Ombi la kurejeshwa kwa mada maalum ya waliotekwa ama waliopotea

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Will due respect
Naomba uongozi wa JF utafakari tena uamuzi wa kuifuta mada husika niliyoiweka hivi karibuni
Ni mada inayohusika na uhai wa watu .. Kwenye dunia hii hakuna kitu cha thamani kama uhai kwakuwa hakuna vipuri vya uhai
Naomba with all due respect mada husika iweze kurudishwa ili JF ionekane ni sehemu ya kuunga mkono dhidi ya udhalimu wa utekaji na mauaji yanayoendelea nchini
Naamini kati ya wengi waliotekwa, kupotea ama kuuliwa wamo pia wanachama, wapenzi na wafuasi wa jukwaa letu pendwa la JF

JF ina watu wa kila aina na wenye habari za kila aina kwenye kila kitu .. Na ndio maana kwasasa inachukuliwa kama chanzo cha uhakika cha taarifa nyingi (credible source)
Naamini kwa dhati ya moyo mada husika ingeachwa hewani zingekuwa zimeshapatikana taarifa nyingi na pengine nyeti juu ya hali tuliyo nayo kwasasa kuliko kila wakati kuwa na mada nyingine mpya
Waliotekwa, waliopotea, waliopotezwa na waliouawa ni sehemu ya JF kwakuwa JF ni ya wote.. Naomba sana tuitoe kifungoni mada husika kuonesha support yetu kwa hao wahanga wote wa natukio tajwa
Kwa heshima na tadhima
Kwa uhai na ustawi wa JF
Naomba ikuwasilisha

Ndimi mjoli wenu
Mshana Jr
Kilingeni Msata
September 12 2024
 
Andika tena na ku post
 
Ewe Kigagula wa Msata umeleta wazo zuri sana. Ila sisi wanazi wa CCM tunakukumbusha tu uende Chato ukatubu dhambi zako za kumsagia kunguni Dkt Magufuli kusema alikuwa anatuma watu kutekwa na kuuawa na baada ya kifo wewe ni mmoja ya mlioshangilia na mkasema sasa mauaji mwisho hahaha. Tuliwaambia watekaji na wauaji walikuwa kundi la wahuni ambao lengo lilikuwa kuharibu urais wa Dkt Magufuli kiasi kwamba hata Dkt Samia aliwaunga mkono hao wahuni kwa kusema eti sasa viroba hakuna hahaha kumbe wanasubiri mambo yao yakikwama waanze tena. In short utawala wa Dkt Samia ni kama wa Commodus wa enzi za Roman Empire.
 
Umeandika ujinga
 
Kuandika mada lukuki mitandaoni,kuandamana mitandaoni,kutukana mitandaoni hakusaidii!
Watanzania tutafakari hatua za kuchukua zaidi ili tujinusuru na roho hizi za kikatiri ambazo Shetani kwa kutumia vyombo vya Ulinzi na Usalama amezimwaga kwenye nchi yetu.
 
Matukio kama haya yanayoendelea nchini yote tungeyaweka kwenye mada husika
Andika tena na ku post
Sikuwa na backup ndio maana nimeomba wairudishe
 
Matukio kama haya yanayoendelea nchini yote tungeyaweka kwenye mada husika
Andika tena na ku post
Sikuwa na backup ndio maana nimeomba wairudishe
View attachment 3093727
Ungekuwa karibu ningekuzaba makofi fasta liwe fundisho kwa wahuni ka wewe
Mbona vayolensi tenaπŸ˜‚
 
Huyu Jr nilishamvua nyota kitambo sana, siasa zinamfunika ufahamu wake ila tu kuna watu humu huwaambii kitu juu yake
 
Matukio kama haya yanayoendelea nchini yote tungeyaweka kwenye mada husika
Andika tena na ku post
Sikuwa na backup ndio maana nimeomba wairudishe
View attachment 3093727
Unajua ni vitu vingapi vimeshiriki mpaka ukaweza kuandika reply yako hapa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…