuzomea badala ya kutoa hoja
Hii katiba ni ya wote sio ya chama kimoja ni kwa ajili yetu na vizazi vyetu.
Upinzani sio uadui bali ni emokrasia ambapo kila raia ana haki ya kufuata siasa za chama akipendacho.
Mimi leo naweza kuwa CCM kesho NCCR Mageuzi au hata CUF na hakuna wa kuniuliza kwa sababu ni haki yangu.
Namuomba mwenyekiti wa bunge Mheshimiwa Sita akae chini na ukawa wamalize tofauti warudi bungeni kwa faida ya taifa.
Katiba ikitungwa bila kushirikisha upinzani itakuwa ni kinyume na demokrasia na sio haki kwa watanzania wengine zaidi ya milioni kumi wanaowakilishwa na upinzani.
Tukumbuke kuwa hii ni historia na tuweke historia kwa heshima kila mtu aridhike hata kama wasipopata wakitakacho wawe wameshindwa kihalali bila kinyongo.
Mungu Ibariki Tanganyika...