Ombi la Ulaya kwa China: Mshaurini Putin asitishe vita Ukraine

Ombi la Ulaya kwa China: Mshaurini Putin asitishe vita Ukraine

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
4,016
Reaction score
6,759
Charles Michel, Rais wa Baraza la Ulaya, amekutana na kuzungumza na Rais Xi Jinping katika ziara yake rasmi nchini China. Katika mkutano huu.

Michel alimwomba Xi kutumia ushawishi wa Beijing kwa Russia ili kusitisha vita nchini Ukraine.

Ombi hili la afisa wa juu zaidi wa Ulaya kwa Rais wa China linaonyesha kufeli kwa nchi za Magharibi katika kuihami Ukraine dhidi ya Russia. Ulaya pamoja na Marekani, wametumia nyezo zao zote hasa vikwazo vya pande zote dhidi ya Russia katika mgogoro wa Ukraine ili kuishinda Moscow katika mgogoro huo, lakini safari ya Rais wa Baraza la Ulaya nchini China na ombi lake kwa Beijng kutumia ushawishi wake kwa ajili ya kusimamisha vita huko Ukraine ni sawa na kukiri nchi za Magharibi kwamba zimefeli na kushindwa mkabala wa Russia.

Konstantin Vorontsov, mtaalamu wa masuala ya kimataifa wa Russia, anasema kuhusu jambo hili kwamba: "Magharibi imetoa kila kitu hata aina mbalimbali za satelaiti zake kwa Ukraine. Huu ni mchakato hatari sana ambao umeripotiwa kwa Umoja wa Mataifa."

Sambamba na safari ya Charles Michel nchini China, ndege za kivita za nchi hiyo na Russia zilifanya mazoezi ya kupaa kwa pamoja, jambo ambalo limetajwa kuwa ni aina fulani ya kutunisha misuli na kuonesha muungano na umoja wa Beijing na Moscow dhidi ya madola ya Magharibi.

Korea Kusini imetangaza kuwa anga yake imekiukwa; hata hivyo Russia imekanusha madai hayo na kutangaza kuwa, hakuna anga ya nchi yoyote iliyokiukwa.

Ijapokuwa hadi sasa Russia na China hazijazungumzia lolote kuhusu muungano wa kijeshi baina ya pande hizo mbili, lakini utekelezaji wa baadhi ya mipango ya kijeshi kati ya nchi mbili hizo unaonyesha kuwa, zinajiandaa kwa tishio lolote la Jumuiya ya Kijeshi ya Nchi za Magharibi (NATO).

Kwa sababu, NATO imedhamiria hasa kupanua eneo lake la kijiografia upande wa Masharikki, na mgogoro wa Ukraine ulisababishwa na msisitizo wa Marekani wa kupewa uanachama Ukraine katika jumuiya ya NATO, jambo ambalo Russia inalitambua kuwa ni tishio kwa usalama wake.

Ali Bigdeli, mtaalamu wa masuala ya kimataifa, anasema kuhusu suala hili kwamba: "Russia inahisi kutishiwa sana na upanuzi wa NATO kwenye mipaka yake; Uchina pia ina hali kama hiyo katika maji ya Bahari ya Kusini, kwa sababu ya uwepo wa meli za kivita za Marekani katika eneo hilo.

Kwa sababu hiyo Moscow na Beijing zinakabiliana na vitisho vya pamoja na zinajiandaa kwa hali yoyote ile inayoweza kujitokeza."

Kwa hiyo safari ya Charles Michel nchini China, wakati Ulaya ikelekea kwenye msimu wa baridi kali, inaonesha udhaifu mkubwa wa nchi za bara hilo mbele ya hali ya kuendelea mgogoro wa Ukraine na athari zake mbaya kwa mahitaji ya nishati, suala ambalo limechochea maoni ya umma na watu wa Ulaya dhidi ya sera za misaada ya nchi za Magharibi kwa Ukraine ambazo zimezidisha mgogoro wa uchumi barani Ulaya.

Hii ina maana kwamba, maoni ya wananchi barani Ulaya yanautambua mgogoro wa Ukraine kuwa ni mtego wa Washington kwa nchi za bara hilo, ambapo kwa kuzitumbukiza pande hizo mbili kwenye vita, sasa Marekani imeiweka Ulaya katika hali ngumu ya vikwazo katika maeneo tofauti na kuvurugika hali ya maisha ya watu wa bara hilo.
 
Ukraine hata kama kapoteza sio habari manake wao sio wavamizi.
Habari inakuja pale kwa mvamizi anayejiita superpower anapopigika🤔
Hivi katika vita, mfano upande mmoja wamekufa wanajeshi 6, vifaa 10 vimeharibiwa, nk na upande mwingine wanajeshi 3 wamekufa na vifaa 3 vimeharibiwa, hapo utasema ni upande upi umepigwa? Vita inalinganishwa kwa njia hiyo, mfano Tz tulipopigana na Uganda tulishinda vita, je katika hali hiyo hakuna wanajeshi waliokufa na vifaa nk vya Tz vilivyoharibiwa nk? Kumbuka huwezi kushinda vita cleanly bila na wewe kupata hasara na Russia katika hali hiyo haiwezi kuwa UNIQUE.
 
Hivi Urusi kipindi cha karibuni imefanya nini kupambana na vikosi vya Ukraine zaidi ya kushambulia tu miundombinu ya umeme na maji;Huku wao Urusi wakipoteza wanajeshi wengi na vifaa vya kijeshi frontline?🤔
......
Kwani Urusi anapigania wapi? Ndani ya Ukrein au Rusia? Km kapoteza kiasi hicho iweje aendelee kuwepo ndani ya Ukrein si angesharudi kwao? Mnamezeshwa propaganda za kitoto km mataahira mnapokea tu
 
Hivi Urusi kipindi cha karibuni imefanya nini kupambana na vikosi vya Ukraine zaidi ya kushambulia tu miundombinu ya umeme na maji; huku wao Urusi wakipoteza wanajeshi wengi na vifaa vya kijeshi frontline?🤔
......
Usinichagulie sehemu wala silaha ya kukupigia hii ndo vita,,,,,mbona mmarekani alipoona anakaribia kutolewa kamasi akaamua tu kuangusha nuclear Japan.......kwani mjapan alimwambia atumie silaha gani kumpiga
 
[emoji116]
20221206_215955.jpg
 
Hivi katika vita, mfano upande mmoja wamekufa wanajeshi 6, vifaa 10 vimeharibiwa, nk na upande mwingine wanajeshi 3 wamekufa na vifaa 3 vimeharibiwa, hapo utasema ni upande upi umepigwa? Vita inalinganishwa kwa njia hiyo, mfano Tz tulipopigana na Uganda tulishinda vita, je katika hali hiyo hakuna wanajeshi waliokufa na vifaa nk vya Tz vilivyoharibiwa nk? Kumbuka huwezi kushinda vita cleanly bila na wewe kupata hasara na Russia katika hali hiyo haiwezi kuwa UNIQUE.
Umeelezea vyema
 
Kwani Urusi anapigania wapi? Ndani ya Ukrein au Rusia? Km kapoteza kiasi hicho iweje aendelee kuwepo ndani ya Ukrein si angesharudi kwao? Mnamezeshwa propaganda za kitoto km mataahira mnapokea tu
Bora umeyaona
 
Hivi Urusi kipindi cha karibuni imefanya nini kupambana na vikosi vya Ukraine zaidi ya kushambulia tu miundombinu ya umeme na maji; huku wao Urusi wakipoteza wanajeshi wengi na vifaa vya kijeshi frontline?🤔
......
Whatever it is lakini deaths na other damages zinaendelea kutokea.

Marekani inavyowaua viongozi wako wa Afrika ni sehemu ya war tactics au?

Tuache kushabikia hizi moves za hawa mahasimu. Tumkemee Russia, na tuikemee NATO tena ikiwezekana tuwazomee wote kwa pamoja.

Vita ni upumbavu mkubwa wa wanadamu wanaojifanya wana akili sana
 
Fact
 
Back
Top Bottom