Ombi la Dharula : CAF ichunguze haraka vyumba vya kubadilishia nguo kwenye uwanja wa Martyrs Kinshasa

Ombi la Dharula : CAF ichunguze haraka vyumba vya kubadilishia nguo kwenye uwanja wa Martyrs Kinshasa

Mpira una matokeo matatu sasa kama wao walienda kucheza bila kujua hili au wewe mtoa mpost umepost bila kujua hili basi visingizio vyako ni sahihi kwako
 
Upo uwezekano mkubwa sana kwa chumba ambacho timu yetu ya simba ilipewa kuwekewa kitu kibaya , haiwezekani Simba kucheza vile , ni lazima kutakuwa na kitu kimefanyika , hii si ile simba tunayoifahamu , napinga vibaya sana .

Na kwa hili ni lazima timu ya AS VITA ifungiwe maisha , hii michezo ya kupuliza dawa za usingizi kwenye vyumba vya timu pinzani imepitwa na wakati

Nakala - Ismail Aden Rage
Acha kuuchafua mpira.Wachezaji mlionao wamechoka wote ni vizee.Mliambiwa mnanunua wahenga mkabisha.Leo mnavuna mlichopanda.Acha uongo.Kila siku mbona mnalia lia? Nendeni CAS mkakate rufaa.Wazee wakulialia.Kila siku nyinyi tuu mnaoonewa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usiwe na ushabiki wa kishamba hatuna timu ya ushindani kama unavyodhani.

Ulijua Simba atamfunga AS Vita? Uwe unatumia akili vizuri basi, siyo kisa una mahaba na Simba basi hata akili nazo uwape.

Mimi huwa ni shabiki msema ukweli sina konakona kama nyoka.

SIMBA HATUTAPATA POINT HATA MOJA KWENYE MECHI ZA UGENINI. Ukitaka meza ukiona chungu tema.
Wachezaji karibia wote ni 35+ walishatumika kila mahali unafikiri utashindaje.As Vita ni timu kubwa sana.Roul Shungu ni kocha mkubwa sana lakini ni kocha msaidizi pale, Uchebe hata CV take in ya kutafuta kwa tochi lkn ndo kocha mkuu simba unategemea nini? Unajifanya kwenda huku huna breki!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukinukuu maneno ya ovyo nawe unakuwa wa ovyo. Hebu kama kweli maneno haya aliyasema Manara mwache na maneno yake wewe endelea na busara zako. Nilishasema Timu za Tanzania zinafeli kuanzia menejimenti hati uwanjani. Angalau upande wa walimu pale ambapo hawaingiliwi na menejimenti. Huwezi kuwa na Msemaji wa timu asiyejua aongee nini wakati gani? Masuala mengi anayoongea Msemaji wa Yanga, Simba, Mtibwa au Ruvu Shooting hayapaswi kusemwa na yeye.

Sent using Jamii Forums mobile app
Msemaji wasYanga Dismas Ten usimfananishe na Manara na hao wengine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
AS Vita ikirekebisha makosa ya umalizaji, kwa mchina Simba atapigwa kuanzia 3 kwenda juu. Jana AS Vita wangetulia vizuri Simba alikuwa anakufa kama 8 hivi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakika tulizidiwa kila mahali.Kaduguda anatudai cjapati.WaKongo walikumbuka rambirambi za mafisango mara wakasema leo Simba atapata taabu saana.Uongo mtupu babake Simba tulihororoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Banyamulenge wa M23 walikuwa wanajitwangia tuu simba watakavyo, kwa hiyo walikuwa wanacheza huku wamesinzia? mipira walikuwa wanaionaje!!?? hakuna timu ya kizembe kama simba, wamekariri kucheza pasi fupi fupi hata wanapokutana na mafundi kama vita.Wao wanajitamba kwenye ukurasa za kijamii za timu mahasimu kama mbabane, nkana na juzi wakaangukia pua kwa vita eti wana KAGERE, CHAMA, BOKO nk wakati wenzao timu nzima imesheheni watu wenye vipaji na phisique ya hali ya juu,, wakati simba wanashindia chips wenzao vita asubuhi wanakula supu ya POPO , mchana ugali na nyama ya NYANI na jioni Ugali na MAPANKI (MIFUPA) ya sangara utawaweza wapi?
 
Jana ilikuwa bahati mbaya, kwenye mpira lolote linaweza kutokea.
(Mtani jana ni bora ungevaa jezi nyekundu)
IMG-20190119-WA0006.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwan manara kashatoa tamko?icho ndo tu nasubiri wana msimbanzi ayo mengine maneno tu
 
Mkuu mimi ni Simba ila kubali tu wachezaji wetu walishindwa kujiamini ikapelekea kucheza chini ya kiwango.

Tujipange kwa mechi zinazokuja tukianza kufikiria hivyo vitu hatutofika popote.
 
Acha kuuchafua mpira.Wachezaji mlionao wamechoka wote ni vizee.Mliambiwa mnanunua wahenga mkabisha.Leo mnavuna mlichopanda.Acha uongo.Kila siku mbona mnalia lia? Nendeni CAS mkakate rufaa.Wazee wakulialia.Kila siku nyinyi tuu mnaoonewa?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanini usiache uchunguzi ufanyike ili ukweli ujulikane mkuu ?
 
Back
Top Bottom