Uchaguzi 2020 Ombi maalum kwa Muhashamu Askofu Bangoza, PhD

MIXOLOGIST

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2016
Posts
14,311
Reaction score
36,056
Baba Askofu,

Nimesoma nyaraka zako nyingi unazozitoa kwa kwa Watanzania wote. Kimsingi, ujumbe wako ni fikirishi, thabiti na hitimishi. Thamani ya ujumbe wako ni wa-kiungu unaoishi na kubeba kweli isiyopingika.

Kwakuwa wewe ni mtumishi wa Mungu na hakuna shaka Mungu anafanya kazi ndani yako, mimi kama mguswa nina ombi maalumu.

Naomba uzikusanye nyaraka zako na kuziweka pamoja kwa mfumo wa kitabu ili zidumu na zisambae kwa walengwa kwa urahisi.

Aidha, ninzidi kukutia moyo uendelee kufanya kazi ya Bwana bila kuchoka kama walivyofanya mitume wenzako akina Pauli na Peter ambao nao walitoa nyaraka nyingi kwa jamii zao katika wakati wao.
 
Kama walivyofanya mitume wenzako akina Pauli na Peter ambao nao walitoa nyaraka nyingi kwa jamii zao katika wakati wao.'

Kweli mkuu umeongea neno zito na muhimu sana.
Hizo nyaraka za Peter na Pauli zilikuwa za siasa kama za Bagonza?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…