Ommy Dimpoz azuiliwa kuingia Marekani!

Ommy Dimpoz azuiliwa kuingia Marekani!

OMMYD.jpg


Mwanamziki Ommy Dimpoz amerudishwa Tanzania baada ya kuzuiwa kuingia Marekani kwa kokosa vibali vinavyomruhusu kuingia nchi hiyo.

Chanzo: Clouds

Pia na aina ya begi nalo limechangia ni la kizaman mno.
 
Pole Dimpoz, ukisikia kuishi kwingi ni kuona mengi ndio huko lkn ni challenge katika maisha.
 
Hivi majuzi msanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongo Fleva) Ommy Dimpoz alisafiri kwenda Marekani kikazi. Wasanii ni vioo vya jamii yetu. Kwa hiyo wengi tulipata taarifa za safari hii kupitia baadhi ya vyombo vya habari.

Lakini pia siku mbili hizi kumekuwa na taarifa tata kuhusu safari hiyo na pia kuna picha zimeonekana Ommy Dimpoz akiwa Dar airport kwamba karejea bila kufanya maonyesha yake Marekani.

Kwa sababu moja tu kwamba kwa vile yeye ni kioo cha jamii na ni 'public figure' kwa sasa, wenye taarifa sahihi watiririke hapa!
 
Anadai alichelewa kwa ajili ya connection ya ndege hivyo alivyofika marekani alikuta shoo tayari imehairishwa hivyo maafisa uhamiaji wa marekani kwa kuwa wako makini walimzuilia Airport kwani kilichokuwa kinampeleka hakikuwepo tena,nilimsikia akijitetea hivyo radioni,sijui ukweli wake kama ni show au VISA ndio inahusika hapo?
 
Ni kuwa alitonywa kuwa madawa aluyoyabeba akifika USA kaisha so akageuza faster...natania tu...
 
Watanzania wana matatizo makubwa kuliko mnavyodhani.

Kuna rafiki yangu pumbavu fulani jinga kabisa lilikuja Bongo likiwa na passport ya Marekani basi kwa uzuzu na ulimbukeni kila hotel tukienda lenyewe linaona sifa kutoa US Passport matokeo yake kinakosa prevallige za wazawa linachajiwa kama mzungu mimi nachajiwa kizalendo.

Nina uhakika pale airport Marekani mahojiano yalikuwa hivi;

Immigration officer: Hellow mr Dempoz why u came to US?

Ommy dempoz: You know i have big show, big concert in America and my President Kikwete he select me to perform in Ameria for Ccm Celebrates.

So far i have big project with Wema you can follow me in Insta.

Immigration officer: Ok Mr Dimpoz wait there seat on the coach wait for the next flight back to your country.
Watoto wa mjini tunaita deal limebuma, no shame no offence

Kwataarifa yenu tu wote mnaopiga madongo hakuna mwanamuziki wa kibongo anakwenda kupiga show USA akakata visa ya kufanyia shows
Sababu ni kwamba promota na msanii watatakiwa kulipa kodi kubwa wakati show zenyewe za kimagumashi tu

Kilichotokea ni mabifu ya mapromota huku USa wamemchoma kwa kupeleka vipeperushi kwa uhamiaji kuwa Dimpoz anakuja kwa show na sio matembezi

Narudia tena hakuna msanii yeyote anayekwenda marekani kwa visa ya kufanya show..... HAKUNA
Labda vikundi vya sanaa vinavyokwenda kwenye matamasha kwa mialiko maalum na si hizi show za "sebuleni"
 
Namsachi msanii wangu yule wa msaada wa Tigo na Fiesta habari zake sizioni au hana jipya au wanambania???????????
 
Au ni tudawa twa Ze Domo, yeye aende Marekani naye aende, yeye ampende Beatif onyinyi naye ampende, yahuuuu
 
Miongoni mwa stori zilizochukua headline kwenye radio mbalimbali, hata kwenye magazeti ni kuhusiana na msanii wa Ommy Dimpoz kuzuiliwa kuingia Marekani na kurudishwa Tanzania bila kufanya show zake.

Sasa basi Kupitia Amplifaya ya Clouds FM Ommy Dimpoz ame amplify na kusema;”…Mimi hata mwenye hizo habari zimenishangaza na kilichonishangaza zaidi stori jinsi zilivyokuja na zilizovumishwa sijui zimekuja vipi kimenishangaza zaidi au unakuta hata mtu ni professional, watangazaji, Waandishi,wengine mtu aandika tu stori au anaongelea stori kwa maana unatengeneza stori kwa kusikia kitu ambacho hauna ushahidi wala haujamsikia mhusika pengine hata kuongea na management yangu, au lakini hata kuongelea ile kuhusu mhusika maana meneja wangu aliniambia ameulizwa imekuaje akawajibu kwamba Ommy ame ni text anarudi leo kwa hiyo yeye atakuwa na majibu yote lakini unakuta stori tu zinaongelewa ambapo hata mimi mwenyewe sijasikilizwa kitu gani kimetokea..”





Millardayo….. Ilikuwaje?

Ommy Dimpoz:…”kilichotokea ni kwamba mimi nilitoka hapa nikaenda mpaka Amsterdam na Amsterdam nilikuwa na connect flight kutoka Amsterdam kwenda detroit na detroit kwenda Vegas kwahiyo kufika Amsterdam nilimiss flight ya connect Amsterdam kwenda detroit kwa hiyo ikabidi ni rebook booking yangu ili nipate flight nyingine ya kwenda Las Vegas kwa hiyo nikakosa connection ya kwenda detroit nikapata connection nyingine ya kupitia Minnesota nilivyofika kule wakati nimefika airport ndege ambayo nilipata connection na hii ya pili ikawa tayari ilikuwa imenichelewesha kwasababu ilikuwa inatakiwa inifikishe siku ya show sasa pale kukawa na tatizo kule watu wa venue siku ambayo waliokuwa wameongea nao



kwa hiyo ikabidi waongee kuwa msanii amechelewa lakini tunaomba event tufanye siku nyingine lakini wale jamaa wakakataa wakasema haiwezekani na lengo ilikuwa mimi ni perform kwenye hiyo weekend ya ruby kwa hiyo kutokana na mazingira hayo ikabidi wale watu wa immigration unajua siku zote ukifika ile ni nchi unavyoingia siku zote lazima kuna maswali ya security pale lazima uulizwe, unajua watu hawajui kitu kimoja kwamba kupata visa sio ndio kuingia kwenye nchi ya mtu kwamba ukifika nchi yoyote hata sisi tunaenda South Africa naona ni nchi ambayo tunaingia bila visa ukifika airport lazima uulizwe unakuja kufanya nini, unakaa siku ngapi, kwa hiyo nchi zote utaratibu ndio huo kwa hiyo katika pale kuulizwa nikawambia naenda Las Vegas kwenye show, kwa hiyo mara nyingi unajua wa marekani ni watu wakutaka kujiridhisha au hata hapa Tanzania wageni wanakuja unaweza ukamuona Mzungu, Mhindi, Mwarabu, mtu mweusi akifika pale kwenye passport control lazima wahusika wa hapo airport wajiridhishe pengine hata wapige simu kwa huyo mwenyeji wako, kwahiyo wakapiga simu kule kwa watu wa event pamoja na sehemu ya Venue kwa hiyo watu wa Venue wakaambiwa kulitakiwa kuwe na show ila msanii hakufika kwa hiyo wakabidi waongee na promote akasema tumeisongeza kwasababu msanii amechelewa amemiss flight sasa wakarudi kwangu wakaniambia lengo lilikuwa uje kwenye hii show na show tayari umeshaimiss kwasababu ya matatizo ambayo sisi hatutakiwa kuyajua yamesababishwa na nini wakasema kwamba lakini hapa inaonesha una show nyingine New york tarehe 21 nikawaambia ndio nilikuwa ninayo ila nilipanga nikitoka Las Vegas naelekea huko.



Wakaniambia sasa hii show ndio tunatatizo nayo kwasababu ni show ambayo inahusisha chama cha kisiasa na kama uliona hata kwenye promotion yangu nilikuwa nimeandika kuwa nitakuwa na show ya miaka 38 ya CCM Marekani, unajua vyama cha siasa hivi Chadema, CCM wanamatawi yao kule Marekani watu wanaoishi nje mara nyingi uwa wanafanya sherehe sherehe za Annivesary , kwa hiyo wakaniambia kuwa hii visa yako haikuruhusu wewe kuperform kuna aina ya Visa ya inayoruhusu msanii ku perform kwasababu show yako ni kama ya kisiasa, kwa hiyo kwa kuangalia hivyo wakaniambia option iliyopo itabidi nirudi nyumbani kwasababu shughuli iliyokuleta imeshindikana kwa hiyo unaweza ukaja mwenyewe baadae kwa matembezi yako au kwa nini lakini hata ikitokea mfano leo nikakatiwa ticket au nikate ticket nirudi Marekani visa yangu sasa hivi hainiruhusu kwa hiyo ina maana ninataka kuchukue visa nyingine yenye kibali maalumu chenye kuperform mimi kwenye show, na kama ukivunja sheria zao wanaweza wakakufungia miaka mitano halafu wanakupiga faini dola elfu 1o kwa hiyo mimi mwenyewe nikakubali lazima pia uangalie mazingira na mimi lazima nitengeneze mazingira yangu ya kazi kwa hiyo nikawaambia sawa nitarudi nyumbani kwa hiyo nasubiri tu sasa hivi wale promote wa show ya Las Vegas wapange kwaajili ya venue ya show nyingine then nitaendelea na mchakato mwingine kama kawaida.

.

Millardayo…: ‘ilikuwaje mpaka unamiss Flight?Ommy Dimpoz: unajua kumiss flight kunatoka hata hapa Dar unaweza ukamiss flight, unajua nilishazoea kukaa kwenye zile connection za masaa matatu reporting time kwahiyo nilijichanganya kwenye masaa halafu ukishaondoka hivi inakuwa kidogo hivi masaa yanazigua kwa hiyo inabidi uwe makini kidogo kwa hiyo katika kuangalia pale yaani mimi fikra zangu na mawazo na nilishazoea zile flight za kuunganisha labda za kwenda DC unaweza ukakaa pale masaa matatu au masaa matatu na nusu kufanya connection ya kwenda lakini ile ilikuwa na connection ya muda mfupi kama lisaa limoja kwa hiyo mpaka ushuke, utoke sijui geti unalotakiwa kwenda kwahiyo katika mishe mishe nikakuta ile flight mlango umeshafungwa kila kitu wakasema haiwezekani na hata begi langu walikuwa wamelishusha kitu kingine nimeshazoea kama mule uwanja unataka watu wanatangaza kwasababu ilishawahi kunitokea mara nyingine labda unakuta abiria amechelewa flight kwasababu sisikii tangazo lolote nimekaa angani kama almost masaa tisa nafikiri nane kutoka Dar kwa hiyo nilipofika nikaunganisha wifi nikawa nimepata internet nikaingia ghafla kwenye whtsspp nasoma SMS nawaambia washikaji wa kule marekani kuwa nakuja nimeshafika Amsterdam kitendo cha pale kuchati kuwa wish watu valentine nakutana flight imeshaondoka.

Millardayo…: ‘Baada ya wao sasa kukuambia unarudi Tanzania yaani uligeuzia pale pale Airport au mazingira yalikuwaje?..

Ommy Dimpoz…;“Waliniweka Hotel kwasababu hiyo flight ilikuwa ni ya siku inayofata ambayo ni jioni mpaka zile ndege zinavyotoka huku zifike Amsterdam, zifike pale kwa hiyo ilikua ni siku inayofata…”

...........................................
COPY & PASTE FROM: Millardayo.Com

 
Ommy kuna mambo amedanganya ukifatilia,kikubwa visa yake sio ya show ni ya matembezi,sababu ingekuwa ya show angebaki kusubiri show ya ccm New York
 


Wednesday, February 18, 2015

Wakaniambia sasa hii show ndio tunatatizo nayo kwasababu ni show ambayo inahusisha chama cha kisiasa


wwwwwwwwwwwwwww.jpg


Wakaniambia sasa hii show ndio tunatatizo nayo kwasababu ni show ambayo inahusisha chama cha kisiasa na kama uliona hata kwenye promotion yangu nilikuwa nimeandika kuwa nitakuwa na show ya miaka 38 ya CCM Marekani, unajua vyama cha siasa hivi Chadema, CCM wanamatawi yao kule Marekani watu wanaoishi nje mara nyingi uwa wanafanya sherehe sherehe za Annivesary , kwa hiyo wakaniambia kuwa hii visa yako haikuruhusu wewe kuperform kuna aina ya Visa ya inayoruhusu msanii ku perform kwasababu show yako ni kama ya kisiasa, kwa hiyo kwa kuangalia hivyo wakaniambia option iliyopo itabidi nirudi nyumbani kwasababu shughuli iliyokuleta imeshindikana kwa hiyo unaweza ukaja mwenyewe baadae kwa matembezi yako au kwa nini lakini hata ikitokea mfano leo nikakatiwa ticket au nikate ticket nirudi Marekani visa yangu sasa hivi hainiruhusu kwa hiyo ina maana ninataka kuchukue visa nyingine yenye kibali maalumu chenye kuperform mimi kwenye show, na kama ukivunja sheria zao wanaweza wakakufungia miaka mitano halafu wanakupiga faini dola elfu 1o kwa hiyo mimi mwenyewe nikakubali lazima pia uangalie mazingira na mimi lazima nitengeneze mazingira yangu ya kazi kwa hiyo nikawaambia sawa nitarudi nyumbani kwa hiyo nasubiri tu sasa hivi wale promote wa show ya Las Vegas wapange kwaajili ya venue ya show nyingine then nitaendelea na mchakato mwingine kama kawaida.

Ommy Dimpoz: unajua kumiss flight kunatoka hata hapa Dar unaweza ukamiss flight, unajua nilishazoea kukaa kwenye zile connection za masaa matatu reporting time kwahiyo nilijichanganya kwenye masaa halafu ukishaondoka hivi inakuwa kidogo hivi masaa yanazigua kwa hiyo inabidi uwe makini kidogo kwa hiyo katika kuangalia pale yaani mimi fikra zangu na mawazo na nilishazoea zile flight za kuunganisha labda za kwenda DC unaweza ukakaa pale masaa matatu au masaa matatu na nusu kufanya connection ya kwenda lakini ile ilikuwa na connection ya muda mfupi kama lisaa limoja kwa hiyo mpaka ushuke, utoke sijui geti unalotakiwa kwenda kwahiyo katika mishe mishe nikakuta ile flight mlango umeshafungwa kila kitu wakasema haiwezekani na hata begi langu walikuwa wamelishusha kitu kingine nimeshazoea kama mule uwanja unataka watu wanatangaza kwasababu ilishawahi kunitokea mara nyingine labda unakuta abiria amechelewa flight kwasababu sisikii tangazo lolote nimekaa angani kama almost masaa tisa nafikiri nane kutoka Dar kwa hiyo nilipofika nikaunganisha wifi nikawa nimepata internet nikaingia ghafla kwenye whtsspp nasoma SMS nawaambia washikaji wa kule marekani kuwa nakuja nimeshafika Amsterdam kitendo cha pale kuchati kuwa wish watu valentine nakutana flight imeshaondoka.

‘Baada ya wao sasa kukuambia unarudi Tanzania yaani uligeuzia pale pale Airport au mazingira yalikuwaje?..

Ommy Dimpoz…;“Waliniweka Hotel kwasababu hiyo flight ilikuwa ni ya next day ambayo ni jioni mpaka zile ndege zinavyotoka huku ifike Amsterdam, ifike pale kwa hiyo ilikua ni next
day…”

CREDIT:MILLARDAYO.COM WA CLOUDS FM











 
kilichotokea ni kwamba dimpos alikuwa na visa ya kutembelea marekani
hii visa haimaanishi kibali cha kufanya kazi hata ya muda mfupi kama show marekani

Alipokamatwa alidai ameenda kwa ajili ya matembezi tu AMERICA
maafisa uhamiaji wakamwonesha mabango\VIPEPERUSHI yaliyokuwa yakitangaza show yake, dimpos akabaki kuduwaa

UKWELI NI KWAMBA UKAWA MAREKANI WALIWAPATIA MAAFISA UHAMIAJI YIVYO VIPEPERUSHI ili wamzuie DIMPOS kuingia AMERCA.

Dimpos hakuchelewa ndege wala nini, awe mkweli aseme wazi kuwa alioneshwa vipeperushi vya show yake na maafisa uhamiaji
 
Back
Top Bottom