Ombi la kuteuliwa kuwa Kamishna wa Petroli na Gesi



Nasikia anatafutwa Mzanzibari .
 
Hata kama hujawa Commissionner lakini unapaswa kupsta nafasi ya kutoa mchango wako kwa Taifa lako Zuri la Tanzania!

Hongerasana Brother
 
Mara unataka ubunge mara unataka ukamishna wa gesi na petroleum.
Huyu kijana haijui CCM vizuri.

CCM inataka counterfeit intellectuals , ukiingia na expertise na integrity kwao sio kigezo muhimu.

Kigezo muhimu ni kwanza ukubali kuacha kutumia akili zako na pili ukubali kupokea maelekezo kwa yoyote hata asiye mtaalam katika eneo ulilobobea.

Kijana nilimshauri angeenda shule akiweza abakie hukohuko kinyume na hapo akirudi afungue firm yake kwa ajili ya mambo ya consultations .
 
Humuitaji raisi kukuweka pale, bali unaitaji wananchi au rasilimali watu kukuweka pale unapotaka..

1.Je uko tayari kuwatumikia wananchi?

2. Je! Wewe uu mzalendo au sii mzalendo?

3.Financially status yako ikoje?

4. Kuna kitu kinaitwa bureaucracy? Katika kazi hasa sekta kama hiyo, je! Wewe umejipanga vipi kutokomeza huo mfumo kabisa endapo ukiwa na dhamana? ( Majibu kwa maneno yasiyozidi 30 )

5. Changamoto za mafuta na gesi, je! Ni watu, ni mfumo, au ni vyama au chama ndio kisababishi cha hiyo hali.

6. Una experience yeyote katika kitengo unachotaka kukifanyia kazi?

Asante.......📝
 
Nashukuru sana kwa maswali yako mazuri yenye ufahamu. Nina furaha kutoa majibu yaliyojaa taarifa za kina kwa faida ya wadau wote wa jukwaa hili.

Nikianza na swali la kwanza napenda kusema ukweli nipo tayari kwa moyo wangu wote kuwatumikia wananchi wa Tanzania. Nimejitoa kwa hilo na ninaamini katika uwajibikaji na kuleta mabadiliko chanya katika sekta ya mafuta na gesi kwa manufaa ya taifa letu.

Mimi ni mzalendo wa kweli. Ninaipenda nchi yangu ya Tanzania, nina wapenda watanzania na nina dhamira ya dhati ya kuchangia katika kuleta maendeleo, ustawi, na heshima kwa taifa letu.

Hali yangu ya kifedha inaruhusu kutekeleza majukumu yangu bila kuingiliwa na masuala ya kifedha, hivyo kuwezesha uwajibikaji wangu kwa umakini.

Ninatambua changamoto za bureaucracy. Kama nikipewa nafasi nitatumia mifumo ya kielektroniki kuboresha ufanisi na nitasisitiza uwazi na uwajibikaji, na kushirikiana na wadau kufanya marekebisho yanayohitajika katika sekta ya mafuta na gesi.

Changamoto za mafuta na gesi katika taifa letu zinaweza kutokana na mfumo uliopo, usimamizi wa watu, na mwingiliano wa vyama vya kisiasa. Nitachunguza kwa kina kubaini chanzo na kuchukua hatua kwa kushirikiana na wadau.

Ingawa sina uzoefu wa moja kwa moja katika nafasi hiyo ya ukamishna wa petroli na gesi, uelewa wangu wa kina katika masuala ya mafuta na gesi utaniwezesha kuleta mabadiliko chanya na kufanya kazi kwa ufanisi.

Ahsante sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…