Ombi: Tujumuike na kuwajibika kuenzi umoja wetu watanzania

Ahsante ,lakini bado pia tunaonesha kutokua tayari kurudi kwenye mstari ndugu.Naona tunaendeleza zaidi kuchokonoa kidondonda badala ya kutibu kidonda. Makosa yalitokea,tumeafanya makosa na walifanya makosa. Tunafanyaje kutka hapa..njia sahihi ni kukubali kurudi chini na kuanza upya
 
Nadhani tunaweza kuacha hisia na tukajikita kwenye jambo jema nililo omba. Tupunguze kumvalisha mtu uzanzibar au utanganyika bali tuvae utanzania.
 
29october25 ulipoteza hata ndugu mmoja?
 
Ili aliwezi kua na faida kwetu.Nafikiri tunaweza kuamua kujenga kuliko kuendeleza kuboa ndugu. OMBI LANGU NI FAIDA KWA TAIFA LETU TANZANIA
Kumbuka kuwa kwa zaidi ya miaka 60 mmejaribu kuwabeba wanaojibeba kwanza ndo wanakuja kwenu.
Tafuteni na shikilieni maslahi ya Tanganyika kila mnapotaka kuijadili Tanzania!
Hata kwenye ndoa kuna namna mwanaume lazima usimamie maslahi yako kwanza!
 
29october25 ulipoteza hata ndugu mmoja?
Kupoteza ndugu,mali,rafiki,mtoto nk sio jambo zuri ata siku mmoja. Lakini pia atuwezi kuamini kua kwakua yalitokea hayo basi tuendelee kua na chuki,visasi,ugomvi nk Bila shaka utanielewa baadae. Amin aliua watanzania wengi pale Kagera lakini leo sisi na Uganda tuheshimiana na tunao urafiki wa kudumu. Tukianza kumtafuta nani mchawi nk ukweli nikua ata tunaomtafuta mchawi tutajikuta kua nasi ni umojawa wachawi hao.
 
Basi wekeni katiba nzuri siyo hii ya kujitafutia marefa peke yako kwanza uwalipe wewe mwenyewe na uwakochi jinsi gani wachezeshe! Hapo tutaelewana uzuri sio kutupoza wakati chanzo cha tatizo ni katiba
 
Utofauti wetu wa itikadi za kisiasa zisivuke mipaka na kusababisha maumivu makali yasiyo futika mioyoni mwetu.
Nimekusoma kwa uangalifu sana.
Matokeo ya uelewa wa andiko lako ni kwamba bado hujui matatizo yetu yanakoanzia; na kwa maana hiyo huwezi kupata ufumbuzi wake.

Inawezekana kabisa nia yako ni njema kabisa kama waTanzania wote wanaoguswa na hali yetu duni tuliyonayo kwenye taifa hili.
Kwa bahati mbaya sana bado unaogopa, unaficha ugonjwa unaotusumbua; na kwa maana hiyo usitegemee kuuponya ugonjwa wenyewe.

Matatizo yetu Tanzania hayaanzii na kuishia kwenye "utofauti wa itikadi za kisiasa".

Hizi itikadi za kisiasa hasa ni zipi zinazotuhatarishia utulivu wa taifa letu. Unazijuwa?
 
Naona wewe jamaa inawezekana hujui unachozungumzia kwenye mada yako hii, ambayo kwa kweli ingekuwa inaghusa sana kila mmoja wetu.

Lakini naona unafanya maonyesho tu!

Unatoa mfano wa Uganda na Idd Amin; hujui alikoishia huyo Idd Amin?
Idd Amin alikuwa mwakilishi wa waganda wote kwa uhasama na sisi?

Hutaki kughusia hawa waliotufanyia maovu hapa kwetu hiyo Oktoba; ni kama hujui kabisa kuwa wapo na wanaendelea kufanya maovu; na huku wewe unahimiza waTanzania wasahau maumivu na majonzi yaliyowapata?
Hii ni akili ya wapi hii?
 
Sasa nimekuelewa; kumbe ni mpiga ulaghai kama Samia mwenyewe!

Kwa kusoma yaliyochangiwa kwenye mada yako hadi hapa, sina shaka yoyote kwamba umepata mrejesho usiokuwa na konakona ndani yake toka kwa wachangaiji wa mada yako.

Kamlaumu Samia Suluhu Hassan, kwa haya yote yaliyotokea.
Ungekuwa umeguswa kweli na hali ulivyoieleza; usingeandika mada kwa mtindo huu ulioutumia hapa.

Huu ni udanganyifu/ulaghai.
 
Pole katika ili mkuu,tupunguze hisia na mihemko tunaweza kufika mbali
 
Hii ni hatari sana ndugu,unafikiri ndugu walio tangulia mbele za haki tukiendelea kuendeleza visasi au chuki tutakua tumetibu au tutaendelea kuchochea moto?
 
Post za kijinga kama hizi sana sana zinaamsha tu hasira na machungu kwa Watanganyika waliokufa na wanaoendelea kuuwawa kwa kutetea rasilimali za Nchi yao waliyokabidhiwa na MUNGU.

Mnawauwa watu, mnaiba, mnapora, mnauza, mali zao kwa fujo na makusudi, kiburi na madharau, halafu mnataka umoja, eti umoja wa madudu gani.

Mmeiharibu Nchi ya Nyerere kwa viwango visivyorekebishika kirahisi.
 
Ahsante kwa hoja yako ingawa sijaona kama unataka au unao utashi wa kujenga kuliko kubagaza. Hamna mtu alieko tayari au kushangilia uovu
 
Acha kuleta uandishi wa kukwepa ukweli, na kutaka kurahisisha mambo. Rais anakaa madarakani kwa kura 31m za uongo, kisha yanafanyika mauaji ya kutisha ili kulinda uchaguzi wa wizi, halafu unaleta habari za vyama vya siasa sijui porojo gani.
 
Ahsante kwa hoja yako ingawa sijaona kama unataka au unao utashi wa kujenga kuliko kubagaza. Hamna mtu alieko tayari au kushangilia uovu
Hushangilii uovu, kisha unataka kuleta uandishi wa kufunika uovu!
 
Hii ni hatari sana ndugu,unafikiri ndugu walio tangulia mbele za haki tukiendelea kuendeleza visasi au chuki tutakua tumetibu au tutaendelea kuchochea moto?
Naona huna tofauti yoyote na 'Tlaatlaah, ule mzoga unaovunda humu JF siku nzima ukijaza uchafu tu!
Pole katika ili mkuu,tupunguze hisia na mihemko tunaweza kufika mbali

Nyinyi watu sijui mnafikiri ujinga huu ndio utakuwa hali ya kawaida ya taifa hili?
 
Mliona raha kuua watoto wa watu Mo29 sasa hivi mnataka umoja na amani. Mliona raha kujiita nyie kizimkundule mkatukana na kufanya kila baya. Leo mnataka umoja na amani kirahisi rahisi tu.
Kila jambo litalipwa ×100 zaidi, mioyo inavuja damu roho zinauma, malipo ni hapahapa duniani
 
 
Mkuu unataka kusema kua sisi wa upande usio madarakani tukatae umoja?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…