Mjomba wangu alikuwa anapenda kusema " Nice observation"King Tiger ilikuwa na emergency power on. Kuna kitu kama button mbele walikuwa wanawasha crew ikitokea ambush au wakiwa sehemu yenye adui ambapo wakitoka nje wanakuwa exposed. Ila hiyo ilikuwa ni rare kuitumia, ya uhakika ni hii ya kutoka nje hapo ambapo ni gunner na driver ndio wanatoka kama ilikuwa tank platoon isiyo na troops. Kama ni troops wako nje wanajua basi ndio wanawasha.
Kwenye baridi ya Siberia kifaru hiki Tiger kilipata shida. Kizito mno kupita kwenye tope, kiliundwa very complicated kama Wajerumani wanavyopenda, spare parts ngumu kutengeneza kirahisi, kigumu kufanyiwa services, kigumu kuwa mass produced, gharama kubwa kutengenezwa.
Kwenye vita vifaru kama T-34 cha Urusi na M4 Sherman cha Marekani ndio vilifanya vizuri.
Stalin hapo ndio aliposema "Quantity has a quality of its own"
Tiger kilikuwa bora kwenye range, shabaha, armour ila mapungufu yake niliyoandika mwanzoni yalikifanya kiwe na mchango mdogo mwishoni mwa vita.
Gustav.Hivi uliwahi kufuatilia lile dubwana walilojaribu kulitengeneza wajerumani kama prototype lilikuwa likifaru moja kubwa la ajabu zito mno sikumbuki walilipa jina gani
Miaka ya 90s tz zlikuwepoIyo inaitwa handel ata gari za zamani zilikua zikiwashwa ivo
Kama nimekosea nirekebisheni wakubwa
Ni sawa,kulikuwa ma landlover 109 za kuzungusha hivyoIyo inaitwa handel ata gari za zamani zilikua zikiwashwa ivo
Kama nimekosea nirekebisheni wakubwa
Yup Germany war machine,yote hiyo ilimpa kichwa bwana mkubwa Hitler ya kutaka kujitwalia nchi kadhaa kuwa makoloni yake,ila walikuwa vizuri sana kivita wajerumani unaikumbuka blitzkrieg ilivyokuwa inazitwaa nchi kadhaa kama mwewe anyakuavyo vifaranga,blitzkrieg ilifaulu kwa urahisi kwenye nchi kadhaa japo naona Britain haikufanikiwa kutwaliwa pamoja na zile heavy bombing za ujerumani kwa kutumia air raidGustav.
Wajerumani walikuwa obsessed na teknolojia kubwa kwenye vita. Sababu walijiona ni superior race, hivyo lazima wapigane kwa silaha za kustaajabisha zenye akili kubwa kwenye kuunda. Walikuwa na silaha za kimkakati za Wunderwaffe (wonder weapon) mwishoni mwa vita ili ziwasaidie kupindua.
Matatizo ya King Tiger MBT na silaha nyingine za Ujerumani ni yale yale. Gustav ni cannon ilikuwa na zaidi ya tani 1,000 na ilikuwa inahitaji operators zaidi ya 1,000. Ilikuwa inalazimisha mafundi wa reli waje kufunga na kufungua ndio isogee. Ilikuwa na usumbufu mtupu na matumizi machache sana, kwa gharama kubwa na matokeo madogo mno.
Ilitumika kwenye siege miji ya Ukraine, wakati Wasovieti upande wao waliunda Katyusha multiple rocket launchers. Wajerumani waliziita "Stalin's organs" na zilikuwa effective. Sifa zile zile kama nilizotaja awali kwa Soviet T-34 tank.