jMali
JF-Expert Member
- Nov 9, 2010
- 8,404
- 4,973
Zile radio za rwanda ambazo zilichochea mauaji mbona huziongelei?. Watutsi mamilioni waliouliwa kinyama na miili yao ikawa inaeleka katika mto Kagera nao umewasahau?. Nimemuongelea Kagame katika angle ya economic reforms alizozisimamia kwa umahiri mkubwa. Na sio kweli kwamba Kagame ameyakuta maendeleo, amefanya kazi kubwa ya kuweka masuala ya kisiasa pembeni na kufanya kazi za kiuchumi kwa faida ya wote. Kaka ukubali wala usikubali there is something wrong with our mentality, inategemea na uwezo wako wa kuyaona mambo. Ninayeongea na wewe sio mtutsi ni Mtanzania ambaye mzazi wake alifanya kazi serikalini tangu 1962 kafanya mengi sana, marehemu Mama yangu ni mmoja wa walimu wa kwanza wa shule ya msingi mzimuni pale magomeni, alikuwa pale mwaka 1965. Nimekulia Dar tangu utoto wangu miaka ya 70 mwishoni. Jaribu kuelewa concept ya mtu kabla hujaanza kutoka mapovu kwa hasira. Mimi ni mtanzania kama wewe najaribu kujenga hoja, zielewe hoja kwa undani, usitangulize vitisho, najenga hoja, zitafakari na zijibu. Mimi ni mtanzania mwenye kujivunia utanzania kama wewe.
1. Radio iliyoanza uchochezi ni ile ya RPF iliyokuwa inatangaza kutoka Uganda iliitwa radio Muhabura, hii ndio iliyoanza uchochezi toka ianzishwe mwaka 1991!
2. Miili iliyoelea mto kagera aliitupa nani? Nafasi za mtoni hapo ni Kagame na majeshi yake ndio waliokuwa wamekaa! Muulize bosi wako Kagame hiyo miili aliitupa nani. Haiwezekani mtu amiliki Dar es salaam nzima halafu aulize nani anatupa miili coco beach! Huo ni upopoma!
3. Economic reforms. Nani aliyevurunda economy ya Rwanda? Kagame kavuruga uchumi wa Rwanda kwa miaka minne, halafu wewe unapima maendeleo kuanzia 1994? Kwa nini usipime maendeleo based on takwimu za Habyarimana alipoishia kabla ya yeye kupiga mabomu na kuvunja barabara ambazo leo wewe unadhani hazikuwapo?
4. Unaongea kana kwamba siasa ni adui na inatakiwa kukaa pembeni. You can't be serious. Bila siasa unaendeshaje nchi? Nchi bila siasa inaweza kuendeshwa kwa haki na Mungu tu. As long as binadamu ndio wanaishi kwenye hiyo nchi siasa ni lazima. Ukiona mtu 'anaweka siasa pembeni' basi jua huyo hafai.
5. Kama wewe umekulia miaka ya 70 basi mama yako being a teacher should be ashamed of you. How can a grown man like you be so ignorant of history especially ya Kagame? Kutokana na mkataba wa Arusha wa mwaka 1993 majeshi ya kagame yalipewa ruksa ya kukalia eneo lote linalozunguka mto Kagera kwa upande wa Rwanda kuingia lake victoria. Sasa hiyo miili iliyoelea mwaka 1994 iliuliwa na nani? We ulikuwa mtu mzima miaka ya 90 kwa nini hujui mkwara ambao jeshi letu lilimpiga kagame kuhusu hiyo miili ya mto kagera iliyokuwa inakuja kwetu? You can choose to be anybody on social media kwa vile hatukuoni lakini siamini hata kidogo kunaweza kukawa na mtu mzima mtanzania anayeongea kama wewe.