Ombi maalum kwa wanasheria popote walipo

Ombi maalum kwa wanasheria popote walipo

Nelson Masaduki

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2017
Posts
346
Reaction score
380
Wanabodi,

Nchi hii ina Wanasheria lukuki na siamini kama wananchi wote tunafahamu masuala hayo ya sheria ila ni muhimu tufahamu. Kwa kupitia forum hii, naomba watusaidie kufahamu ukomo wa jinai ya mtu. Kwa mfano kama hizi tuhuma tuhuma za kufukua fukua makaburi. Nchi isije kuingia katika hasara kama kesi hizo hawatashinda Jamhuri.

Msaada tafadhali.

Nelson
14/11/2017
Dar es Salaam
 
Jinai ina ukomo wake kwa kutegemea sheria zilizopo, kwakua sheria ina sifa ya ku look foward yaan siku inapoputishwa ndio ita dili na makosa ya kuanzia siku hio iliyopitishwa kwenda mbele na haitarudi nyuma ata siku moja, unless iseme wazi mfano wa sheria za mauaji ya kimbari, ukwepaji kodi, ulipwaji mikopo nk nk.

Sasa kama mtu alifanya jinai 1943 alaf sheria ya jinai ya leo ya 1968 na haikuandika mahala kudili na jinai za nyuma basi mtu uyo atakua free au mahakama inaweza kutumia tu busara kumuhukumu na kwa kutumia sheria za wakat huo kwa dharura kuu.

Ya Nyalandu hayana ubishi yumo ndani ya muda na kama kweli alifanya na sio kuchafuana tu.
 
Back
Top Bottom