KERO Ombi la hatua dhidi ya matumizi ya lugha chafu katika Stendi ya Mwendokasi Mbezi kwa Nabii Mashimo

KERO Ombi la hatua dhidi ya matumizi ya lugha chafu katika Stendi ya Mwendokasi Mbezi kwa Nabii Mashimo

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
YAH: OMBI LA HATUA DHIDI YA MATUMIZI YA LUGHA CHAFU KATIKA STENDI YA MWENDOKASI MBEZI YALIYOTOLEWA LEO JUMAMOSI YA TAR3 OCTOBER 2026 NA NABII MASHIMO

Ndugu viongozi na mamlaka husika,
Ninaomba kutoa malalamiko kuhusu tukio nililolishuhudia katika stendi ya Mwendokasi Mbezi, ambapo mhubiri alikuwa akitoa mahubiri yenye kutumia maneno machafu na yasiyofaa mbele ya abiria na wananchi mbalimbali, wakiwemo watoto.

Ninaamini kila mtu ana haki ya kuabudu na kutoa mahubiri kwa mujibu wa sheria, lakini uhuru huo unapaswa kuambatana na kuheshimu maadili, utu na utulivu wa jamii, hasa katika maeneo ya umma yanayotumiwa na watu wa makundi na rika mbalimbali.

Naomba mamlaka husika ilichunguze suala hili na kuchukua hatua stahiki ili kuhakikisha maeneo ya stendi yanatumika kwa utulivu na shughuli zinazofanyika hapo hazivunji maadili wala kuwasumbua wananchi.

Lengo langu si kuzuia uhuru wa mtu wa kuabudu, bali kuomba lugha chafu na kauli zisizofaa zidhibitiwe katika maeneo ya umma, kwa maslahi ya wananchi wote.

Nawasilisha malalamiko haya kwa heshima na kwa nia ya kulinda utu, maadili na amani katika maeneo yetu ya umma.

Asanteni kwa kulifanyia kazi jambo hili.
 
Daudi Mashimo unabii anatoa wapi?
Yule dogo kichaa na tapeli.
Dogo utapeli kaanza zamani sana, laana ya kudhulumu watu tangu akiwa mgambo wa jiji wanamwaga vyakula vya mama lishe, bidhaa za machinga n.k.
 
Sauli ndie baadae alikuja kujulikana kama mtume Paulo

Jamaaa alikua chinja chinja wakristo

Hata Malaya anaweza kugeuka akatangaza injili galilaya
 
Sauli ndie baadae alikuja kujulikana kama mtume Paulo

Jamaaa alikua chinja chinja wakristo

Hata Malaya anaweza kugeuka akatangaza injili galilaya
Kwa taarifa yako Daudi wakati anafanya hayo alikuwa tayari mlokole anasali kabisa la TAG Ubungo Msewe.
The only difference he was not priest yet, but an ordinary born again christ believer. Not a self proclaimed prophet.
Siyo kwamba alibadilika akabatizwa na kuwa mlokole baadaye.
 
Sawa mkuu nimekuelewa
 
Back
Top Bottom