Ombi kwa Wachambuzi wa michezo wa radio

Ombi kwa Wachambuzi wa michezo wa radio

Jacobus

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2011
Posts
4,703
Reaction score
1,724
Wakuu,

Hakuna asiyefahamu kuwa hivi sasa pana mgao wa umeme nchini hivo nawaba sana sana wachambuzi wetu wa michezo radioni kuipa heshima ligi yetu ya mpira wa miguu.

Kipindi kinaanza tatu kasoro robo hivi asubuhi mpaka saa tano (Wasafi FM) na mwengine saa tatu kamili asubuhi mpaka saa sita kamili (E FM) lakini habari wanayoingumzia mwanzoni ni ya j2 mpaka leo mpaka umeme unachukuliwa na wenyewe.

Nawashauri wawe na utaratibu wa kuanza na mechi zilizochezwa hivi karibuni, mfano jana palikuwa na mechi mbili za ligi nazo ni Geita na Tabora na Mashujaa dhidi ya Singida sasa wote hao wameng'ang'ana kwa kuanza kipindi kuelezea mechi ya j2 kati ya Simba na Yanga mpaka umeme ukachukuliwa saa nne.

Badilikeni.
 
Tafuta karedio kadogo vile vya BT speaker vinahifadhi chaji na vipo hadi vya sola utasikiliza habari zote kama unapenda radio.
 
Back
Top Bottom