Mwanaume wa miaka 32 amekamatwa Nairobi baada ya kudaiwa kutoa matamshi yaliyowalenga raia wa Burundi wanaoishi na kufanya kazi Kenya, katika kipindi ambacho mjadala kuhusu wafanyabiashara wa kigeni tayari umeibua hofu miongoni mwa baadhi ya wahamiaji.
Kwa mujibu wa DCI, Kevin Odiwuor Otieno, anayejulikana pia kama Engineer Kevin, alitoa matamshi hayo katika mkutano wa Bunge la Mwananchi katika Jacaranda Grounds, Kayole. Video iliyosambaa mitandaoni inadaiwa kumuonyesha akiwashutumu Warundi kwa kuchukua nafasi za biashara za Wakenya na kuwapa saa 24 kuondoka nchini, huku akionya kuhusu madhara kwa watakaobaki.
DCI sasa inachunguza kama matamshi hayo yanafikia kiwango cha hate speech au incitement.
Lakini tukio hili linatokea katika mazingira nyeti. Baada ya maagizo ya serikali kuhusu wafanyabiashara wa kigeni, mamia ya Warundi waliripotiwa kufika katika ubalozi wao Nairobi wakitafuta nyaraka za kurejea nyumbani, baadhi wakisema wameanza kuhisi kutishiwa. Serikali baadaye ilisisitiza kuwa haitavumilia xenophobia na ikatoa dirisha la siku 90 kwa baadhi ya raia wa EAC wasio na nyaraka kurekebisha hali yao.
Katiba inalinda uhuru wa kujieleza, lakini Article 33 inaweka wazi kuwa uhuru huo haujumuishi uchochezi wa vurugu, hate speech au advocacy of hatred. Sheria ya National Cohesion and Integration pia inatambua chuki dhidi ya watu kwa misingi ya nationality kama sehemu ya ethnic hatred.
Wakati viongozi na wananchi wanazungumzia “foreigners taking our businesses,” nani anahakikisha mjadala huo haugeuki kuwa xenophobia?