Ondoa ''misconception'' kuhusu Wanyarwanda

Ondoa ''misconception'' kuhusu Wanyarwanda

Mkuu, hapo katika namba 3 umenistaajabisha saaaana!! tena umenifurahisha kusema ukweli :-- msumeno Ukweli wako ni shuhuda na funzo Kwa wapendao Amani,Haki na matendo mema..!! Yaani siajaabu hiyo huduma haipatikani hapa kwetu japo kuwa WaIslamu tupo wengi kila mtaa...!!! LAZIMA TUJIFUNZE hatujachelewa...
 
Waungwana kaka yenu nakaribia kurudi nyumbani baada ya kuishi hapa DRC kwa Takriban miaka 2.

Katika kipindi chote nilichokaa hapa nimejifunza mengi sana ila leo nitazungumzia kuhusu hawa jirani zetu Wanyarwanda.Maana nimekua nikipita hapa mara kwa mara. Kwa kifupi ondoeni dhana potofu kuhusu hawa jamaa maana mimi dhana hiyo tayari nimesha ifuta. Wengi wenu kama sio wote mnadhani kuwa wanyarwanda ni watu ''wasio poa'' au ni wenye majivuno labda wengine mnadhani eti hawatupendi Watanzania.

Dhani hizi ni potofu kweli kweli, mwanzoni nikipita hapa sikua nikiongea kiswahili ili nisitambulike maana niliogopa kweli hawa jamaa. Baadae nikagundua dhana yangu sio sahihi kabisa na Mungu anisamehe.

Hawa jamaa hawana shida kabisa na wageni hasa Watanzania. Nimekaa Hoteli mbali mbali hapa nikiwa transit kwenda DRC au kurudi Home Tanzania, na kote huko nimechukuliwa vizuri sana tu.

Sio hotel tu , nimepanda boda boda, nimefika masokoni, msikitini , madukani kote huko hawa jamaa ni wakarimu sana na nimetendewa vizuri kwa kweli.

Wacha niweke mifano michache hapa mnielewe, nasisitiza michache mana nimengi nimeyaona positive.

1. Nikitoke DRC kurudi home ( niko njiani) tukiwa pale Kingarama Restaurant nikapata shida kidogo ya chenji ya Dollar kwa FRC ya Rwanda ili nipate Supu, wakati nikitaka kutoka nikatafute nje chenji mzee mmoja akasema kumwambia mhudumu mwache apate hiyo supu nitalipa mimi kama 'felistation' maana walitufunga kombe la CHAN huyu mzee alijua mimi ni Mkongo, nikala na wala hakukaa kuni bore kwa vile ameninunulia supu alitimua.... nikashangaa maana DRC husema hawa jamaa hawawapendi

2. Mh PK alitoa ma Bus kadhaa kuja pale Gisenyi kuchukua mashabiki wa DRC bure ili waje washangilie timu yao .... BUS zilijaa wakongo na walilindwa na wakarudi kwa amani.

3. Nilipofika Kigali na baada ya kuchukua Hotel, nikataka kwenda Masjid kusali , nikauliza Reception , kwa mshangao akadakia jamaa mmoja na kuniambia ''msikiti uko mbali ila subiri nitakupeleka maana naelekea njia hiyo hiyo huyu hakua musilam na hakua akinijua , ni tax man tu alie leta mteja pale. Njiani tulipiga soga sana.

4. Nikiwa hapa kwa siku ya pili na ticketi yangu ikiwa ya jioni nikaona ni negotiate nikae mpaka jioni kwa kulipa kidogo chumba maana check out ni saa tano asubuhi... Manager akasema ''kaa tu usilipe chochote , karibu tena wakati mwingine''.

5. Huko mitaani niliko kwenda kutembea jana usiku, nilikutana na ukarimu sana hasa unapouliza direction na mengine. hawa jamaa wana smile sana na sio ya smile ya kinafiki au ya kutegemea kitu

(a) Kitu nimegundua labda unaweza sema cha kushangaza au sio kizuri ni kwamba watu hapa hawaongelei siasa sana , ni aghalabu kukuta watu wakiongelea siasa hapa tofauti na home TZ kila mtu politician

(b) Printing media sio nyingi ila TV station wanazo nyingi tu

(c) Polisi ni vijana na hawacheki cheki wako serious kweli ila ukiuliza kitu wanakujibu vizuri tu

(e) Rushwa hapa sio sana labda niseme hakuna, polisi akikumata unaandikiwa charge hakuna zile za kuvutana nyuma ya gari na watu wanatii sheria kweli kweli

(f) Ule mfumo wa ukusanyaji kodi kila duka hapa, na kuna ka machine kama ka fingure print sijauliza ni ka nini ila ni ka mamlaka ya Kodi ya Rwanda. ( hapa nikakumbuka zile machine zetu sijui zilishia wapi maana zilileta sintofamu)

(g) Taxi zina Automatic Counter kama za Europe

NIMEONA MENGI WACHA NIACHIE HAPA NA WENGINE WACHANGIE MAANA NATUMAINI KUNA WENGI WAMEPITA HAPA PIA, WITO WANGU KAMA UNA JIRANI YAKO MNYARWANDA USIMTENDEE VIBAYA HAWA WATU WENGI WAO NI WAZURI SANA KWETU

Ukiwachukia WANYARWANDA hasa Watutsi utakuwa na MATATIZO MAKUBWA YA AKILI. Asante sana mkuu kwa kuweka UKWELI kuhusu WANYARWANDA na kama nchi zote za AFRIKA zikiomba msaada wa FIKRA na MIKAKATI basi wasione aibu kuiomba RWANDA kutokana kwamba ndiyo nchi pekee ya AFRIKA iliyobarikiwa kila kitu na Mwenyezi Mungu. Long live RWANDA.
 
Rwanda wanajua madhara ya siasa za uhasama, hawataki kabisa kusikia mawazo ya kipumbavu kuhusu huyu ni mtutsi na huyu ni mhutu. Damu iliyomwagika mwaka 1994 na hata kabla ya hapo ni nyingi na huwa inawakumbusha umuhimu wa amani. Paul Kagame is a genious. Kaitumia CHAN katika kuitangaza Rwanda kimataifa. Kavitumia viwanja vinne kuandaa mashindano makubwa kabisa barani Afrika. Sisi tuna viwanja vinavyoendelea kuzeeka kama viwanda ambavyo vilitaifishwa enzi za Mkapa. Kagame anayo bahati kwamba wanyarwanda sio watu biased kama sisi Watanzania, wanyarwanda wanajenga akili za kimaendeleo, sisi tunajenga akili za kipumbavu za kutazamana kisiasa, yule mwanaCCM huyu mwana CHADEMA.

Rwanda ya miaka 10 ijayo itakuwa mbali zaidi yetu, lakini Rais Magufuli anao uwezo wa kuanza kuifanya Tanzania iwe katika spirit ya kuikimbiza Rwanda. Na alipokaa madarakani kwa siku chache tayari balozi wa Rwanda akaenda Ikulu kuongea biashara za kimataifa. Paul Kagame mtu mwenye progressive mentality, nasikia alimwambia rais wa awamu ya nne nipe bandari ya Dar nikuendeshee nchi yako. Afrika inahitaji viongozi wenye kuweza kuthubutu.
Mkuu yaani umeeleza nimekuelewa vizuri kweli......
 
Ninacho gundua tz ni wivu umewajaa hasa wadada wa bongo hawapendi kabisa wanayarwanda maana waliwafunika mbali sana kisura kiumbo wale watoto wazuri kuanzia nywele hadi unyayo tabia ni misconception tu mwakani naoa mtusi
 
Miaka itaebda itarudi mtusi na muhutu havitahiva. Ukitaka kujua nenda kwenye jera za Rwanda angalia zimejaa wahutu.
Ngoja nisiende mbali.
 
nawafananisha warwanda kwa waafrika mashariki kama wayahudi kwa waarab. vilevile warwanda kwa watanzania kama wana wa israel kwa wasaudia na iran
 
jMali ni Mnyarwanda wa kabila la Wahutu,anaonekana kuwa na hasira sana na Paul Kagame na Watutsi wote,sijui Kagame alimfanya nini huyu jamaa.Ananikumbusha jamaa yangu mmoja niliyepiga naye kitabu nchi flani alikuwa ni Mhutu,alikuwa na chuki kali na Watutsi.Ila kuna dada mmoja wa Kitutsi alikuwa bestie wangu sana,mtoto mrefu na mkali kinoma,alikuwa poa sana yule dada ila yule jamaa yangu wa Kihutu,ana misimamo mikali linapokuja swala la Watutsi yaani balaa.
Nyie extremists kila non-tutsi ni mhutu, kwa hiyo sioni ajabu. Kikwete na Salma ni wahutu, jacob zuma ni mhutu...
 
kumbe uko mashindanoni?!
elewa kiswahili nimesema sio facts bali ni mihemko, yaani hizo unazoziona ni facts either ni positive ama negative kiuhalisia sio facts bali ni mihemuko yako dhidi ya unaowapinga
Kwa hiyo facts huwa ni positive tu, zikiwa negative sio facts bali mihemuko? Doh umenishinda tena.
 
Kaka ujumbe wangu ni ule ule punguza jazba wakati unaongea na watu ambao huwajui vizuri. Nilijenga hoja ya kukwambia mimi sio mtutsi nikakupa historia ya wazazi wangu kwa ufupi tu. Wewe unakuja humu JF unajifanya unajua mambo ambayo kwa maandishi yako jinsi yalivyo, inaonyesha umesikiliza story za wakubwa zako, na story zenyewe unazileta humu zikiwa na makosa mengi ya details. Unadanganywa na watu kuhusu Kagame na wewe unaingia kichwa kichwa. Points zangu zinabakia pale pale kwamba mentality za kitanzania lazima zibadilike ikiwa tunataka kufika mbali. Kama moyo wako umeumia kwa sababu Kagame kapewa sifa anazostahili, sina cha kufanya kwa ajili ya kukuponya. Kagame licha ya madhambi yake mengi, bado ameweza kufanya vitu vingi wakati sisi tukiwa tumekwamba kwenye majibizano mengi ya wanasiasa. Tanzania yetu kila mtu anajua kila kitu, very wrong concept.
jazba hapo iko wapi? nimekupa facts kujibu facts zako feki. Umeongea redio, umeongea maiti mto kagera, umeogea economic reforms...yote hayo nimeyapangua with facts, lakini wewe unasema ni jazba. wewe unapoongea uongo ili kumsifia kagame kwa kila hali tukuite una nini? Mahaba?
Hebu taja mambo ambayo sisi tumekwama kutokana na hicho unachokiita siasa ambayo Kagame amefanya kutokana na kuweka siasa pembeni.
 
ungejua ninaombea muheshimiwa rais abadilishe katiba na atawale mpaka 2045 kubadilisha viongozi ni usumbufu tu.watanzania tunahitaji rais kama magufuli kwanza hii kasi aliyoanza nayo bado naona ni ndogo .aongeze tena mara tatu ili tubadilike maana tunaishi kwa mazoea.rwanda ni nzuri sana
Kama Rwanda nzuri wakimbizi haramu wanafuata nini bongo 'kubaya'?
 
jazba hapo iko wapi? nimekupa facts kujibu facts zako feki. Umeongea redio, umeongea maiti mto kagera, umeogea economic reforms...yote hayo nimeyapangua with facts, lakini wewe unasema ni jazba. wewe unapoongea uongo ili kumsifia kagame kwa kila hali tukuite una nini? Mahaba?
Hebu taja mambo ambayo sisi tumekwama kutokana na hicho unachokiita siasa ambayo Kagame amefanya kutokana na kuweka siasa pembeni.
Mambo ambayo ni siasa ni mengi sana, mfano mpaka leo tuhangaika na umeme, Rwanda wana sera ya nishati inayoeleweka. Mpaka leo tuhangaika na elimu, Rwanda wako vizuri sana kielimu kuliko sisi. Mpaka leo tunahangaika na economic reforms, Rwanda wanaajiri waafrika wengi tu kwa sababu sera zao kiuchumi zimekuwa wazi na zenye kueleweka wakati sisi tunahangaika na mambo yetu mengi tu. Mpaka leo tuna bandari lakini ni mpaka aje Magufuli na kuyaweka mambo sawa tena baada ya watu wengi kupelekwa mahakamani ndipo tunakaa sawa, Rwanda hawana bandari na wanatushangaa kwanini tunalia na umasikini wakati tuna bandari. Mpaka leo Tanzania tunashindwa kuwatumia wataalam wetu wengi walio huko nje kwa faida ya uchumi wetu. Rwanda pamoja udogo wake wanayo network inayoeleweka linapokuja suala la wasomi wa kinyarwanda waliotapakaa duniani kote. Kaka sipendi kuongelea suala moja halafu wewe siku inayofuata inakuja kuniambia niongelee kitu kilichoongelewa jana. Samahani sana lakini kama unataka kuzungumza na mimi jitahidi tumalize mada moja ndani ya siku moja. Ni alama ya heshima

Unapokaa zaidi ya siku nzima halafu unakuja kuongelea kitu kilichoongelewa jana, inakuwa sio dalili ya heshima kwako na kwangu pia, naomba usirudie tena kurudia mada ambazo zimeshapitwa na muda wa kuzungumziwa.
 
1. Rwanda wana access ya umeme asilimia ngapi na sisi tuna ngapi? Jadili kisomi tafadhali.
2. Kuhusu elimu Rwanda wametuzidi nini labda. Maana ukicheki viongozi wao wengi walioendesha serikali katika ngazi za uwaziri kama prof Lwakabamba, donald kaberuka, oda gasinzigwa...wamesomea TANZANIA! Na hao wengine wote wamesomea nje na sio Rwanda! Hebu onyesha tumezidiwa vipi kielimu na Rwanda ikiwa wataalamu wanatoka UDSM kwenda Rwanda na sio vice versa. Hata vyuo vikuu kama KIST si vimekuzwa na Lwakabamba mwenye elimu ya UDSM? Unaongea nini wewe?
3. Sitaki kukusumbua kichwa chako kwa mada nyingine kama ulivyoomba, jibu hizo basi kwanza kisha tuendelee.
 
My friend tusisumbuane akili kama unaweza uka google then why should you tell me to tell you things that you can find by yourself. Mheshimiwa kama huna jambo la kufanya vuta shuka ulale. Hii ni mada ya juzi unaendele kuivuta kwa misingi ipi?. Tafuta la kufanya ufanye, hii mada sio mpya.
 
Aliyekwambia mimi siipendi Tanzania ni nani?. Aliyekwambia mimi sio mtanzania ni nani?. Naipenda nchi sana ndio maana naandika mawazo yangu ndani ya JF nikitegemea yatawagusa watu ili tubadilike kimitazamo, tuachane na dhana za kujiona we are the best, kiasi cha kushindwa kupiga hatua chanya za kimaendeleo.
Vipi mkuu wakeiii unawaonaje ukilinganisha na watizeed .
 
1. Rwanda wana access ya umeme asilimia ngapi na sisi tuna ngapi? Jadili kisomi tafadhali.
2. Kuhusu elimu Rwanda wametuzidi nini labda. Maana ukicheki viongozi wao wengi walioendesha serikali katika ngazi za uwaziri kama prof Lwakabamba, donald kaberuka, oda gasinzigwa...wamesomea TANZANIA! Na hao wengine wote wamesomea nje na sio Rwanda! Hebu onyesha tumezidiwa vipi kielimu na Rwanda ikiwa wataalamu wanatoka UDSM kwenda Rwanda na sio vice versa. Hata vyuo vikuu kama KIST si vimekuzwa na Lwakabamba mwenye elimu ya UDSM? Unaongea nini wewe?
3. Sitaki kukusumbua kichwa chako kwa mada nyingine kama ulivyoomba, jibu hizo basi kwanza kisha tuendelee.

Mkuu usihangaike sana kwa mambo yaliyo dhahiri.
Dr. KIKWETE aliwahi kusema " Kama Tz ingekuwa Rwanda basi tungesambaza umeme mpaka kwenye matendegu ya vitanda"
 
Back
Top Bottom