Ombi maalum kwa wale tu wanaonipenda na kuvutiwa nami sana kiuwasilishaji wangu hapa JamiiForums

Ombi maalum kwa wale tu wanaonipenda na kuvutiwa nami sana kiuwasilishaji wangu hapa JamiiForums

Tafadhali kutokana na nyie kila mara (kwa upendo na mapenzi yenu nami) mnaamua kueleza hisia zenu kwangu na kunisifia na kuishia kuhusishwa nami kuwa hizo ID's zenu ni zangu (mimi GENTAMYCINE), nawaombeni acheni kunisifia huko ili kutowakera wanaonichukia. Badala yake muwe mnaanzisha tu threads za kunisema vibaya ili wafurahi na waridhike wao, sawa?

Na mkiweza zaidi badala ya kunianzishja threads za kunisifia hapa JamiiForums, basi mimi GENTAMYCINE nawaomba muwe mnatumia muda wenu huo wa upendo na kunipenda kwenu kwa kuniombea baraka zaidi na nyingi kwake Baba Muumba Mwenyezi Mungu (Mungu wa Ibrahim, Isaka na Yakobo) ili niendelee kuwa na tofauti kubwa na wapumbavu wote wenye chuki na husuda nami mjukuu wa Mtemi wa Wazanaki wa (mkoani Mara) nchini Tanzania. Na pia mwenye damu tukuka ya Kitutsi tokea mkoani Gisenyi nchini Rwanda bila ya kuisahau na damu ya Kimakuwa (Mtwara).

Asante Mwenyezi Mungu kwa baraka!
👀
 
Mkuu!
unajishtukia bure tu ahahah
humu jokes nyingi!

uwepo wako ni muhimu kwetu, mungu akubariki & tuzidi kuombeana
 
Back
Top Bottom