Ommy Dimpoz naunga mkono msimamo wako, ila tupo wazazi tunaohukumiwa tofauti na makosa yetu

katawa

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2010
Posts
1,103
Reaction score
2,575
Nimesoma na kusikiliza maoni mbalimbali kuhusu nachoweza kuita kutowajibika kwa malezi kwa baba yake Ommy kwa mwanae.

Hapa nitaeleza mkasa unaonihusu mimi wa kutowajibika kulea mtoto wangu.

Mwaka 2001 binti niliyekuwa na mahusiano naye aliniambia kuwa ana mimba, sikuikataa.

Jirani a nilipokuwa naishi kulikuwa na muuguzi rafiki yangu, nikamuomba ampime kuthibitisha ikiwa ni kweli ana mimba. Jibu la muuguzi lilikuwa tata kwangu, akaniambia ni kama ana mimba lkn inatakiwa turudie kupima tena.

Mimi nikahukumu kuwa hana mimba.
Maisha yakaendelea nikahama huo mkoa na kuhamia mkoa mwingine.Mwaka 2019 namba ngeni ikapigwa kwangu baada ya kuipokea akajitambulisha kwangu na kwa uhakika nikamkumbuka.

Akaniambia mtoto wako kakua na kamaliza kidato cha nne.Nilipigwa na butwaa kisha nikapuuzia. Nikajiuliza kama kweli ana mtoto wangu imekuwaje kwa miaka yote hii hakuniambia?

Nikahisi Kuna namna ya kutengenezewa mazingira ya kupigwa.

Siku nyingine akanipigia kusisitiza kuwa Kuna mtoto, mara ya pili nikahisi huenda Kuna ukweli nikamuambia mke wangu kuhusu hili.

Nikampa namba wife wakaendelea kuwasiliana na wife akanieleza kweli yule mwanamke ana mtoto wako.

Ikafanywa mipango mtoto nimuone, akaja na mamake mkoa nilipo lkn mtoto akakataa kuonana na mimi, akakutana na rafiki yangu, rafiki akasema kweli mtoto ni wa kwangu kwa muonekano.

Nikaamua tukutane rasmi, toka 2019 mpaka leo sijafanikiwa kumuona pamoja na kuwekeza nguvu kubwa kumtafutia.

Baadaye nikaona isiwe shida nikaachana naye na kamwe sitakuja kuja kumfuatilia.

Binafsi nahesabu kuwa mimi ni 'sperm donor 'kwa yule mtoto. Sijichukulii kama ni baba mzazi.

Moyo wangu unahisi hatia kidogo sana na kamwe sitakuja kuomba msaada kwake kama baba yake.

Baba Dimpoz komaa na maisha yako, muache dimpoz aishi maisha yake.
 
Itungwe sheria kama Ulaya ukimpa mwanamke mimba ni lzm uwajibike juu ya matunzo ya mimba hio na mtoto atakaezaliwa hadi atakapojitegemea. Hii itaepusha wahuni kutunga hovyo mimba na kutelekeza watoto waishie kupata tabu duniani.
 
Hukupaswa kusimulia hiki kisa kisicho na manufaa yoyote.
Mwanaume muwajibikaji usingekaa kimya miaka yote hiyo wakati hata nesi alikwambia uwezekano wa mimba.
Rafiki yako naye amekuhakikishia pia.

Ulipaswa ufunge safari au ufanye namna umuone isingeshindikana.
 
Yaani mtu ambaye upo kwenye mahusiano naye ya kimapenzi anakuambia Ana mimba yako, haumuamini unashirikisha rafiki yako mtaalam wa afya anakuambia ni Kama vile ana mimba ila "mrudie vipimo" Ila wewe unapuuzia na kuhama mkoa kabisa, halafu hapo Tena analaumiwa mwanamke kweli?? Kwa hiyo ulitaka aje Tena kwako akubembeleze kwamba ni kweli Nina mimba yako,twende tukapime tena au ulitaka afanyeje Sasa?? The fact tu kwamba Kuna mtu amekuambia Ana ujauzito wako na haukufuatilia na ukahama mkoa kabisa maana yake haukua tayari kubeba majukumu ya ubaba, na huyo mama kakutafuta tu kwa pressure ya mtoto nadhani maana Kama miaka yote aliweza kumlea bila wewe kuhusika angeweza kumlea usimjue kabisa ,itakua maswali na huzuni ya mtoto ilimsukuma kukutafuta.Anyways endelea kuamini hauna makosa.
 
umesoma maelezo yake ukayaelewa au unakurupuka?
 
umesoma maelezo yake ukayaelewa au unakurupuka?
Mstari kwa mstari...unaamini kuwa mtoto aweza kugoma kuonana na babake lakini akakubali aonane na rafiki yake?
Tumia akili kifogo hapa tunapigwa za macho
 
ila kama inafikirisha kidogo hv,mkuu umesema walifunga safari kuja huo mkoa uliopo sasa ikawaje baada ya kufika huko mtoto akatae kuonana na wewe na akubali kuonana na rafiki yako?au wakati analetwa alikuwa hajui anaenda wapi na kufanya nini?(umesema mtoto amemaliza kidato cha nne kwamaana ni mkubwa)au mimi ndo sijaelewa vizuri labda
 
Sababu ya kukataa kuonana na mimi sijawahi kuijua. Na sio mara moja wamekuja mara tatu na zote kakataa kuonana na mimi.Mara ya mwisho alikuja na mama yake mkubwa,kwa maelezo ya mamake mkubwa nikiwa huwa wanakubaliana kuwa tutaonana lkn mwishowe ugeuka.Kukubali kuonana na rafiki yangu ni kuwa tayari alikuwa na mawasiliano ya karibu na mama yake.Walipoonana na rafiki hakupenda kuongea kila akiulizwa hakuwa anajibu.
Kuna mambo mengi sana hapa sijaandika ila kwa kifupi ni kuwa mtoto kalishwa sumu ambayo hawezi kuitapika.
 
Itungwe sheria kama Ulaya ukimpa mwanamke mimba ni lzm uwajibike juu ya matunzo ya mimba hio na mtoto atakaezaliwa hadi atakapojitegemea. Hii itaepusha wahuni kutunga hovyo mimba na kutelekeza watoto waishie kupata tabu duniani.
Huwa mnasoma wapi huu ujinga?
 
duh hyo changamoto mkuu pole sana,sasa kwa nn hamkwenda tena kufanya tena vipimo kama mlivyoshauriwa na mtaalamu na ukaamua kudhani hana mimba?nadhani mama wa huyo mtoto atakuwa na maumivu fulani kwa kumuacha amletee mtoto peke yake(kwa tafsiri yake ni kama uliwatelekeza)
 
Kutorudia vipimo ni kosa langu, nakiri. Kipindi kile bado kijana sana, mimi nilipoapata taarifa kuwa turudie basi nami nikampima kwa macho'ujinga' na nikahukumu kuwa hana mimba.
 
Kutorudia vipimo ni kosa langu, nakiri. Kipindi kile bado kijana sana, mimi nilipoapata taarifa kuwa turudie basi nami nikampima kwa macho'ujinga' na nikahukumu kuwa hana mimba.
unamuhitaji mwanao kwa sasa?
 
nadhani bado una nafasi ya kuwa nae,jitahid hata kumpigia na umuelezee kilichotokea HAKIKISHA ANAKUELEWA ila kumbuka kukuelewa ni jambo lingine na kukusamehe ni jambo lingine
Nimefanya jitihada kubwa kwenye hilo nimeshindwa. Nilichojifunza ni kuwa watoto wa aina hii huwa wanapenda baba zao tufeli maisha kisha wao wakiwa na maisha mazuri tuwafuate kuomba msaada, hapo wanapata nafasi ya kulipa kisasi.
Nawashauri wanaume waliotelekeza watoto kwa kujua ama kutokujua, ikitokea mtoto anakuwa mtata kama huyu wangu ni kuachana naye hata kama unamuitaji sana. Ukitumia nguvu kubwa kumpata atakugeuza kuwa mtumwa wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…