Onana vs Skudu, ni mchezaji gani atakuwa wa kwanza kupewa mkono wa kwaheri katika timu yake?

Skudu ni mzuri wa chenga, mbio na entertainment football. Ila tu mechi ya juzi imetoa mshtuko kidogo. Kwamba kati ya umri na pancha (gari ya mkaa, trip shamba trip gereji) inawezekana kimojawapo au vyote vikamuathiri.
Naona unefanya copy and paste bila hata acknowledgement
 
Habari wanaJf

Katika kufuatilia aina ya uchezaji wa hawa wachezaji wawili Onana wa Simba na Skudu wa Yanga kwa mechi mbili walizocheza kwa maana zile za utambulisho wa wachezaji na ngao ya jamii kule Tanga kuna vitu nimeviona vya utofauti kutoka kwa wachezaji hawa.

Mahalatse Makudubela "Skudu" amekuwa ni mchezaji ambaye amekuwa akifanya mambo mengi uwanjani yasiyo na tija kwa timu yake ikiwa pamoja na kupenda kukaa sana na mpira lakini mwishowe kupoteza lengo la huo mpira kwa kutozalisha faida yeyote. Amekuwa ni mchezaji wa kutaka sana kushangiliwa kwa kufanya vitu ambavyo mpira wa kisasa unavikataa 'ball dancer' japo amekuwa akiimbwa sana na mashabiki wa Yanga ila kwa mechi hizo mbili ikiwa hajafanya kitu chochote kilicholipa jitihada za mashabiki kumshangilia.

Willy Essomba Onana nae ameimbwa na mashabiki wake lakini amevimba kichwa kwa kutaka kuivaa Simba kuliko kutoa alichonacho jambo ambalo hupelekea kucheza kistaa na kupelekea kupoteza mpira kirahisi mno. Lakini faida ya huyu jamaa ni aina ya mpira wake ambao ni direct and objective footbal[emoji460] ambao ni aina ya soka la kisasa linalopendwa na makocha wengi wa kisasa duniani japo kuna wakati amekuwa akifanya mambo yanayoigharimu timu. Ameipa Simba mwanga na faida ya kile alichonacho.

Kwa soka la bongo ambalo leo shujaa kesho hufai kwa aina ya uchezaji wao na matumaini makubwa waliyonayo mashabiki wao wanayotegemea kutoka kwao je ni kweli wataendelea kupewa imani hiyo au watasalitiwa mapema tu?

Kwa wataalam wa masuala ya soka na wenye jicho la uchambuzi ni mchezaji yupi atakuwa wa kwanza kupewa "Thank you" na timu yake kwa hawa wachezaji wawili?
Nakumbuka Skudu alikaribia kufunga Mechi na Kaizer na Kross kama 6 hivi.
Onana alifunga Mechi yake ya Kwanza tu na akawa threat kwenye Mechi hiyo.
Mnataka wafanye nini zaidi labda?
Skudu kakamiwa na Wachezaji wa Azam na kuumizwa dakika chache baada ya mechi kuanza. Nani haumii akichezewa rafu? Inonga kaumia sababu ya upuuzi wa Kagere, naye ni gari la Mkaa?
Onana kacheza Mechi ya Singida kama winger na kisha second striker na akasumbua Sana japo hakufunga. Mnataka kumuona Kila siku anafunga ndo mseme ni mzuri?
Muda utaongea wala si lazima wapewe hizo senki yuu unazowaombea.
 
skudu ataondoka na kitakachomwondosha ni umri, majeruhi ya mara Kwa mara yatamfanya apoteze namba.
Simba iliwahi kupata Beki mzuri Method Mwanjali ila umri na majeruhi vilimwondoa mapema.
 
Ila mambo mengine bwana haya tufanye ni wewe ungechezewa rafu mbaya halafu ukaumia unaweza jivimbisha uendelee kucheza hali ya kuwa umeumia ili uonekane kwa mashabiki???acheni uzwazwa hata wachezaji ni binadamu pia!
 
Nakumbuka Skudu alikaribia kufunga Mechi na Kaizer na Kross kama 6 hivi.
Onana alifunga Mechi yake ya Kwanza tu na akawa threat kwenye Mechi hiyo.
Mnataka wafanye nini zaidi labda?
Skudu kakamiwa na Wachezaji wa Azam na kuumizwa dakika chache baada ya mechi kuanza. Nani haumii akichezewa rafu? Inonga kaumia sababu ya upuuzi wa Kagere, naye ni gari la Mkaa?
Onana kacheza Mechi ya Singida kama winger na kisha second striker na akasumbua Sana japo hakufunga. Mnataka kumuona Kila siku anafunga ndo mseme ni mzuri?
Muda utaongea wala si lazima wapewe hizo senki yuu unazowaombea.
Nadhani hata muunganiko wa hizi timu zenyewe bado kidogo labda baada ya kucheza mechi 5 hivi
 
Mahalatse Makudubela "Skudu" amekuwa ni mchezaji ambaye amekuwa akifanya mambo mengi uwanjani yasiyo na tija kwa timu yake ikiwa pamoja na kupenda kukaa sana na mpira lakini mwishowe kupoteza lengo la huo mpira kwa kutozalisha faida yeyote

Hapo sikubaliani nawewe kwani skudu kacheza kias hcho had Kusema anakaa na mpira mda mwngi. Wachambuzi vp mbn mnazingua.
 
Unataka tathmini ya nini na wakati ligi bado haijaanza! Wewe ndiyo unaueleta porojo. Maana huwezi kufanya evaluation kwa mchezaji aliyecheza mechi moja tu ya Ngao ya Jamii.
Hahahaaa ni aibu sana mchezaji anafanyiwa evaluation hata kwa mechi mechi moja kwa kuangalia instincts anazotakiwa kuwa nazo mchezaji ambazo ndizo zinatoa mwelekeo wa nini kipo miguuni mwake na kipi ata deliver kwa timu zao
 
Ila mambo mengine bwana haya tufanye ni wewe ungechezewa rafu mbaya halafu ukaumia unaweza jivimbisha uendelee kucheza hali ya kuwa umeumia ili uonekane kwa mashabiki???acheni uzwazwa hata wachezaji ni binadamu pia!
Ile ni rafu mbaya au umri tu ?
 
Umeingia kwenye propaganda za wachambuzi wetu. Skudu Mechi dhidi ya Azam amecheza dk 7 akaumia na mechi ya kaizer hakumaliza dk.90 ila alicheza vizuri.

mnataka kutuaminisha kuwa Skudu hana chochote zaidi ya kuchezea mpira kitu ambacho si kweli. Mechi ya Kaizer alikuwa na shots on target na alipiga crosses nzuri sasa sijui huo ubaya wake uliuona kwenye mechi gani?
Wanajifariji tu hao baada ya kucheza pira makande badala ya pira biliani. Simba msimu huu ni mbaya kwao kuliko uliopita.
 
Ila mambo mengine bwana haya tufanye ni wewe ungechezewa rafu mbaya halafu ukaumia unaweza jivimbisha uendelee kucheza hali ya kuwa umeumia ili uonekane kwa mashabiki???acheni uzwazwa hata wachezaji ni binadamu pia!
Umestiki kwenye ishu mdogo sana hata mchezeji mzuri anaumia so hatuangalii yeye kuumia ila ni namna anavyocheza ndivyo inakutambulisha ni mchezaji wa kalia ipi so hebu tu deal na hicho kitu
 
Wanajifariji tu hao baada ya kucheza pira makande badala ya pira biliani. Simba msimu huu ni mbaya kwao kuliko uliopita.
Kwa kigezo kipi cha ubovu maana hata msimu uliopita haya maneno yalizungumzwa kwamba ilikuwa bora kuliko ile ya msimu uliyopita.

Lakini sikushangai kwakuwa ndiyo maneno ya watanzania yaani kinachopita ndicho bora kuliko kilichokuwepo trace kwa viongozi wetu wa nchi
 
Hv ww huoni kwamba hamna timu?
 
Habari wanaJf

Katika kufuatilia aina ya uchezaji wa hawa wachezaji wawili Onana wa Simba na Skudu wa Yanga kwa mechi mbili walizocheza kwa maana zile za utambulisho wa wachezaji na ngao ya jamii kule Tanga kuna vitu nimeviona vya utofauti kutoka kwa wachezaji hawa.

Mahalatse Makudubela "Skudu" amekuwa ni mchezaji ambaye amekuwa akifanya mambo mengi uwanjani yasiyo na tija kwa timu yake ikiwa pamoja na kupenda kukaa sana na mpira lakini mwishowe kupoteza lengo la huo mpira kwa kutozalisha faida yeyote. Amekuwa ni mchezaji wa kutaka sana kushangiliwa kwa kufanya vitu ambavyo mpira wa kisasa unavikataa 'ball dancer' japo amekuwa akiimbwa sana na mashabiki wa Yanga ila kwa mechi hizo mbili ikiwa hajafanya kitu chochote kilicholipa jitihada za mashabiki kumshangilia.

Willy Essomba Onana nae ameimbwa na mashabiki wake lakini amevimba kichwa kwa kutaka kuivaa Simba kuliko kutoa alichonacho jambo ambalo hupelekea kucheza kistaa na kupelekea kupoteza mpira kirahisi mno. Lakini faida ya huyu jamaa ni aina ya mpira wake ambao ni direct and objective footbal[emoji460] ambao ni aina ya soka la kisasa linalopendwa na makocha wengi wa kisasa duniani japo kuna wakati amekuwa akifanya mambo yanayoigharimu timu. Ameipa Simba mwanga na faida ya kile alichonacho.

Kwa soka la bongo ambalo leo shujaa kesho hufai kwa aina ya uchezaji wao na matumaini makubwa waliyonayo mashabiki wao wanayotegemea kutoka kwao je ni kweli wataendelea kupewa imani hiyo au watasalitiwa mapema tu?

Kwa wataalam wa masuala ya soka na wenye jicho la uchambuzi ni mchezaji yupi atakuwa wa kwanza kupewa "Thank you" na timu yake kwa hawa wachezaji wawili?
Huyo Skudu miye simkubari hata kidogo show off tembo mpira sungura
 
Lengo lako lilikua kumzungumzia Skudu na sio Onana hilo linajidhihirisba kwenye Uchambuzi wako.

Na kingine utakua Mpuuzi na Jinga la Kupindukia kama Skudu utampima kwa Dakika 7 za Community shield au zile dakika za Yanga Day.

The same kwa Onana utakua Fala na zwazwa kama utamzungumzia na kumkosoa kisa zile dakika z Simba Day na Hizi za Community shield.

Bado wana mda tulia acha kuandika ili ujaze thread ambazo zinaonyesha ujinga wako.
 
Unataka tathmini ya nini na wakati ligi bado haijaanza! Wewe ndiyo unaueleta porojo. Maana huwezi kufanya evaluation kwa mchezaji aliyecheza mechi moja tu ya Ngao ya Jamii.
Tanzania tunawajinga wengi mkuu mtu ana anza kutaka Evaluation kupitia Dakika 7 za mchezaji duuuh!!
Ndio maana hua wanapigwa sana Makolo kwenye swala la Usajili.
 
Back
Top Bottom