Ommy Dimpoz: Ugonjwa wangu ulisababishwa kunywa kitu chenye sumu, inabidi niende kutibiwa nje

Mbona hilo linafahamika? Yeye yuko SA, kwa matibabu kwahivyo licha ya hayo matibabu, yeye ndo anayeumwa na anaona bado anahitaji matibabu zaidi ya kwenda nje ya Afrika kutibiwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ok, sasa nimeelewa.

Ila basi walau ungeandika kwenda kutibiwa zaidi Ulaya, maana hapo juu maelezo hayakujitosheleza.
 
Ok, sasa nimeelewa.

Ila basi walau ungeandika kwenda kutibiwa zaidi Ulaya, maana hapo juu maelezo hayakujitosheleza.
Unataka kulazimisha vitu ambavyo hakuvisema, utaandikaje anaenda Ulaya? Je akienda Amerika Kusini? Kwani kila nje ya Tanzania au Afrika ni Ulaya mkuu.?

Mwenyewe hajabainisha nchi ambayo ataenda. Amesema nje! Kwa kuwa yuko Afrika Kusini, na hospitali za Tanzania na Kenya tayari, amemaanisha nje ya bara la Afrika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nasikia jamaa ni mnyonyaji mashuhuri sana pale wilayani #Hombolo
 
Write your reply...mungu akusaidie brother upone,wewe bado kijana na una nguvu za kuifanya Tanzania iinuke kwa shughuri zako,god bless you my blood
 
Ok, sasa nimeelewa.

Ila basi walau ungeandika kwenda kutibiwa zaidi Ulaya, maana hapo juu maelezo hayakujitosheleza.
Jamaa kakosea tu kuandika ila hataki kukubali ukweli.

Nimeangalia hayo mahojiano, alivyougua alianza kutibiwa Tanzania.

Wakati yupo Kenya Ma daktari wakamshauri aende India, South Africa au nchi nyingine iliyo advanced kwenye tiba.

Akaamua aende Afrika Kusini sababu ni karibu na hakuna mambo ya Visa.

Katika interview yake hajazungumzia suala la kwenda kutibiwa popote zaidi ya hapo halipo.

Mtoa mada kajiachanganya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio tatizo letu Wabongo.

Hata mimi nimemuitika tu lakini mpaka sasa hicho alichoandika sijaona kwingine popote.
 
Mbona hilo linafahamika? Yeye yuko SA, kwa matibabu kwahivyo licha ya hayo matibabu, yeye ndo anayeumwa na anaona bado anahitaji matibabu zaidi ya kwenda nje ya Afrika kutibiwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Haya wewe umeayatoa wapi na hakuna popote amesikika mwenyewe akisema hivyo?
 
Haya wewe umeayatoa wapi na hakuna popote amesikika mwenyewe akisema hivyo?
Nimekuwekea chanzo kuwa Millard Ayo hapo, na kipindi cha Amplifaya au nyie mnasomaje?

Na nakuongezea zaidi fungua page ya Instagram ya Clouds FM. Ili ujionee na ufungue hiyo akili iliyofungwa.

Wewe unapelekwa puta na huyo member.! Nimempotezea baada ya kuona nimeshatolewa ufafanuzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…