Ondoa ''misconception'' kuhusu Wanyarwanda


1. Radio iliyoanza uchochezi ni ile ya RPF iliyokuwa inatangaza kutoka Uganda iliitwa radio Muhabura, hii ndio iliyoanza uchochezi toka ianzishwe mwaka 1991!
2. Miili iliyoelea mto kagera aliitupa nani? Nafasi za mtoni hapo ni Kagame na majeshi yake ndio waliokuwa wamekaa! Muulize bosi wako Kagame hiyo miili aliitupa nani. Haiwezekani mtu amiliki Dar es salaam nzima halafu aulize nani anatupa miili coco beach! Huo ni upopoma!
3. Economic reforms. Nani aliyevurunda economy ya Rwanda? Kagame kavuruga uchumi wa Rwanda kwa miaka minne, halafu wewe unapima maendeleo kuanzia 1994? Kwa nini usipime maendeleo based on takwimu za Habyarimana alipoishia kabla ya yeye kupiga mabomu na kuvunja barabara ambazo leo wewe unadhani hazikuwapo?
4. Unaongea kana kwamba siasa ni adui na inatakiwa kukaa pembeni. You can't be serious. Bila siasa unaendeshaje nchi? Nchi bila siasa inaweza kuendeshwa kwa haki na Mungu tu. As long as binadamu ndio wanaishi kwenye hiyo nchi siasa ni lazima. Ukiona mtu 'anaweka siasa pembeni' basi jua huyo hafai.
5. Kama wewe umekulia miaka ya 70 basi mama yako being a teacher should be ashamed of you. How can a grown man like you be so ignorant of history especially ya Kagame? Kutokana na mkataba wa Arusha wa mwaka 1993 majeshi ya kagame yalipewa ruksa ya kukalia eneo lote linalozunguka mto Kagera kwa upande wa Rwanda kuingia lake victoria. Sasa hiyo miili iliyoelea mwaka 1994 iliuliwa na nani? We ulikuwa mtu mzima miaka ya 90 kwa nini hujui mkwara ambao jeshi letu lilimpiga kagame kuhusu hiyo miili ya mto kagera iliyokuwa inakuja kwetu? You can choose to be anybody on social media kwa vile hatukuoni lakini siamini hata kidogo kunaweza kukawa na mtu mzima mtanzania anayeongea kama wewe.
 
Facts zikiwa negative zinageuka uongo au bado zinabaki kuwa za ukweli?
 
Kaka usitangulize jazba kwenye maongezi utaumiza moyo na akili yako. GDP na hela wapi na wapi?. Jaribu kutuliza kabisa akili unapojaribu kuchangia mada. Usiingie kwenye maongezi wakati una hasira zako binafsi, utaharibu maana nzima ya great thinkers.
Okaaay basi sawa tufanye GDP haina uhusiano na hela.😀
 
Kaka ujumbe wangu ni ule ule punguza jazba wakati unaongea na watu ambao huwajui vizuri. Nilijenga hoja ya kukwambia mimi sio mtutsi nikakupa historia ya wazazi wangu kwa ufupi tu. Wewe unakuja humu JF unajifanya unajua mambo ambayo kwa maandishi yako jinsi yalivyo, inaonyesha umesikiliza story za wakubwa zako, na story zenyewe unazileta humu zikiwa na makosa mengi ya details. Unadanganywa na watu kuhusu Kagame na wewe unaingia kichwa kichwa. Points zangu zinabakia pale pale kwamba mentality za kitanzania lazima zibadilike ikiwa tunataka kufika mbali. Kama moyo wako umeumia kwa sababu Kagame kapewa sifa anazostahili, sina cha kufanya kwa ajili ya kukuponya. Kagame licha ya madhambi yake mengi, bado ameweza kufanya vitu vingi wakati sisi tukiwa tumekwamba kwenye majibizano mengi ya wanasiasa. Tanzania yetu kila mtu anajua kila kitu, very wrong concept.
 
"Facts zikiwa negative zinageuka mihemuko" okay fine umeshinda!
kumbe uko mashindanoni?!
elewa kiswahili nimesema sio facts bali ni mihemko, yaani hizo unazoziona ni facts either ni positive ama negative kiuhalisia sio facts bali ni mihemuko yako dhidi ya unaowapinga
 
Meja rwegema unamjua?
 
Mkuu uko sahihi..binafsi Kigali ni mitaa yangu..unachosema sawa sawa nimekua kule 2010,nikarudi tena 2014,na mwaka huu nitakua huko..Mitaa yangu..Remera,Gahinga,kicycuro..viwanja vya bata,K club,KBC ,pwani Kivu mixer Gisenyi..Urakoze cyane
 
Nimekuelewa uzuri tatizo watu wana mihemko waqt ni mambo ya kujadiliana na sio kukashifianaso tuvumiliane ndugu humu wengi wetu hatujuani lakini mtu atataka akuelezee kama mnakaa mtaa mmoja sidhani kama kuna haja ya malumbano na kutoka penye mada all and all umeeleza unachoka jua big up sana ndugu yangu.
 
ungejua ninaombea muheshimiwa rais abadilishe katiba na atawale mpaka 2045 kubadilisha viongozi ni usumbufu tu.watanzania tunahitaji rais kama magufuli kwanza hii kasi aliyoanza nayo bado naona ni ndogo .aongeze tena mara tatu ili tubadilike maana tunaishi kwa mazoea.rwanda ni nzuri sana
 
Bukililo hili jina nalifananisha na kijiji/kitongoji kule kwetu Ngara
 
Rwanda jamani wale watoto tu hatari nimekaa remera pale watoto wa kike wapo very calm very sweet yani wazuri kuanzia rohoni kichwani hadi nje maji walikua wananichotea wao mda nikiwa busy sana nguo zangu wanafua wana roho nzuri sana asee i miss kigali sana tu
 
jMali ni Mnyarwanda wa kabila la Wahutu,anaonekana kuwa na hasira sana na Paul Kagame na Watutsi wote,sijui Kagame alimfanya nini huyu jamaa.Ananikumbusha jamaa yangu mmoja niliyepiga naye kitabu nchi flani alikuwa ni Mhutu,alikuwa na chuki kali na Watutsi.Ila kuna dada mmoja wa Kitutsi alikuwa bestie wangu sana,mtoto mrefu na mkali kinoma,alikuwa poa sana yule dada ila yule jamaa yangu wa Kihutu,ana misimamo mikali linapokuja swala la Watutsi yaani balaa.
 
Duh!unanikumbusha union trade pale wacha mchezo kila sampuli utaiona pale yaani inaweza kuja moja kisha kwa utashi wako unajisemea angepungua chini kidooogo angekuwa poa baada ya dakika kumi unamuona huyo uliekuwa ukimfikiria.
 
Yani huyu jamaa kauona ukarimu wa wanyarwanda kwa kua alinunulia supu na kusamehewa hela ya guest kwa muda aliongeza,sasa tujiuilize hizo ndo sababu tosha za kufanya mtu uone nchi flan ni nzuri pamoja na watu wake?
Ngoja nikwambie kitu ndugu yng,wanyarwanda wenyewe wanakubali wao ni sumu kwa yyte asie mnyarwanda yn ni km utamaduni wao,na huyo kagame unaemsema wenzio wanatamani hata kesho aondoke ila jamaa mfumo alioweka ndo mana husikii hata watu wakizungumza siasa hapo Kigali,
Halafu unaposema baada ya miaka10 Rwanda itaishinda Tanzania sijui unatumia vigezo gani au hujui mambo ya kiuchumi yalivo kaka.Rwanda haitakaa iizidi Tanzania hata siku moja na wao wanajua hivo ila kinachobaki ni kujitutumua tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…