Ondoa ''misconception'' kuhusu Wanyarwanda

Mkuu kuna watu hapa utaumiza akili na kila kitu wanavuga wanafahamu kumbe hata kutembea hawajatembea. Kipindi sijasafiri na kuja huku niliko kwa sasa (kimatembezi) nilikuwa natembelea Kampala ambapo Wanywaranda wapo kibao japo kuna kabila la Wanyankore (analotoka Mseveni),hawana noma kabisa wala malingo na wanaheshimu watu pia mama yangu ni mwenyeji wa Biharamulo (Msubi) huko ndiko unaweza kujifunza ukarimu wao,ukiomba maji unapewa maziwa. Karibu Durban kwa leo
 
Wazingue ndio utajua rangi yao.
 
Nashukuru sana kwa mawazo yako, umeongelea tatizo la kutosafiri, tatizo la kufikiria kwamba kile kitu ambacho mtu anakifahamu ndio kila kitu. Opinions za watanzania wengi ni sheria, kwani kwa mawazo yao zinapaswa kusikilizwa na kufanyiwa kazi. Asante kaka kwa picha nzuri
 
Pengine ufananishe Rwanda na Mkoa wa Kigoma. Serikali ya Rwanda inanuka damu na dhuluma kwa wahutu iliyowaua na kwa madini wanayoyiba huko DRC.

Please saidia ufafanuzi hapo pa kufananisha na Mkoa wa Kigoma huku unazungumzia dhuluma, mauwaji na wizi wa madini.

Kigoma nao wanafanya kama haya wanayoyafanya Rwanda?
 
Mada pana hii tena ina utata mwingi na kila mtu anachangia kwa uelewa wake na mleta uzi sijui by chance au coincidence kakutana na ukarimu huo.Ila watu wa mipakani wanawajua uzuri watu hao walivyo unaweza kushangaa unakutana kama 8 hivi barabarani wanatembea kumbe wenzio wapo mkutanoni walifika njia panda kila mtu ana elekea kwake mkutano umeisha ni watu wa kutunza vitu kwa muda mrefu kujithamini wao kupita kiasi dharau ndo nyumbani kwake hapo unafiki na kujipendekeza kwa wenye mamlaka hapo umefika.Kiongozi kama kiongozi ana ubaya na uzuri wake kagame kuna mambo mengi ya msingi kawafanyia watu wake ule uhutu na ututsi haujaisha upo kwa mbali na wengi wenye mamlaka ni tutsi coz baada ya genocide wengi walikimbilia uganda tanzania hata kenya achilia mbali ulaya na %kubwa upstairs wapo uzuri so alipochukua nchi kagame akawaita kuhusu kina nyamwasa na kalegea jamaa baada ya kuchukua nchi wakataka yale mambo ya kuhodhi madaraka pk ndipo alipo kosana nao simpendi kagame kwa dharau zake na hila anazo wafanyia wakongo kwa kuiba na kufanya congo pawepo na vurugu ila kwa upande wa pili anafanya mema kwa nchi yake .
 
ni bora yule anayeenda kuiba kwa ajiri ya watu wake kuliko hawa ambao wanacho lakin wanagawa bwelele kwa wazungu
Kabisaa baba mzuri ni yule anayethamini familia yake sio yule anayetesa na kuilaza njaa familia yake wakati ana Mali nyingi
 
Mh! Nna wasi wasi, Niwie radhi ndugu yangu hamna kauhusiano pengine umeoa kwao au wameoa kwako? maana ulivyo wapamba ni tofauti sana na ninavyo wasikia.
 
Mkuu Msumeno, uko sahihi kabisa kuhusu hao watu raia wa Rwanda.

Najiuliza tu, sijui kama ingekuwa Mombasa hizo ofa ungezikubali na kuleta uzi hapa kwamba watu wa Mombasa ni wakarimu, na majibu ambayo ungeyapata kama yangeshabihiana na haya unayopata sasa. (nawalenga wachangiaji wenye mihemko)

Sema (sisi watanzania) tunakuwa na mitazamo ya karibu, ya mtupo wa jiwe na ukute mtu mwingine anachangia hapa wakati hajawahi kukaa na mnyarwanda sehemu yoyote wala kuwahi kufika Rwanda
 

Umejitahidi sana lakini bado huwezi kudanganya watanzania wanaojua mbinu zenu.

1. Huyo genius wako (sio genious 😛) ndio aliyeanzisha vita mwaka 1990 mpaka 1994, huyo genius wako ndio aliyeua majority ya hao waliokufa 1994, huyo genius wako ndio aliyechinja maelfu ya wahutu mwaka 1995 pale Kibeho ndani ya Rwanda, huyo genius wako ndio aliyesababisha vifo vya watu milioni 6 DRC, huyo genius wako ndie aliyepindua Rwanda, Congo DRC na sasa anataka kupindua Burundi. Kama huyo Kagame ni genius kwako basi sawa. Si tunachojua ni kuwa hata form 6 hajafika....
2. Hivyo viwanja na mengineyo yote kavikuta: Who brought development in Rwanda?
3. Kagame hana bahati kuwa wanyarwanda sio watu biased. Kagame anatawala kimabavu watu hawamtaki. Na ukome kusema "sisi tuna akili za kipumbavu". Wapumbavu ni nyinyi mnaopigana kila siku kwa sababu ya pua zenu, tuliwapa uraia nchini kwetu toka miaka ya 1960. Watch what you say about us. Tukiamua kuanza upumbavu utajikuta pabaya.
4. "Rwanda itakuwa mbali zaidi yetu" based on what exactly? watu wenu wanakimbia nchi yenu wanakaa maporini kwetu!

Nice try though, hii ID ya ngapi?
 

Jione unavyojiumbua, kumbe unajua tunamshambulia kagame lakini nyinyi mnasema tunawashambulia wanyarwanda! Kwani Kagame ndio wanyarwanda wote? Tulimpompiga Iddi Amin waganda walituchukia? Na je watanzania ndio watu pekee tunaomchukia kagame? Huko DRC alikokaa mleta mada, hakuona wala kusikia wacongo walivyokata mauno kwa furaha waliposikia tetesi kuwa Kagame kafa?
Na je kwa nini unadai ni 'dhana potofu' kumshambulia Kagame? Katika mambo ambayo Kagame anashutumiwa wewe umejibu mangapi ambayo ni potofu?
 
Sema wanaheshimu watutsi walio kila kona ya dunia hii. Ndio maana wamejazana kwenye uongozi katika nchi ambayo wao ni watu wawili kati ya 10! Pili takwimu za Rwanda ni za kupikwa, ndio maana huoni watanzania wanahamia Rwanda kiharamu kufuata hizo elimu na afya ambazo supposedly mmetupita. Badala yake hapa bongo mpaka madada poa toka Rwanda wanakuja kutafuta soko kwa vile huko kwenu uchumi mbovu, hamuwezi kumudu hata gharama za nanihii...
 
Zile radio za rwanda ambazo zilichochea mauaji mbona huziongelei?. Watutsi mamilioni waliouliwa kinyama na miili yao ikawa inaeleka katika mto Kagera nao umewasahau?. Nimemuongelea Kagame katika angle ya economic reforms alizozisimamia kwa umahiri mkubwa. Na sio kweli kwamba Kagame ameyakuta maendeleo, amefanya kazi kubwa ya kuweka masuala ya kisiasa pembeni na kufanya kazi za kiuchumi kwa faida ya wote. Kaka ukubali wala usikubali there is something wrong with our mentality, inategemea na uwezo wako wa kuyaona mambo. Ninayeongea na wewe sio mtutsi ni Mtanzania ambaye mzazi wake alifanya kazi serikalini tangu 1962 kafanya mengi sana, marehemu Mama yangu ni mmoja wa walimu wa kwanza wa shule ya msingi mzimuni pale magomeni, alikuwa pale mwaka 1965. Nimekulia Dar tangu utoto wangu miaka ya 70 mwishoni. Jaribu kuelewa concept ya mtu kabla hujaanza kutoka mapovu kwa hasira. Mimi ni mtanzania kama wewe najaribu kujenga hoja, zielewe hoja kwa undani, usitangulize vitisho, najenga hoja, zitafakari na zijibu. Mimi ni mtanzania mwenye kujivunia utanzania kama wewe.
 
Kwa hiyo unataka kusema wanyarwanda mna hela kuliko watanzania? enhe mmetupita GDP kwa asilimia ngapi vile?
 
katika mada kama hizi wewe si wa kuamini hata kidogo, make tayari unamlengo wako na komenti zako zinatabirika
 
Kwa hiyo unataka kusema wanyarwanda mna hela kuliko watanzania? enhe mmetupita GDP kwa asilimia ngapi vile?
Kaka usitangulize jazba kwenye maongezi utaumiza moyo na akili yako. GDP na hela wapi na wapi?. Jaribu kutuliza kabisa akili unapojaribu kuchangia mada. Usiingie kwenye maongezi wakati una hasira zako binafsi, utaharibu maana nzima ya great thinkers.
 

1. Sio kweli kuwa upstairs wapo uzuri, wangekuwa wapo vizuri wasingepigana kwa sababu ya urefu wa pua zao na kuishia kuishi nchi za wengine kama wakimbizi.
2. Nyamwasa na Karegeya hawakuitwa na kagame Rwanda, wewe hata historia hujui. Nyamwasa na Karegeya wote wamezaliwa Uganda na wamekulia na kusoma huko. Wakati RPA wanavamia Rwanda mwaka 1990 ni Karegeya ndio aliyekuwa mpanga mipango. Jadili vitu unavyovijua tafadhali.
 
katika mada kama hizi wewe si wa kuamini hata kidogo, make tayari unamlengo wako na komenti zako zinatabirika
it doesn't matter mi hutoa facts and figures, nyinyi 'msiotabirika' kazi yenu kusifia uongo tu.
 
it doesn't matter mi hutoa facts and figures, nyinyi 'msiotabirika' kazi yenu kusifia uongo tu.
facts gani ambazo muda wote ni negative tu kwa side fulani?! hakuna kitu kama hicho asee, na hii tabia mnaambukizana sana na ndo maana hapa nchini utawala wa awamu ya nne chini kikwete unajadiliwa negatively tu hata ukileta mada ya iyo serikali iliboresha miundombinu kuna watu kama wewe badala ya kutoa big up mtaponda tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…