Ombi kwa Sitta, ongea na UKAWA warudi kwa faida ya taifa zima, katiba ni ya wote sio upande mmoja tu

Ombi kwa Sitta, ongea na UKAWA warudi kwa faida ya taifa zima, katiba ni ya wote sio upande mmoja tu

Pole sana, watakujibu maana wangine wamo humu na kwa kuchelea aibu hawaingii kwa majina yao kamili/ halisi.

Unaposikia wanakuambia maneno haya yameishaenea kwenye mitandao, ilitakiwa hapo uiname na kisha ufikiri na utie akili.

Ama unaye mmoya ambaye waamini ni mlengwa na humu hakuna wa kumfikishia ujumbe....!?

Kama ndivyo tusaidie jina ili ujumbe umfike kwa njia nyangine.

Na ntarejea.

Nikusaidie kidogo kwamba humu jf wamo wengi tu wanaingia kwa majina bandia lakini kuna baadhi yao wanatumia majina halisi kwa kutaja wachache ni Anna Tibaijuka, Mwigulu Nchemba, Nape Nnauye, na wengineo wengi tu.

cc: Mbochele
 
Last edited by a moderator:
jamaa bwana wamegundua msingi wao zanzibar wanadai wanaenda kuanziapo mikutano pole wee, jambo usililijua ni sawa na usiku wa giza
sasa ukawa wataisoma namba
 
nikisoma post hizi nakumbuka Prof Lipumba aliposema tunawaachia Intarahamwe kikao chao...hahaaaaaaa ...yaaani maneno yale yatakaa akilini mwangu siku nyingi sana..watunge katiba wanayoitaka basi ila UKAWA hakuna kurudi nyuma ..
 
warudishe jasho la wananchi ndipo waende zanzibar

Walicho kifanza ni kikubwa sana, acha wachukue tu, hata kama ni kuwachangia tupo radhi ili kukomesha upuuzi na dhereu na dhihaka za wachache waliobeba nchi.
 
Jameni mwenye nö za simu za Chris lukosi ampigie na kumtarifu kuna mtu anatumia ID yake huku!
 
Post ya leo imenifurahisha kweli,msg imeshawafikia walengwa,taifa hili linajengwa na watu wote.
 
Sina uhakika kama ile misukule kule Dodoma itaelewa hii lugha uliyoiandika hapa...
 
Ndugu zanguni,

Wabunge karibia 146 wamesusia kikao cha katiba baada ya kuonekana kuwa wale walio wengi wanawabeza na kuwaburuta walio wachache.


Mimi ni CCM damu lakini nimekerwam kuona katiba inayoandaliwa sasa ni kwa ajili ya manufaa ya upane mmoja na sio wote.


Kitendo cha kuwabeza wawakilishi 146 ambao wanawakilisha watanzania si chini ya milioni kumi ni dharau kubwa sana na ni ubakaji wa demokrasia.
Ninaamini kuwa pale bungeni kuna wengine wanakwenda kusaini posho tu hata hawajui nini kimewapeleka , bora wamelipwa basi.

Ni aibu kubwa kuona mbunge anakwenda bungeni kwa shuguli maalum ya kuzomea badala ya kutoa hoja


Hii katiba ni ya wote sio ya chama kimoja ni kwa ajili yetu na vizazi vyetu.


Upinzani sio uadui bali ni emokrasia ambapo kila raia ana haki ya kufuata siasa za chama akipendacho.


Mimi leo naweza kuwa CCM kesho NCCR Mageuzi au hata CUF na hakuna wa kuniuliza kwa sababu ni haki yangu.

Namuomba mwenyekiti wa bunge Mheshimiwa Sita akae chini na ukawa wamalize tofauti warudi bungeni kwa faida ya taifa.

Katiba ikitungwa bila kushirikisha upinzani itakuwa ni kinyume na demokrasia na sio haki kwa watanzania wengine zaidi ya milioni kumi wanaowakilishwa na upinzani.

Tukumbuke kuwa hii ni historia na tuweke historia kwa heshima kila mtu aridhike hata kama wasipopata wakitakacho wawe wameshindwa kihalali bila kinyongo.


Mungu Ibariki Tanganyika...

Ama kweli uzalendo halisi wa watu wa eneo hili haupo katika Tanzania bali Tanganyika.
Ona watu hawa waongeavyo toka mipyoni mwao, wameweka u-vyama pembeni. Wamegoma kabisa kuingizwa kayikaagerza ya fikara, magereza ambazo zingefinya uhuru wao wa kufikiri kwa ku pre-empty vichwa vyao na kufanyiwa planting ya mahitaji kundo la wahafidhina wachache.
Ukimkuta Lokosi ndani ya Tanzania unaweza kumchukia lakini ukimkuta ndani ya Tanganyika utamkubali tu
 
Mbochele husika na nukuu hii hususani kwenye mkolezo wa wino wa kijani.

Mkuu Skype binafsi huvutiwa sana na mpangilio wako wa lugha.....back to the topic, nimegundua kuwa kumbe intarahamwe huwa wapweke sana pindi wasaliapo wenyewe kwenye kile kiota maalum cha uumbaji wa sheria mama.
 
Last edited by a moderator:
Sasa unategemea nini kama wote wenye hoja mzuri wanaambiwa wamemtukana baba wa Taifa?

Kwa mantiki hii ya CCM hata kuandika katiba mpya ambayo haina mchango na maoni ya waasisi wa Muungano lazima tutaambiwa katiba MPYA imemtukana baba wa Taifa.
 
Hii move ya ukawa isiangaliwe kijuuujuu ina athari kubwa kwa,siasa za kimataifa, statement aliyoitoa Prof. LIPUMBA kwamba kuna kundi la “Intarahamwe” inatuweka pabaya kama taifa, ni busara kufanya maridhiano.
 
MUNGU MKUBWA japo Sina hakika kama kweli ni Lukosi huyu karejewa na ufahamu.
 
Back
Top Bottom