Ombi la kuteuliwa kuwa Kamishna wa Petroli na Gesi

Leo nimeona report ya mwenendo wa matumizi ya gesi tangua ilipoanza kutumika toka mwaka 2004 tumetumia futi za ujazo b700 mpaka mpaka mwaka huu (miaka 20) wakati zilizogundulika ni futi za ujazo trillion 57 kibubu kipo cha kutosha tunahitaji watu wenye weledi mkubwa kusimamia hii rasimali muhimu kwani inachangia 70% ya uzalishaji umeme
 
Mkuu ninashukuru sana kwa maneno mazuri sana na kwa kuonyesha nia ya kusaidia. Hakika unaonekana una moyo mwema wa kuwainua vijana wa kitanzania hasa wanao onyesha kile walichonacho kinachoweza kuleta matokeo chanya katika taifa letu. Na niseme tu kwamba ninathamini sana fursa za kujifunza na kuungana na watu muhimu kwenye sekta yetu ya mafuta na gesi.

Lakini pia ninashukuru sana kwa kusoma CV yangu na kutoa mawazo yako mazuri.

Kuhusu hatua yangu ya masomo na dhamira ya kufikia kiwango cha PhD, siku zote ninaamini kwamba elimu ni njia muhimu ya kujenga msingi thabiti wa maarifa ili kuchangia katika maendeleo ya taifa letu. Lakini pia ninaelewa kwamba safari ya masomo ya PhD inaweza kuchukua muda mrefu (miaka 4 hadi 5). Hivyo kwasasa, nimesimamisha masomo ili nipate kuwatumikia watanzania wenzangu kidogo.

Nashukuru Mungu niliweza kuzungumza na supervisor wangu na kumweleza hali halisi kwamba ningependa kuendelea na masomo mara baada ya kutumia maarifa haya kidogo niliyoyapata. Hivyo ningependa kukwambia kwamba, mimi nipo tayari kuwatumikia Watanzania muda wowote ule kuanzia sasa.

Asante tena na tena kwa kutambua juhudi zangu. Napenda kumalizia kwa kusema kwamba mimi nipo tayari kuungana na watanzania wenzangu wakati wowote kwa kufanya kazi kwa bidii na uzalendo wa hali ya juu ili kufikia malengo ya taifa letu.
 
Mkuu asante sana kwa kutuletea taarifa hii muhimu katika jukwaa hili. Ni kweli gesi asilia ni rasilimali muhimu sana inayochangia kwa kiasi kikubwa katika uzalishaji wa umeme katika taifa letu tangu serikali ilipowasha mitambo ya kuzalisha umeme wa gesi.

Kuna umuhimu mkubwa serikali yetu kuendelea kuimarisha mfumo wa usimamizi wa gesi asilia ili kuhakikisha matumizi yake ni endelevu na yanawanufaisha watanzania wote. Uhakiki wa mara kwa mara wa mikataba na makubaliano na kampuni zinazohusika na uzalishaji na usambazaji wa gesi ni wa muhimu pia.

Pia, kuna umuhimu wa kuwekeza zaidi katika miundombinu ya kusafirisha na kuhifadhi gesi ili kuhakikisha uzalishaji na usambazaji unafanyika kwa ufanisi. Kuendelea kukuza soko la gesi ni muhimu pia kwa kuendelea kuvutia wawekezaji na kuhakikisha upatikanaji wa uhakika wa gesi kwaajili matumizi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na viwandani, kwenye magari na matumizi ya nyumbani.

Kutoa taarifa kwa uwazi kuhusu matumizi ya gesi na faida zinazopatikana ni hatua nyingine muhimu. Hii ni pamoja na kutaja wazi kiwango cha gesi kilichopo, ili kuwawezesha wananchi kuelewa jinsi rasilimali hiyo inavyoendelezwa na kuleta manufaa kwao.

Mwisho kabisa kuwekeza katika elimu na mafunzo kwa wataalam na watendaji katika sekta ya nishati ni jambo jingine la kuzingatia ili kuongeza weledi na ufanisi.

Hatua zote hizi zitaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kusimamia na kutumia vizuri rasilimali ya gesi, ambayo inachangia asilimia 70 ya uzalishaji wa umeme katika taifa letu.
 
Kuwa finyofinyo Kwanza
Mkuu nipatie hii siri yaani niweje mimi nipo flexible mkuu. Kiukweli nipo tayari kujifunza kwa yeyote yule ili mradi tusaidiane kuchangia chochote tulichonacho ili kusukuma mbele guruduma la maendeleo ya taifa letu.
 
Na sio tu uthubutu,huyu ndugu ni MAHIRI kwenye sekta hii.
Mkuu wangu nashukuru sana kwa moyo wako mwema. Pia namshukuru Mungu kwakukuonyesha kitu kidogo nilichonacho. Mungu akubariki sana mkuu wangu. Hakika Mungu akubariki wewe na familia yako.
 
Hakika una stahili katka nyuzi zako zote hzo Basi mama akuone una kitu unakijuwa kwenye nishati na gesi

Kila kheri manager wa makampuni
Asante kwa maneno yako mazuri mkuu wangu hakika yanatia moyo sana.
Ahsante sana.
 
Hello my dear sister, first of all accept my sincere congratulations.

Wewe ni mtu, I can see from your writing. Uko vizuri. CV inajieleza kwa maandiko. Pambania ndoto zako na tunakuombea.
 
Meneja wa Makampuni, hongera kwa udhubutu uliouonyesha. Bahati mbaya watu wenye nia nzuri, ubobezi, uchapakazi na wanyoofu hawatakiwi. CV haitoshi bila connection.
 
Hello my dear sister, first of all accept my sincere congratulations.

Wewe ni mtu, I can see from your writing. Uko vizuri. CV inajieleza kwa maandiko. Pambania ndoto zako na tunakuombea.
Hello mkuu wangu,

Nashukuru sana sana kwa pongezi nyingi na maneno mazuri ya kutia moyo, kiu na hamasa. Nimezipokea zote kwa moyo wangu wote.

Nitajitahidi sana kadri niwezavyo kuhakikisha napambania ndoto zangu, na nawashukuru sanasana kwa maombi yenu.

Pia nishukuru tena kwa kunitia moyo mkuu.
Ahsante sana.
 
Meneja wa Makampuni, hongera kwa udhubutu uliouonyesha. Bahati mbaya watu wenye nia nzuri, ubobezi, uchapakazi na wanyoofu hawatakiwi. CV haitoshi bila connection.
Asante sana kwa pongezi na maneno mazuri ya kunijenga ili nivuke kwenda hatua nyingine ya kimtazamo.

Ni kweli kabisa safari ya kufanikiwa katika maisha inahitaji zaidi ya ujuzi na uzoefu ulionao. Hapa hata vijana wenzangu wanapaswa kutambua hili katika jukwaa hili, kwamba connection ni kiungo muhimu sana sana wakati wa kupambania ndoto yako.

Hivyo mkuu naomba kusema kwamba umeniongezea kitu kikubwa sana katika mtazamo wangu.

Nimepokea ushauri huu kwa moyo wangu wote na ninakuahidi katika mapambano yangu ya maisha nitajitahidi kuchanganya si tu ujuzi na uzoefu bali pia kutafuta, kujenga na kudumisha connection.

Asante sana kwa ushauri mzuri mkuu.
 
Mkuu nafasi za bodi sasa unaweza kuapply. Tuma maombi yako huko uwe kwenye bodi ufanye mabadiliko unayoyatamani.
 
Mkuu nafasi za bodi sasa unaweza kuapply. Tuma maombi yako huko uwe kwenye bodi ufanye mabadiliko unayoyatamani.
Ahsante sana kwataarifa mkuu wangu nimeshaanza mchakato wa kutuma maombi. Nitahakikisha natuma maombi mapema sana.

Ahsante sana
 
Kuhusu timu yetu ya taifa naomba sanasana nilichokiandika kwenye andiko hili walau kianze kufanyiwa kazi:
 
Utekelezaji wa ilani utauzingatia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…